Lowassa ataka Kikwete asaini kunyonga wauaji wa albino
Na Nuzulack Dausen na Pamela Chilongola,
Jumatatu,Aprili20
2015
Kwa ufupi
Kauli ya Lowassa imekuja wiki moja tu baada ya Rais
Kikwete kusema hajapelekewa majina ya watu 16 waliohukumiwa kifo
kutokana na mauaji ya albino kutokana na mlolongo mrefu wa kisheria
uliopo kabla ya kumfikia
Mwanasiasa huyo anayetajwa kutaka kugombea urais
katika Uchaguzi Mkuu ujao, aliuambia umati uliokusanyika katika viwanja
vya TCC Chang’ombe kuwa suala la ulinzi wa albino si la Serikali pekee
bali la wananchi wote.
Mapema Machi mwaka huu, Mahakama Kuu ya Tanzania
iliwahukumu watu wanne kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na kosa
la kumuua Zawadi Magindu (32) mwenye ulemavu wa ngozi, mkazi wa Kijiji
cha Nyamaruru, Wilaya ya Geita.
Kifungo cha CCM
Awali wakati akitoa hotuba yake Lowassa alisema
kutokana na kifungo alichowekewa na CCM hawezi kuzungumza mambo mengi
kwa sababu yatamletea balaa.
“Kule CCM bado nina kifungo, nikisema mengi
nitaleta balaa,” alisema huku akishangiliwa na kundi la vijana
waliokuwapo uwanjani hapo.
Lowassa yupo kifungoni na makada wengine watano
ambao ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari
Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard
Membe, Mbunge wa Sengerema William Ngeleja, Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika Stephen Wasira na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.
Aliyekuwa mbunge wa Temeke (CCM), John Kibaso
alisema Lowassa alikubali kuwa mgeni rasmi baada ya kumuomba aridhie
ombi hilo kutokana na mambo yake ya kisiasa yanayomkabili.
- Mbinu bora za Uandishi
- Uchaguzi mwezi Oktoba
- Mbinu za uandishi bora
- Kada CCM atinga na chopa ya Ndesa mkutanoni Moshi
- Moyo atimuliwa CCM Zanzibar
- Lowassa ataka Kikwete asaini kunyonga wauaji wa albino
- Wizi wa magari ni balaa tupu
- KOMBE LA SHIRIKISHO: Tumekosa wote
- KUTOKA LONDON: Usalama na kujipenda wewe na nchi yako- ndiyo siri ya nguvu zako Mtanzania
- KATIBA MPYA: Wingu linavyogubika hatima Mchakato wa Katiba Mpya
- Sitta: Huu ni mtaji wangu wa urais
- Aliyenusurika ajali ya Mbeya asimulia
- Mtaalamu kuwachambua makada wanaotajwa urais
- Vurugu Afrika Kusini zadaiwa kuua Mtanzania
- Mastaa 10 wenye mijengo ya maana Bongo
- Vita ya Serikali, madereva mbichi
- Polisi 20 wazingira nyumba ya Gwajima
- Chadema yaitaka Serikali kuangalia Watanzania waliopo A.Kusini
- Mwamvita Makamba anusurika kifo Afrika Kusini
- NYANZA: Mwalimu ajinyonga, mtendaji agongwa na kufariki papo hapo
- KOMBE LA SHIRIKISHO: Tumekosa wote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni