Waziri Mkuya ajikanganya
Na Mwandishi Wetu
Posted Alhamisi,Aprili30 2015 saa 11:1 AM
Posted Alhamisi,Aprili30 2015 saa 11:1 AM
Kwa ufupi
Juzi Mkuya alisema kuwa kipa umbele kwenye bajeti ya
mwaka 2015/16 kitakuwa kwenye suala la wafanyakazi na huduma za jamii,
akisisitiza kuwa bajeti haitajikita kwenye Uchaguzi Mkuu kwa kuwa suala
hilo lilishashughulikiwa kwenye bajeti inayomalizika.
Dar es Salaam. Ndani ya saa 24, Waziri wa Fedha,
Saada Mkuya ametoa kauli mbili zinazokinzana kuhusu fedha za Uchaguzi
Mkuu baada ya juzi kuliambia gazeti hili kuwa fedha kwa ajili ya
shughuli hiyo zilikwishatengwa mwaka jana, lakini jana akaziweka kwenye
mapendekezo ya bajeti mpya.
Juzi Mkuya alisema kuwa kipa umbele kwenye bajeti
ya mwaka 2015/16 kitakuwa kwenye suala la wafanyakazi na huduma za
jamii, akisisitiza kuwa bajeti haitajikita kwenye Uchaguzi Mkuu kwa kuwa
suala hilo lilishashughulikiwa kwenye bajeti inayomalizika.
Hata hivyo, kwenye bajeti ya 2014/15 suala la
Uchaguzi Mkuu limetajwa tu na hakuonekani kiasi cha fedha kilichotengwa
kwa ajili hiyo.
Akiwasilisha mapendekezo ya mapato na matumizi ya
Bajeti ya Mwaka 2015/16 jana, Mkuya alisema Sh22.4 trilioni zimetengwa
kwa ajili ya bajeti hiyo na kwamba Uchaguzi Mkuu umepewa kipaumbele cha
kwanza kati ya vinne vilivyopo.
Hata hivyo, Waziri Mkuya hakutaja asilimia wala
kiwango cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu, ambao
kikatiba unatakiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba.
Katika hali inayoongeza sintofahamu, Mkuya alisema
moja ya mafanikio yaliyopatikana katika Bajeti ya Mwaka 2014/15 ni
kufanyika kwa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu.
Alivitaja vipaumbele vingine kuwa ni kukamilisha
miradi inayoendelea, kuweka msukumo maalumu kwenye miradi ya umeme na
maji vijijini na kuimarisha rasilimali watu.
Alisema Serikali imepanga kutumia Sh16.7 trilioni
kwa ajili ya matumizi ya kawaida, Sh6.6 trilioni kwa ajili ya mishahara
ya watumishi wa Serikali na taasisi na Sh2.6 trilioni zitatumika kulipia
hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva.
Hata hivyo, Mkuya alishindwa kuweka wazi jumla ya
fedha zitakazotumika kwenye Uchaguzi Mkuu au kiasi kilichokwishatengwa
kwa ajili ya kazi hiyo mpaka sasa.
Akizungumza na Mwananchi jana, Mkuya alisema:
“Bajeti hii imezingatia pia maandalizi ya Katiba Mpya, Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa mwaka 2014 na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2015.”
Mapendekezo ya matumizi ya kawaida ya Serikali kwa
mwaka 205/16 pia yanaonyesha kuwa Mfuko Mkuu wa Serikali utatumia
Sh6.3trilioni, matumizi mengineyo wizarani Sh3.4 trilioni, matumizi
mengineyo mikoani Sh83 bilioni na matumizi mengineyo Mamlaka za Serikali
za Mitaa Sh208 bilioni.(source mwananchi)
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA)
imesitisha kwa siku 14 utozaji wa nauli mpya za mikoani zilizokuwa
zianze leo baada ya kupata maombi ya rejea kutoka kwa wamiliki wa mabasi
ya mikoani kutaka kuangaliwa upya nauli hizo zilizoshushwa.
Kutokana na hatua hiyo, wamiliki wa mabasi ambao jana walipanga kugoma walisitisha uamuzi huo hadi hapo serikali itakapotoa uamuzi kutokana na malalamiko yake hayo.
Aprili 15 mwaka huu serikali ilitangaza viwango vipya vya nauli ambavyo vilitarajiwa kuanza leo Aprili 30, mwaka huu kwa kushusha nauli za mabasi ya mikoani huku nauli za mijini za daladala zikibaki palepale.
Kwa mujibu wa kanuni za tozo za mwaka 2009 uamuzi kuhusu nauli hizo utafanyika baada ya siku 14 baada ya kusikiliza malalamiko yao na kamati maalum na kisha kutolewa maamuzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Giliard Ngewe aliliambia gazeti hili kuwa walipokea barua ya maombi ya rejea jana (juzi) ambayo ilikuwa siku 14 kisheria kwa wamiliki kupinga nauli hizo ka maandishi, na kama siku hiyo ingepita wasingesikilizwa.
Naye Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu alisema Serikali imetoa wiki mbili kwa Wamiliki wa Mabasi yaendayo mkoani (Taboa), kupeleka hoja yahesabu kwa nini wanasema nauli isishushwe.
Alisema tangu nauli ziliposhushwa mafuta na dola yameendelea kupanda.
“Tukishusha sisi ndio tutakaoumia kwa sababu hatuna duka letu la tairi, vipuri wala mafuta yetu wenyewe ambayo hayatatozwa kodi,” alisema.
Imeandikwa na Anastazia Anyimike na Lucy Ngowi (Chanzo:Habari leo)
JESHI la Polisi mkoani Rukwa limewakamata watuhumiwa 50 na silaha za
aina mbalimbali zikiwemo bunduki 48 , risasi 768 na maganda ya risasi
101.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Namanyere alionesha silaha hizo na risasi zake haradharani mbele ya waandishi wa habari.
Kamanda Mwaruanda aliongeza kuwa watuhumiwa hao na silaha hizo zilikamatwa kutokana na operesheni ya kupambana na visa vya ujangili na uhalifu mwingine katika maeneo ya Namanyere na kijiji cha Kirando mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani humo iliyofanyika kati ya Aprili 18 na 27 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda operesheni hiyo ilifanyika kwa ushirikiano wa Polisi mkoani humo, kikosi kazi taifa na askari wa wanyamapori wa pori la akiba la Lwafi wilayani Nkasi.
Alizitaja silaha zilizokamatwa kuwa ni bunduki aina ya AK 47 yenye namba 1162416 na risasi zake 409, bunduki nane aina ya rifle na risasi zake 83, bunduki 19 aina ya shotgun na risasi zake 138, bastola tano na risasi zake 133 na magobori 15.
Vitu vingine vilivyokamatwa ni pamoja na maganda ya risasi aina ya shotgun 96, maganda ya risasi aina ya rifle tano, magazini za bunduki aina ya SMG nne na vifaa vya kutengeneza bunduki za kienyeji ‘magobori’ mitutu sita.( chanzo:Habari leo)
Sumatra wasitisha nauli mpya kwa siku 14
- Last Updated on 30 April 2015
- By Waandishi Wetu
- Hits: 53
Kutokana na hatua hiyo, wamiliki wa mabasi ambao jana walipanga kugoma walisitisha uamuzi huo hadi hapo serikali itakapotoa uamuzi kutokana na malalamiko yake hayo.
Aprili 15 mwaka huu serikali ilitangaza viwango vipya vya nauli ambavyo vilitarajiwa kuanza leo Aprili 30, mwaka huu kwa kushusha nauli za mabasi ya mikoani huku nauli za mijini za daladala zikibaki palepale.
Kwa mujibu wa kanuni za tozo za mwaka 2009 uamuzi kuhusu nauli hizo utafanyika baada ya siku 14 baada ya kusikiliza malalamiko yao na kamati maalum na kisha kutolewa maamuzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Giliard Ngewe aliliambia gazeti hili kuwa walipokea barua ya maombi ya rejea jana (juzi) ambayo ilikuwa siku 14 kisheria kwa wamiliki kupinga nauli hizo ka maandishi, na kama siku hiyo ingepita wasingesikilizwa.
Naye Katibu Mkuu wa Taboa, Enea Mrutu alisema Serikali imetoa wiki mbili kwa Wamiliki wa Mabasi yaendayo mkoani (Taboa), kupeleka hoja yahesabu kwa nini wanasema nauli isishushwe.
Alisema tangu nauli ziliposhushwa mafuta na dola yameendelea kupanda.
“Tukishusha sisi ndio tutakaoumia kwa sababu hatuna duka letu la tairi, vipuri wala mafuta yetu wenyewe ambayo hayatatozwa kodi,” alisema.
Imeandikwa na Anastazia Anyimike na Lucy Ngowi (Chanzo:Habari leo)
Rukwa wakamata bunduki 50, risasi 768
- Last Updated on 30 April 2015
- By Peti Siyame, Sumbawanga
- Hits: 68
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda jana wakati akizungumza na waandishi wa habari Namanyere alionesha silaha hizo na risasi zake haradharani mbele ya waandishi wa habari.
Kamanda Mwaruanda aliongeza kuwa watuhumiwa hao na silaha hizo zilikamatwa kutokana na operesheni ya kupambana na visa vya ujangili na uhalifu mwingine katika maeneo ya Namanyere na kijiji cha Kirando mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani humo iliyofanyika kati ya Aprili 18 na 27 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaruanda operesheni hiyo ilifanyika kwa ushirikiano wa Polisi mkoani humo, kikosi kazi taifa na askari wa wanyamapori wa pori la akiba la Lwafi wilayani Nkasi.
Alizitaja silaha zilizokamatwa kuwa ni bunduki aina ya AK 47 yenye namba 1162416 na risasi zake 409, bunduki nane aina ya rifle na risasi zake 83, bunduki 19 aina ya shotgun na risasi zake 138, bastola tano na risasi zake 133 na magobori 15.
Vitu vingine vilivyokamatwa ni pamoja na maganda ya risasi aina ya shotgun 96, maganda ya risasi aina ya rifle tano, magazini za bunduki aina ya SMG nne na vifaa vya kutengeneza bunduki za kienyeji ‘magobori’ mitutu sita.( chanzo:Habari leo)
Wanazuoni wajadili mustakbali wa Tanzania ndani ya demokrasia ya vyama vyingi
Jaji Francis Mtungi akifungua mkutano wa wadau wa siasa wa uimarishaji demokrasia ya vyama vingi.
Dk. Benson Bana wa
Chuo Kikuu cha Dare s salaam ambaye amebobea katika masuala ya siasa
amewataka wadau wa siasa na wananchi kwa ujumla kuzuia uvunjifu wa amani
kuelekea uchaguzi mkuu kwa kufuata Sheria na kutobeza mamlaka.
Dk Bana alisema
hayo jana akijibu swali la msimamizi wa mdahalo wenye lengo la
kuimarisha demokrasia ya vyama vingi ulioandaliwa na Msajili wa Vyama
vya siasa kwa ufadhili wa UNDP, Profesa Bernadetta Killian.
Profesa Killian
alitaka kujua baada ya maelezo ya awali ya Dk Bana juu ya mtazamo wake
kuhusu ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania , nini
kinastahili kufanya kuepuka uvunjifu wa amani hasa katika muda huu
ambapo viashiria vipo.
Dk Bana alisema
kama watu hawatafuata utamaduni wa vyama vingi, utamaduni wa kufuata
sheria na kutobeza mamlaka, taifa litaingia katika machafuko.
Alisema watu kama
wanaona wanaonewa wanatakiwa kufuata taratibu na kama taratibu hizo
zinaonekana ni tatizo bado wanatakiwa kuwa na subira na kuondoa taratibu
hizo zenye matatizo kwa kufuata utaratibu.
Katika shauri hilo
la viashiria vya mizozo Profesa Rugumamu, aliyebobea katika masuala ya
kutanzua mizozo aliihimiza Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa
kutengeneza mfumo wa utambuzi wa viashiria vya hatari (early warning)
ili iweze kukabiliana navyo mapema.
Akizungumzia kama
Tanzania ni nchi ya demokrasia Dk. Bana alisema kwamba kuna maendeleo
makubwa yamepatikana tangu mtindo wa vyama vingi kuingia nchini miaka 23
iliyopita.
Alisema demokrasia haijengwi kwa siku moja, ina safari ndefu yenye milima na mabonde na wakati mwingine watu wasifike.
Mkurugenzi wa
Mkazi wa Shirika Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Philippe Poinsot
akizungumza na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa na kiraia
katika mkutano huo.
Aidha alisisitiza
kwamba demokrasia sio suala jepesi, lakini watanzania wanastahili
kujivuna kwa hatuha waliyofikia katika mambo mbalimbali ambayo hata
mataifa mengine ya Ulaya hayajafikia.
Alisema mwaka 1994
wakati taifa linaingia katika vyama vingi taifa lilikuwa na vyama 13
kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 1995 lakini sasa tunapozungumza kuna
vyama 22 vyenye usajili wa kudumu, wigo wa kuwania dola ukiwa umetanuka
zaidi.
Pia alisema
mafanikio mengine ni namna ambavyo vyombo vya habari vina nafasi kubwa
ya kuandika inavyoona sawa, japo kumekuwa na tukio la kufungiwa kwa
gazeti la Mwanahalisi, Mtanzania na Mwananchi, lakini kadhia hizo
haziondoi ukweli kuwa kumekuwepo na uhuru mkubwa wa vyombo vya habari.
Dk Benson Bana akizungumzia demokrasia ya vyama vingi.
Alisema taifa hili
halina sababu ya kuomba radhi kwa mafanikio yaliyopo na changamoto zake
katika siasa kwani uelewa katika masuala ya siasa unazidi kutanuka.
Alisema pamoja na
mafanikio hayo bado kuna mapungufu mengi hasa ya kutokuwa na utamaduni
wa vyama vingi, utamaduni unaoambatana na vyama kuwa na aidolojia
(itikadi), kukosekana kwa lugha za kistaarabu katika majukwaa ya siasa
na hata mitafaruku ya ndani ya kivyama.
Alisema kutanuka
kwa wigo wa ushiriki wa kuwania dola (vyama vingi vya siasa) kunatakiwa
kwenda sanjari na kujenga utamaduni huo wa kuimarisha ustawi wa
utamaduni wa vyama vingi.
Alisema pia kuna
haja ya kuimarishwa kwa taasisi zinazosaidia utamaduni huo kama Tume
huru ya Uchaguzi, Bunge na hata mfumo wa utawala ambapo wakuu wa mikoa
na wilaya wasiwe katika hali ya kikada bali wale wanaoweza kutekeleza
majukumu yanayostahili katika maeneo yao.
Jaji Mutungi akiteta jambo na Mkurugenzi UNDP, Bw. Poinsot.
Aidha alisema kwamba vyama vingi vya siasa vinafanyakazi ya uanaharakati badala ya kuwa na itikadi ya kuifuata .
Alizungumzia pia
haja ya vyama vya upinzani kujivunja na kuanzisha chama kimoja na
kutengeneza mkakati wa kutwaa dola huku akisema muungano wa Ukawa kwa
sasa una mushkeri zaidi badala ya kusaidia kujiandaa kutwaa dola.
Katika mdahalo huo
ambao ulielezwa na Msajili wa vyama vya Siasa jaji Francis Mutungi, si
mkusanyiko wa kufanya kampeni ya uchaguzi bali jukumu la ofisi ya
msajili hasa kuelekea uchaguzi mkuu, washiriki wake pia walielezwa
changamoto za siasa za vyama vingi.
Profesa Rugumamu
alisema kwamba katika tafiti aliyoifanya yeye na wenzake katika nchi 15
za bara la Afrika wamekumbana na changamoto takribani saba ambazo ni
kikwazo katika kupata na kukuza utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi.
Jopo la
wanazuoni kuanzia kulia Dk Bana, Profesa Meena, Profesa Rugumamu na
mwishoni ni msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.
Miongoni mwa
changamoto hizo ni vyama vikongwe na utamaduni wake kushindwa kuainisha
kati ya mamlaka ya dola na vyama vyenyewe, kuwepo kwa vyama vya kikanda
na kidini katika kipindi cha mpito katika demokrasia ya vyama vingi,
wanasiasa kubadili katiba waendelee kutawala, vyama na wanachama kutojua
haki na wajibu wao kutokana na kutofundishwa uraia tangu awali.
Pia alizungumza
uadui unaojijenga kwa nchi ambazo zimetoka vitani na uanzishaji wa
makundi ya ulinzi ya vyama ambavyo husababisha mitafaruku wakati wa
uchaguzi au kwenye uchaguzi na matumizi ya fedha yasiyojulikana kwa ama
kukosa sheria au sheria kuwapo na watu kutoizingatia.
Alisema dosari zote hizo zinatikisa ujenzi wa utamaduni wa demokrasia ya vyama vingi.
Awali
akimkaribisha Jaji Mutungi kufungua mkutano huo Mkurugenzi wa UNDP
nchini, Philippe Poinsot alisema Umoja wa mataifa umefurahishwa kwa
wadau wa siasa nchini Tanzania kuwa na mazungumzo yenye lengo la
kustawisha amani kuelekea uchaguzi na kutengeneza mfumo wa majadiliano
kama kukiwepo na kutokuelewana.
Alisema mkutano
huo walioufadhili ni sehemu ya makubaliano ya Ofisi ya Msajili na UNDP
kupitia mradi wake wa kuimarisha demokrasia (DEP) yenye kulenga kujenga
uwezo na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi na kuleta maelewano ndani
ya vyama na kitaifa wakati nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.
Msimamizi wa mdahalo Prof Bernadetta Killian.
Alisema ni matumaini yake kwamba mkutano huo utatengeneza mustakabari bora wa Tanzania kuwa na uchaguzi huru na wa amani.
Alisema kutokana
na ushindani, uchaguzi unaweza kuleta matata kwa hiyo ni vyema kama
wadau wataliangalia hilo na kuona namna ya kutanzua matata ili taifa
libaki na amani na kusonga mbele katika maeneo yote ya jamii.
Naye Jaji Mutungi
aliwaasa washiriki kutambua kwamba hakuna sababu ya kukamiana na
kukomoana miongoni mwa vyama vya siasa kwani wote wanajenga nyumba moja
na kimsingi hawana sababu ya kugombania fito.
Alitaka wadau kucheza mchezo wa siasa kwa maridhiano ili wasibomoe misingi ya amani ya taifa na mafanikio yake.
Alisema lengo la
mkutano huo ni kuweka sawa dhana ya demokrasia ya vyama vingi na
kutafuta majibu ya changamoto zinazokabili pasipo kuvunja amani ya nchi.
Profesa Ruth Meena akizungumzia ushiriki wa kijinsia katika demokrasia ya vyama vingi.
Profesa Rugumamu akizungumza.
Baadhi ya washiriki( SOURCE ZANZIBAR NEWS)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni