Kikoti.com

Kikoti.com: habari za uhakika

ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumamosi, 19 Desemba 2015

MAPENZI: mjue mwanamke bora

Na mwandishi wetu;Kijangai y
Wengi wangekuja na orodha isiyokuwa na mwisho ambayo inaeleza tofauti tofauti kuhusu tabia nzuri za mwanamke.

Hapa tumekuja na orodha ya sifa nzuri na muhimu zaidi ambazo zinafaa kutumiwa kama kuwa kigezo cha kupima tabia nzuri za mwanamke.
Kwa kuwa wanawake huwa na tabia tofauti tofauti, hatuwezi kusema lazima mwanamke awe na tabia zote hizi ili asomeke kama mwanamke mwenye tabia nzuri. La. hizi ni baadhi tu ya tabia ambazo mwanamke anaweza kuwa nazo, na nyingine kutokuwa nazo na bado akaorodheshwa kuwa na tabia nzuri. Zama nami.

Baadhi ya sifa nzuri kutoka kwa mwanamke

1. Kusamehe
Ni vigumu kuwa katika uhusiano halafu uwe hauna moyo wa kumsamehe mpenzi wako. Kawaida katika mahusiano, huwa kuna changamoto kadhaa ambazo hujitokeza hivyo lazima uwe na tabia ya kuweza kusamehe. Hii inaweza kuanzia kukosana kwa mambo ya kinyumbani, ama mambo mengine yanayofanana.
Mwanamke mzuri ni yule ambaye ana uwezo wa kumsamehe mpenzi wake bila kuweka kinyongo. Iwapo mpenzi wako umemshika katika fumanizi nk na bado unampenda, basi jambo zuri la kufanya ni kumsamehe na kuendelea na maisha.
2. Msikilizaji mzuri
Mara nyingi migogoro ambayo inatokea majumbani kati ya wapenzi wawili husababishwa na kutosikilizana. Huyu akiambiwa hivi huyu anajibu hivi. Well, iwapo mwanamke anataka mahusiano yake yake marefu na ya kufaana, basi anapaswa kuwa msikilizaji mzuri.
Mwanamke ambaye huwa anatulia na kumsikiliza mpenzi wake, mahusiano yake na mpenzi wake huwa ya furaha zaidi ukilinganisha na ya yule ambaye hatilii maanani maoni ya mwenzake.
3. Mwaminifu
Hii ni kuanzia kuongea ukweli bila kudanganya hadi maswala ya chumbani. Iwapo mwanamke ana mchepuko mahali fulani ama anamwendea kinyume mpenzi wake, basi aina hii ya tabia haifai kabisa.
Sifa ya mwanamke mzuri ni ile ambayo ni ya uaminifu. Mwanamke mwaminifu kwa mpenzi wake haitofika wakati fulani ambapo atakosana na mpenziwe.
4. Msaidifu
Katika mahusiano, kuna wakati fulani hufika ambapo lazima wapenzi wawili wasaidiane kufanya jambo ama kutimiza kitu fulani. Hivyo mwanamke mzuri ni yule ambaye anatoa msaada wa kumsaidia mpenzi wake na jambo fulani. Mathalan inaweza kuwa kumsaidia kimawazo, kifedha ama jambo tofauti. Mwanamke mwenye tabia hii humpendeza sana mpenzi wake kwa kuwa inaonyesha ya kuwa mwanamke kama huyu ana uwezo wa kumtumikia mpenzi wake wakati ambapo anaweza kupatwa na majanga.
5. Mwenye imani
Kuna tabia za wanawake ambazo huwachosha wanaume, nazo ni kukosa imani. Iwapo wewe una tabia za kutokuwa na imani basi tabia kama hio unafaa kuiacha mara moja. Tabia za kutokuwa na imani ni kama vile kuharakisha jambo, kulazimisha kitu ambacho hakiwezekani nk.
Hali kadhalika, mwanamke mwenye imani ni yule ambayo ana subira. Iwapo ameambiwa na mpenzi wake kuhusu jambo fulani, basi yeye hutulia hadi kungojea matokeo yake.
6. Kuhamasisha
Wanaume humpenda mwanamke ambaye anatoa motisha ili kumsaidia kutimiza lengo lake. Vile vile kwa kawaida kuna wanaume ambao wanahitaji kiinua mgongo ili kutimiza mambo fulani. Hivyo wewe kama mwanamke, mara moja au nyingine unafaa kuonyesha umotisha wako kwa kumuelekeza mpenzi wako mara moja au nyingine.
7. Mcha Mungu
Mwanamke mcha Mungu bila shaka maisha yake huwa ya kufanikiwa. Mtu yeyote yule lazima awe mcha Mungu ili awe na sifa nzuri ya maisha katika jamii.
8. Heshima
Heshima haimaanishi ni kwa mpenzi wako pekee bali kwa jamii nzima. Mwanamke ambaye anapenda kugombana na majirani kila kukicha halafu ikifika jioni anamheshimu mpenzi wake hafai. 
Tabia za mwanamke mzuri ni yule ambaye anaheshimu na kuishi na majirani zake vizuri bila kuwa na mivurutano yeyote ile.
9. Anajiamini
Mwanamke mzuri ni yule anajiamini na anaamini mahusiano yake. Mwanamke mzuri ni yule ambaye hatasikia maneno ya watu halafu akampakizia mpenzi wake. Iwapo kuna swala tata ambalo linafanyika, basi mwanamke aina hii atamwekea kikao mpenzi wake na kujaribu kumuuliza maswali na kutaka kufafanua chochote ambacho kitakuwa kinamkwaza. Mwanamke aina hii hupendwa na wanaume kwa sababu anajua ya kuwa akifanya jambo fulani basi mpenzi wake atataka kuelezewa bila kuwa na hisia zozote mbaya.
10. Anajua mapenzi
Ikija katika swala la mapenzi, mwanamke mzuri ni yule ambaye anaujua mwili wake vizuri, hivyo si mwoga wa kuonyesha sehemu yake ya ndani ya mapenzi. Mwanamke huyu haoni aibu ya kujaribu mitindo tofauti tofauti ya kufanya mapenzi nk.
Wanawake ambao wanajua mapenzi ni moja wapo wa sifa nzuri ambayo wanaume wanapenda.
Hizi ni baadhi tu ya sifa za mwanamke mzuri. Iwapo unataka kuongezea ama kuchangia, angusha comment yako hapo chini.
Imechapishwa na Unknown kwa 14:41:00 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

Ijumaa, 18 Desemba 2015

Ajali yaua 12 Iringa, 28 taabani

Basi la kampuni ya New Force baada ya kugongana

Imechapishwa na Unknown kwa 18:17:00 Hakuna maoni:
Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

Rwanda wafanya uamuzi


Friday, December 18, 2015

Kwa ufupi

  • Shughuli za kuapishwa wabunge Dodoma leo

    Habari Mpya
  • 1 Kitaifa Ajali yaua 12 Iringa, 28 taabani
  • 2 Kitaifa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar yaparaganyika
  • 3 Kitaifa Rwanda wafanya uamuzi
  • 4 Kitaifa Kasi ya mawaziri wa JPM watia shaka
  • 5 Kitaifa Waziri wa Afya ajiweka kitanzi kwa Magufuli
  • 6 Kitaifa Nyumba 100 zabomolewa Msimbazi
  • 7 Kitaifa Aga Khan aishukuru Serikali ya Uganda
  • 8 Kitaifa Wizara ya Afya yawasaka waliokaidi amri ya Magufuli
  • 9 Kitaifa Vigogo wa TRA kesi ya makontena nje
  • 10 Kitaifa Wataja mambo manne kuongeza kodi

  • Imechapishwa na Unknown kwa 17:38:00 Hakuna maoni:
    Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

    Kasi ya mawaziri wa JPM watia shaka






    Rais John Magufuli 
     Kwa ufupi

    Tangu walipoapishwa Desemba 12, mawaziri wengi wamekuwa wakitembelea taasisi zilizo chini yao kufuatilia utendaji na utoaji huduma kwa wananchi na kutoa matamko.
    By Fidelis Butahe na Kalunde Jamal

    Dar es Salaam. Licha ya mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano kutokaa ofisini wakishughulikia matatizo ya wananchi, wasomi bado wana shaka kuwa huenda kasi waliyoanza nayo ni ya muda na kwamba baadhi yao wanafanya kwa nidhamu ya woga.

    Tangu walipoapishwa Desemba 12, mawaziri wengi wamekuwa wakitembelea taasisi zilizo chini yao kufuatilia utendaji na utoaji huduma kwa wananchi na kutoa matamko.

    Mathalan, mara baada ya kuapishwa, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na naibu wake, Hamisi Kigwangalla hawakwenda ofisini na badala yake mmoja alikwenda Hospitali ya Amana na mwingine Hospitali ya Mwananyamala kukagua utoaji huduma.

    Ziara kama hizo zilifanywa na mawaziri wengi, ambao walifika sehemu zinazowahusu na kuhoji masuala kadhaa na baadhi kutoa muda ili wapewe majibu, wengine wakitangaza kusimamisha watendaji au kusitisha zabuni.

    Lakini wachambuzi waliohojiwa wametilia shaka kasi hiyo, baadhi wakisema mawaziri hao walihitaji kupata ripoti kutoka ofisi zao kabla ya kuanza ziara za ufuatiliaji na wengine wakienda mbali zaidi kusema kuna dalili za kutaka waonekane wanafanya kazi.

    “Kufanya kazi siyo kwenda mbio na kutoa maagizo lukuki kwa wakati mmoja. Kinachofanyika sasa ni kufuata maagizo zaidi kuliko utendaji wa dhati. Hali hiyo ipo katika ngazi zote na inasababisha baadhi ya watendaji kukiuka Katiba na sheria za nchi,” alisema mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Hamad Salim. Msomi huyo alisema nchi haihitaji mtu kujionyesha kuwa anafanya kazi. “Anayefanya kazi anatakiwa kutambuliwa na watu wanaomzunguka.”

    Katika kutekeleza kauli mbiu ya Rais John Magufuli ya “hapa kazi tu”, mawaziri wamekuwa wakifanya ziara hizo za ‘kushtukiza’ wakiwa wameambatana na waandishi wa habari na kuwahoji watendaji wa Serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu yao.

    Wakati Mwalimu na Kigwangalla walianzia hospitalini, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na naibu wake Dk Medard Kalemani wameanza kazi kwa kutembelea vituo vinavyozalisha umeme kwa kutumia maji.

    Muhongo, ambaye alishughulikia madini na nishati kwenye Baraza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Nne kabla ya kujiuzulu mapema mwaka jana, alitumia fursa hiyo kueleza mikakati yake na kutoa maagizo kuwa kila mteja aliyeomba kuunganishiwa umeme na hahitaji nguzo, afanyiwe hivyo.

    Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akikutana na wadau wa maji, kutembelea Ruvu pamoja na Dawasa.

    Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga alianzia ofisini kwake akipokea taarifa ya ndani na juzi alikuwa na kikao na maofisa wa polisi huku akiwataka kutoa taarifa za sababu ya Jeshi la Polisi kutolinda Bandari ya Dar es Salaam, kazi inayofanywa na kampuni binafsi.

    Naye Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo alikuwa wilayani Bahi ambako alikutana na tatizo la utoro wa watendaji wa Halmashauri ya Bahi.

    Tofauti na mawaziri wengine walioamua kufanya ziara za kushtukiza, Mwigulu Nchemba anayeongoza Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, alilazimika kusafiri kwenda Mvomero, Morogoro baada ya kutokea mapigano kati ya wakulima na wafugaji, yaliyosababisha mtu mmoja kufariki, wanne kujeruhiwa na ng’ombe 72 kuuawa.

    Lakini alipofika huko aliahidi kushughulikia matatizo ya wakulima na wafanyakazi huku akiwaomba wananchi hao waache kujichukulia sheria mkononi.

    Jenister Mhagama, ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, pia alilazimika kutoka ofisini baada ya mvua iliyonyesha kwa kipindi kisichozidi saa nne, iliposababisha mafuriko jijini Dar es Salaam.

    Waziri huyo aliagiza kusitishwa kwa zabuni ya mkandarasi wa mfereji wa Buguruni na kutaka maelezo ya ujenzi wa mfereji wa Boko Basihaya.

    Wanatumia nguvu nyingi

    Lakini wachambuzi wanaona kuna nguvu kubwa inatumika ambayo inaweza kutoa matokeo madogo.

    “Mtu akipewa kazi ya kukata mti mkubwa, atakaa siku sita mezani akipanga jinsi ya kuukata,” alisema mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (Sua), Profesa Damian Gabagambi, akimnukuu Rais Barack Obama wa Marekani.

    “Utendaji wa kulipuka utatumia nguvu nyingi na kuleta matokeo madogo kwa sababu maeneo yanayohitaji kurekebishwa na kufanyiwa kazi ni mengi na yanahitaji upeo wa kina kuyafahamu, kwanza kwa kushirikisha wataalamu na wadau ili kujadili na kupata ufumbuzi wa pamoja,” alisema Profesa Gabagambi.

    Lakini mtaalamu wa mambo ya Katiba, Profesa Ruth Meena alionyesha shaka kama utendaji huo ni nidhamu ya kazi au ya woga.

    “Kuna vitu viwili; nidhamu ya kazi na nidhamu ya woga, hivyo inahitaji muda kulibaini hilo. Siwezi kusema mengi kuhusu utendaji kazi unaoonyeshwa na walioteuliwa kwa sababu siamini katika vitu vya mbiombio na tabia ya mtu ya kupenda kazi huonekana bayana, muda utaeleza yote.

    “Wapewe muda na mimi nawapa muda pia tuone. Wenye nidhamu ya woga na nidhamu ya kazi wataonekana tu, hawatajificha.”

    Mhadhiri wa OUT, Hamad Salim alisema mawaziri hao wanafanya kitu ambacho hakitokani na utashi wao, bali kuiga uchapakazi wa Rais.

    “Nafikiri tunahitaji kubadili sheria na taratibu mbalimbali ili kuendana na mfumo uliopo wa kuchapa kazi. Kinachofanyika sasa si sawa. Lakini wasaidizi wa Rais hawafanyi kazi kwa utashi, wanafanya kwa amri na kuimba wimbo wa mtu mwingine wakijiaminisha kuwa ni wimbo wao.”

    Hoja ya mfumo pia ilizungumziwa na Profesa Bakari Mohammed wa UDSM: “Ili kuwe na utendaji kazi endelevu, tunatakiwa kuwa na mifumo itakayofanya utendaji kazi wa kasi walioanza nao uendelee hata kama Rais Magufuli ataondoka madarakani,” alisema.

    Alisema yanatakiwa mabadiliko ya sheria na kanuni na kuwe na Katiba yenye maelezo ya utendaji kazi wa mawaziri.

    Alisema hata Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete naye alianza na kasi kubwa, lakini kutokana na utendaji kazi kutokuwapo kimfumo, ilifikia mahali kasi ikashuka na kuwa ndogo.
    Imechapishwa na Unknown kwa 17:14:00 Hakuna maoni:
    Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

    Jumamosi, 8 Agosti 2015

    USIKU KUNA MAMBO: SIMULIZI YA MAPENZI






    Kuna siku nilikuwa maeneo ya Mjini kati (City Center), nikaipenda suruali moja ya shilingi 15,000/= na pesa sikuwa nayo ikabidi niende kutoa kwenye ATM ya Postal.
    Nimefika pale sikukuta mtu hivyo niliingia moja kwa moja, nimefika mle ndani nikakuta Pesa Kibao zimemwagika pale kwenye kitundu cha kutolea pesa, ATM Card ilikuwepo pale imetokezea na Pembeni kulikuwa na Pochi ya Kike iliyoonekana kutuna vilivyo.
    Kwa woga mimi huku nikitetemeka mapigo ya moyo yakiwa yameongezeka nikatizama nyuma yangu sikuona mtu, nikachukua zile Pesa harakaharaka, ATM na ile pochi.
    Ile natoka nje kuna dada mmoja alikuwa anakuja kwa kasi maeneo yale nikapata uoga nikamuuliza “Samahani dada, kuna kitu umesahau humu”, yule dada hakunijibu kitu kaingia kwenye chumba cha ATM akachomeka Kadi kutoa hela mi nikaondoka zangu fasta kuelekea home.
    Nimefika home nikajifungia ndani na kuzibwaga zile pesa kitandani, nikafungua wallet nikakuta imejaa dollar, Vipodozi, iphone na ki-Nokia kidogo cha tochi, ATM Card mbili za Benki tofauti ambazo zilikuwa zimezungushiwa karatasi iliyokuwa na namba za siri za ATM zote, moyo ukanilipuka paaaa!!! Nikaona bora Nipumzike kwanza kitandani!!
    Muda si mrefu ile iphone ikaanza kuita, nilipoangalia halikutokea jina nikaona bora nipokee nimsikilize anasemaje, ilikuwa sauti ya kike iliyoongea kwa huzuni kwa kubembeleza huku akilia na alijitambulisha vizuri kuwa ile mali ni ya kwake! Huruma ilinijia nikamwelekeza nilipo aje kuchukua...
    Hakuchukua muda akawa amefika nami nikamkabidhi vitu vyote naye akavihakiki na kukuta viko sana: Milioni 3 za Kibongo na Dollar 500. Dada kanishukuru na kunipa ile Millioni 3 ya kibongo mi nikazikataa kwasababu ni mali yake na alizisahau tu.
    Alinitoa hofu kwa kunisihi nichukue tu, mi kama binadamu mwenyezi Mungu atanilipa, nikakataa... Mwishowe akaomba namba yangu na kuondoka zake, akawa ameniacha ndani huku njaa sasa nikaanza kuisikia, nilikuwa na buku mbili nikaenda kula viepe kavu na soda nikawa powa.
    Sasa jana kanipigia simu kuwa anakuja nimsubiri, dakika tano tu akanipigia tena kuwa ameshafika yupo nje yupo ndani ya Prado mpyaa nikaingia tukaondoka akaenda kunionyesha kwake kisha tukaelekea kwenye nyumba nyingine iliyokuwa ndo imekamilika kujengwa akaniambia hii itakuwa yako akanikabidhi baadhi ya nyaraka na funguo zote sikuamini...!!
    Akanisindikiza kwangu, kufika home ananiambia hiyo gari (Prado) nayo ananiachia ni kwa mema tu niliyomfanyia, ndani ya ile gari kulikuwa na brifcase iliyokuwa na pesa akaniambia pia hii pesa itakuwa yako ya kuanzia maisha, na kumbe yule dada alikuwa kanipenda akanikumbatia kwa nguvu nikiwa pale kwenye seat oooh!! umasikini baibai...
    Akiwa kanikumbatia akihema kwa kasi juu ya kifua changu nikahisi mtu akinishika begani na kuniita kwa sauti.
    “Anko ankoo we ankoo... amka rafiki yako Salim anakuita!!!”.
    “ALIKUWA MTOTO WA SISTA ALIKUWA ANANIAMSHA !!”.
    Kumbe muda wote nilikuwa nikiota Dah..
    Imechapishwa na Unknown kwa 12:47:00 Hakuna maoni:
    Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

    LIPUMBA ANGESEMA ADC WANGEMWACHIA URAIS


    Profesa Ibrahimu Lipumba
    Kwa ufupi

    Profesa Ibrahimu Lipumba juzi alitangaza rasmi kuachia nafasi ya Uenyekiti wa CUF Taifa
    By Kalunde Jamal na Borrice Bwire

    Dar es Salaam. Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Chifu Lutalosa Yemba, amemkaribisha aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kujiunga na chama hicho.

    Chama hicho juzi kilifanya mkutano wa kuwatambulisha wagombea wake wa nafasi ya urais, Yemba anayewania urais wa muungano na mgombea mwenza wake Said Miraj Abdullah, pia alitambulishwa Hamad Rashid Mohamed, anayewania urasi wa Zanzibar.

    Yemba kwenye mkutano huo alisema anaufahamu uwezo wa Lipumba katika siasa, ujasiri na uvumilivu wake, hivyo hatakuwa na kinyongo kufanya naye kazi ya kusukuma mbele gurudumu la siasa za upinzani.

    Alisema hakujiunga na chama hicho kwa ajili ya kuwa rais, amejiunga kwa ajili ya kutengeneza dola ya uongozi itakayoondoa dhiki na mateso wanayopata Watanzania, hivyo kutokana na uzowefu alionao katika siasa anaamini watafanikisha hilo kwa ufanisi.

    “Walinifukuza mwezi wa sita , mwezi wa nane Lipumba amejing’atua kwenye uongozi, watafahamu sasa kuwa kwenye chama kile kuna udhalimu, namkaribisha Lipumba na ninampongeza kwa uvumilivu wake, ingawa ninaumia kuona kiongozi shupavu aliyekuwa na uwezo wa kuhakikisha wananchi wanaamini katika vyama vingine vya upinzani kukatishwa tamaa na watu wachache wenye uroho wa madaraka, ”alisema Yemba.

    Alisema kuwa anaingia katika kinyang’anyiro cha kuwania urais akipambana na chama kimoja tu, CCM, hivyo vilivyobaki hakuna wa kumtisha kwa sababu wenyewe kwa wenyewe wameanza kuvurugana.

    “Sisi ADC kama bahari, tunachukua maovu yao tunameza, baadaye tunayatema, wakati ukifika wa kufanya hivyo tutafanya kwa sasa , nawaomba Watanzania mpime kwa makini na kuchagua kiongozi anayefaa.

    “Mchagueni asiyekuwa mwizi, fisadi, mnyang’anyi asiye na kashfa na hakuna unapoweza kumpata kiongozi wa namna hiyo zaidi ya ADC, pimeni sikilizeni sera zetu, ilani yetu mtuunge mkono. ”alisema Yemba.

    Jana, Yemba alichukua fomu za kuwania urais wa chama hicho, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), huku akiwasisitiza Watanzania kukipa nafasi chama hicho ili kuifanyia nchi mabadiliko ya haki na kuondokana na ukandamizaji.

    Kabla ya kufikia uamuzi wa kuchukua fomu Nec, Yemba alinukuliwa akisema kama Lipumba angejitokeza jana, angemwachia nafasi ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano. Hata hivyo kuna taarifa Lipumba alisafiri juzi usiku kwenda nje ya nchi.

    Said Miraj Abdulla

    Kwa upande wa mgombea mwenza wa chama hicho Said Miraj Abdulla, alisema kuwa anamualika Maalim Seif awaeleze Watanzania anataka nini katika siasa, kwa nini anavuruga utaratibu wa kuwapo kwa upinzani wa kweli.

    Alieleza kuwa pamoja na kuunga mkono kilichofanywa na Lipumba kutokana na udhalimu unaofanywa na wanasiasa wachache wanaokatisha tamaa wengine, lakini hafurahi kumuona au kusikia anakaa nje ya ulingo wa siasa.

    “Nani asiyejua mchango wa Lipumba katika siasa za upinzani wa nchi, arudi kwenye siasa aje kuendeleza safari aliyoianza mwaka 1995, kukaa kwake nje ya siasa kunapunguza nguvu ya Watanzania kufikia kilele cha mafanikio ya kupata rais atakayejali shida zao, kuwasikiliza, kuwanufaisha na rasilimali zinazopatikana nchini mwao, ”alisema Abdulla.

    Hamad Rashid Mohamed

    Kwa upande wa mgombea urais wa Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed, aliwataka wananchi kuwa makini wanaposhabikia vyama na kuviepuka visivyoheshimu Katiba.

    Alisema alipokuwa kwenye Bunge la Katiba alisema hakuna upawa wala Ukawa, matokeo yake ndiyo hayo watu wanalumbana, Wazanzibar wanahitaji mabadiliko wamekaa kwenye umasikini usiowahusu kwa sababu hakuna ajira.

    Alieleza kuwa kwa wakazi wa Zanzibar wanaohitaji ajira, akijenga viwanda vitano tu hakutakuwa na kijana atakayekosa kazi na huo ndiyo mkakati wake katika miaka mitano ya uongozi.

    “Watanzania shabikieni vyama huku mkiwapima wagombea wana nia gani na nyinyi, maslahi yao binafsi au kuwasaidia, maana “Tumbili akimaliza miti anakuja mwilini” kuweni makini, ”alisema.

    Imechapishwa na Unknown kwa 11:35:00 Hakuna maoni:
    Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest

    Dk Magufuli, Lowassa pambano la karne


    Dk John Magufuli (Kushoto) na Edward Lowassa (kulia)
    Kwa ufupi

    Dk Magufuli na Lowassa ni kati ya makada saba waliosimamishwa na vyama saba kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ambao inaelekea kuwa ndiyo watakaochuana vikali, hasa kutokana na ukweli kuwa Dk Magufuli anatoka chama tawala na Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu, anaungwa mkono na vyama vinne vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

    Dar es Salaam. Wakati zikiwa zimesalia siku 14 kabla ya kuanza kwa kampeni za urais, ubunge na udiwani, macho na masikio ya wengi yanaelekezwa kwa wagombea wawili kutoka vyama vikuu vya siasa, Dk John Magufuli wa CCM na Edward Lowassa wa Chadema, ambao uchambuzi wa gazeti hili unaonyesha wana mengi yanayoshabihiana.

    Wawili hao ni kati ya makada saba waliosimamishwa na vyama saba kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ambao inaelekea kuwa ndiyo watakaochuana vikali, hasa kutokana na ukweli kuwa Dk Magufuli anatoka chama tawala na Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu, anaungwa mkono na vyama vinne vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

    Wengine wanaowania urais ni Mchungaji Christopher Mtikila wa DP, Chifu Lutayosa Chemba (ADC), Macmillan Limo (TLP), Hashimu Rungwe (Chauma), Fahami Dovutwa (UPDP) na mgombea wa ACT Wazalendo ambaye bado hajateuliwa.

    Pamoja na kwamba katika siasa lolote linaweza kutokea, wagombea hao watano hawatazamiwi kuweka ushindani mkubwa zaidi ya ule wa Dk Magufuli na Lowassa.

    Dk Magufuli hakutarajiwa kupita kwenye mbio za urais ndani ya CCM, ambako Lowassa na vigogo wengine walikuwa wakipewa nafasi kubwa, lakini ushindi wake umemfanya awe mgombea wa chama chenye mtandao mkubwa nchini na hivyo mwanzoni kupewa nafasi kubwa ya kushinda.

    Hata hivyo, uamuzi wa Lowassa kujivua uanachama wa chama kilichomlea na kilichompa umaarufu mkubwa, umebadili upepo na sasa vita ya kuingia Ikulu Oktoba 25 inaonekana kuwa ya watu hao wawili.

    Gazeti la Mwananchi linaangalia sifa ambazo wawili hao wanashabihiana pamoja na tofauti zao, kwa kuzingatia maelezo ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa.

    Wote wamesomea ualimu

    Moja ya mambo ambayo wawili hao wanashabihiana ni kusomea ualimu, ingawa wa fani tofauti. Dk Magufuli, ambaye atakuwa akitimiza miaka 56 siku nne baada ya Uchaguzi Mkuu, ni mwalimu aliyejikita kwenye masomo ya kemia na hesabu.

    Alipata diploma ya ualimu mwaka 1982 kwenye Chuo cha Elimu Mkwawa, kabla ya kujiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alipata shahada yake ya kwanza, ya umahiri na ya uzamiri akijikita kwenye somo la kemia.

    Lowassa, ambaye Agosti 26 atakuwa akitimiza miaka 62, alisomea shahada ya ualimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1977, lakini shahada yake ya uzamili ilijikita kwenye masomo ya maendeleo ya jamii.

    Dk Magufuli alitumia taaluma yake kufundisha kemia na hesabu kwenye Shule ya Sekondari ya Sengerema, lakini Lowassa hakufundisha.

    Wote ni makini

    Pengine ni kutokana na maadili ya ualimu, wawili hao wamedhihirisha kuwa ni watu makini katika utendaji wao, jambo ambalo limekuwa likiwafanya watu wanaofanya kazi chini yao kuwa na wasiwasi kila wanapowapeleka taarifa.

    Dk Magufuli na Lowassa hutumia muda mwingi kujiridhisha na taarifa wanazopelekewa kabla ya kufanya uamuzi ambao wakati mwingine huonekana kama wamekurupuka.

    Mhandisi mmoja ambaye amewahi kufungiwa leseni na Magufuli aliiambia Mwananchi kuwa kosa moja kubwa alilofanya ni kumwandikia Dk Magufuli taarifa ndefu, lakini iliyojaa mambo yasiyo sahihi.

    Anasema kuwa aya hiyo ilikuwa ukurasa wa 20, lakini ndani ya muda mfupi Magufuli aliibaini na kibarua chake kiliota nyasi.

    Hali ni kama hiyo kwa Lowassa, ambaye akiwa Waziri Mkuu aliwahi kumtimua mkandarasi wa Wilaya Temeke kwa kushindwa kukagua ujenzi wa maghorofa ikiwemo la Chang’ombe Village lililoporomoka na kusababisha maafa ya mtu mmoja na wengine kadhaa kujeruhiwa mwaka 2006.

    Uchapakazi

    Mbali na umakini, wawili hao wamedhihirisha kuwa ni wachapakazi hodari katika wizara na taasisi walizopitia kiasi cha kujijengea jina kubwa kwa wananchi.

    Utendaji wa Dk Magufuli hauna shaka na ameshaeleza bayana kuwa hapendi wazembe na wasiowajibika sanjari, kama Lowassa ambaye hata siku ya kwanza alipoingia ofisini mwaka 2005 aliwataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

    Wakati Dk Magufuli alipohamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wengi walidhani kuwa amemaliza kisiasa, lakini mbunge huyo wa Chato alifanya kazi kubwa ya kutambua fursa za kiuchumi zilizoko hasa kwenye uvuvi na akafanikiwa kuonyesha ni kiasi gani Serikali ilikuwa ikipoteza fedha.

    Wakati huo, Tanzania iliingia makubaliano na Afrika Kusini na nchi nyingine za ukanda huu kufanya doria kwa pamoja kwenye pwani ya Afrika Mashariki na juhudi hizo zilifanikiwa kunasa meli ya Tawaliq 1 iliyokuwa na samaki wenye thamani ya Sh20 bilioni.

    Uchapakazi wake umedhihirika hasa kwenye ujenzi wa barabara, akiwa amefanikiwa kuunganisha takriban mikoa yote ya Tanzania katikja kipindi alichokaa Wizara ya Ujenzi.

    Lowassa anaonekana zaidi katika kusimamia utekelezaji wa mradi wa maji ya Ziwa Victoria katika shughuli za maendeleo baada ya mpambano mkali dhidi ya Misri, ambayo ilikuwa na ukiritimba wa maji hayo kabla ya nchi tano kuungana na kusaini makubaliano ya matumizi ya maji hayo.

    Lowassa pia anajinadi na mafanikio ya ujenzi wa shule za kata, ambazo kwa kiasi kikubwa zimefanikisha watoto wengi kupata elimu kwa gharama nafuu, ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma ambao aliufanya kwa kukutanisha mifuko ya hifadhi ya jamii na kuiamuru ichangia gharama za ujenzi.

    Jambo lingine walilonalo Dk Magufuli na Lowassa ni misimamo. Dk Magufuli ni kiongozi mwenye misimamo isiyotia shaka na siku zote husimamia anachokiamini, sanjari na Lowassa, ni mwenye misimo yake na itakumbukwa alipokuwa Waziri wa Maji na baadaye Waziri Mkuu alionyesha misimamo.

    Dk Magufuli alitofautiana hata na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati aliposimamia uendeshaji wa kivuko cha Kigamboni, na suala la kiwango cha mizigo inayobebwa na malori.

    Moja ya kauli zilizonukuliwa sana ni ile ya “asiyekuwa na nauli ya kulipia kivuko, apige mbizi”, ambayo ilitafsiriwa kuwa ya kutojali wananchi, lakini faida zake ndio zinamfanya aonekane kuwa msimamo wake ulilenga kunufaisha wananchi.

    Hali kadhalika Lowassa anajulikana kwa kusimamia uamuzi kama wa kubomoa maghorofa yaliyojengwa kinyume na sheria Masaki jijini Dar es Salaam. Msimamo wake pia kwenye suala la mkataba wa City Water iliyokuwa ikihusika na ugavi wa maji jijini Dar es Salaam ndio uliosababisha uvunjwe.

    Ufuatiliaji

    Lowassa na Dk Magufuli pia wanajulikana kwa kuwa wafuatiliaji wazuri kwa watu walio chini yao au wanaofanya kazi chini ya mamlaka zao. Dk Magufuli, ambaye anajulikana kwa kukariri tarehe, kiwango cha miradi, urefu wa barabara na kiwango cha fedha zilizotengwa kwenye miradi, hutumia talanta hiyo kufuatilia miradi mbalimbali na hasa muda wa kumalizika, hali inayomfanya kila mara atishia kuvunja mikataba na wakandarasi au kuivunja kabisa.

    Hilo pia limekuwa likifanywa na Lowassa, ambaye akiwa Waziri Mkuu alikuwa akihakikisha wakuu wa wilaya na mikoa wako sehemu zao za kazi na yeyote ambaye alitaka kutoka alitakiwa awe na kibali, kwa mujibu wa baadhi ya watu waliofanya kazi naye.

    Udhaifu

    Mbali na sifa hizo nzuri, wanasiasa hao wanashabihiana katika udhaifu, hasa uamuzi wa papo kwa papo ambao pia husababishwa na kiu yao ya kutaka kuona kazi inafanyika.

    Wote wawili hufanya uamuzi wa papo kwa pamo ambao wakati mwingine huwa na athari za kisheria. Uamuzi kama huo huwa na kadhia kwa wafanyakazi na makandarasi wanaopewa zabuni mbalimbali na Serikali.

    Hawaachi mfumo wa utendaji

    Udhaifu mwingine wa wawili hao ni hali ya kujituma wao bila ya kutengeneza mfumo ambao unaendeleza ufanisi na badala yake wanapoondoka, hali hubakia kama ilivyokuwa awali.

    Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Dk Magufuli kwenye wizara alizopitia kama ya uvuvi na hali kadhalika kwa Lowassa.

    Pia wanatofautiana

    Tofauti kubwa kati ya Dk Magufuli na Lowassa ni mgombea huyo wa CCM kutokulia ndani ya chama na badala yake amekuwa kwenye nafasi za utendaji zaidi na uwaziri. Dk Magufuli amekuwa mwanachama wa CCM na mbunge, nafasi ambayo humuingiza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu pekee.

    Lakini Lowassa ameshika nafasi mbalimbali kwenye chama kuanzia katibu wa mkoa hadi mjumbe wa vyombo vya juu vya CCM.

    Kauli za wachambuzi

    Baadhi ya wachambuzi na wasomi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (Udsm) wamesema kwa nyakati tofauti kwamba wagombea hao wanaonekana kuwa na tofauti kubwa zinazoweza kufanikisha ushindi katika uchaguzi huo.

    Mohammed Bakari, ambaye ni mhadhiri wa Idara ya Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema wagombea hao wanafanana katika kigezo cha utendaji kazi lakini kiuamuzi na uzoefu wanatofautiana.

    “Dk Magufuli ana uamuzi wa kukurupuka ila Lowassa ametulia,” alisema. “Kuhusu uzoefu pia Lowassa ni mzoefu kiuongozi kuliko Dk Magufuli.”

    Alisema suala la uadilifu siyo rahisi kupata kiongozi mwadilifu kwa wagombea hao na bila kuzitaja kashfa hizo, alisema wote wana kashfa. Aliongeza kwamba, Lowassa ni mgombea anayeweza kuleta mabadiliko kwa Taifa hili, lakini Dk Maghufuli hawezi kutokana na mfumo uliopo kwenye chama chake.

    Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa wa Udsm, Dk Alexander Makulilo pia anaona sifa hizo zinazolingana.

    Alisema wagombea hao wanafanana kwa utendaji mzuri wa kazi na uamuzi wa papo kwa hapo. Aidha, alisema Magufuli ni kiongozi anayeweza kuleta siasa mpya zisizokuwa na makundi.

    Alisema Lowassa ni mgombea anayekabiliwa na changamoto ya Richmond iliyomfanya ajiuzulu uwaziri mkuu, wakati Dk Magufuli hana kashfa kubwa iliyowahi kujadiliwa bungeni.

    “Lakini hali hiyo haiwezi kuwa changamoto kubwa kutokana na mwamko mkubwa wa kundi linalohitaji mabadiliko ya uongozi serikalini. Uchaguzi huu ninaufananisha na Zambia wakati chama cha UNIP kilipoondolewa madarakani kwa kuwa makundi ya kijamii yalikuwa yameamua kiondoke madarakani,” alisema.

    Kuhusu mfumo kuibeba CCM, Dk Makulilo alisema ni sehemu ya changamoto kubwa inayoweza kufanikisha ndoto za Lowassa kuingia madarakani.
    Imechapishwa na Unknown kwa 11:13:00 Hakuna maoni:
    Tuma Hii kwa Barua pepeBlogu Hii!Chapisha kwenye XShiriki kwenye FacebookShiriki kwenye Pinterest
    Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Nyumbani
    Jisajili kwenye: Machapisho (Atom)

    KIKOTI EDUCATION CENTRE

    KIKOTI EDUCATION CENTRE

    kwa afya bora

    kwa afya bora

    Tafuta taarifa

    Orodha Yangu ya Blogu

    • KIKOTI EDUCATION CENTRE
      Tangazo kwa walioomba ajira KIKOTI EDUCATION CENTRE

    WAZO LA LEO

    usiombe pesa, omba kazi
    powered by KIKOTI EDUCATION CENTRE

    Habari mchanganyiko

    • ▼  2018 (42)
      • ▼  Septemba (4)
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya...
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya...
        • Msukuma Asema Lowassa Anampango wa Kurudi CCM
      • ►  Julai (2)
      • ►  Aprili (8)
      • ►  Machi (5)
      • ►  Februari (6)
      • ►  Januari (17)
    • ►  2017 (357)
      • ►  Desemba (13)
      • ►  Novemba (7)
      • ►  Oktoba (10)
      • ►  Septemba (16)
      • ►  Agosti (27)
      • ►  Julai (31)
      • ►  Juni (27)
      • ►  Mei (41)
      • ►  Aprili (32)
      • ►  Machi (59)
      • ►  Februari (53)
      • ►  Januari (41)
    • ►  2016 (593)
      • ►  Desemba (36)
      • ►  Novemba (31)
      • ►  Oktoba (37)
      • ►  Septemba (58)
      • ►  Agosti (57)
      • ►  Julai (82)
      • ►  Juni (75)
      • ►  Mei (95)
      • ►  Aprili (80)
      • ►  Machi (17)
      • ►  Februari (6)
      • ►  Januari (19)
    • ►  2015 (62)
      • ►  Desemba (11)
      • ►  Agosti (3)
      • ►  Julai (6)
      • ►  Juni (7)
      • ►  Mei (21)
      • ►  Aprili (14)

    Jisajili Kwenye

    Machapisho
    Atom
    Machapisho
    Maoni Yote
    Atom
    Maoni Yote

    Kurasa

    • facebook
    • misael B kikoti

    Advertise with us:

    Advertise With Sponsored Post

    I can publish a sponsored post about your business,website,blog, start up, OR add your website address into an existing blog post as a sponsor of the post. />PHONE:+255769694963

    Machapisho Maarufu

    • SIMULIZI FUPI YA MAPENZI
            Kijana mmoja alitokea kumpenda sana dada mmoja ijapokuwa dada huyo alikuwa akimtolea nje mara kwa mara lakini ...
    • SHAIRI YA KWANZA YAITWA TITI LA MAMA
      Titi la mama litamu,hata likiwa la mbwa, Kiswahili naazimu,sifayo iliyofumbwa, Kwa wasiokufahamu,niimbe ilivyo kubwa, Toka kama ml...
    • Makonda ataja majina mengine ya washukiwa wa madawa ya kulevya
    • USIKU KUNA MAMBO: SIMULIZI YA MAPENZI
      Kuna siku nilikuwa maeneo ya Mjini kati (City Center), nikaipenda suruali moja ya shilingi 15,000/= na pesa sikuwa nayo ikabidi niende k...
    • Magazeti ya ijumaa ya Leo tarehe 15/09/2017
    • HAO NDIO MAWAZIRI VIVULI
      Imeandikwa na Stella Nyemenohi, Dodoma ...
    • Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera
      JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU ...
    • Kuona Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Chuo Kikuu 2016/2017,
      UPDATED!: List Ya Vyuo Vilivyotoa Selection Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Mbalimbali 2016/2017 ...
    • Magazeti ya Leo jumamosi ya tarehe 07/05/2016
      Headline hizi za magazeti ya Leo zimeletwa Kwa hisani kubwa ya Airtel jipime kifurushi cha yatosha na kampuni ya uuzaji na utenge...
    • Makonda: Mashoga wanataka kuniangamiza
      MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema tangu alipotangaza kuanza kukamatwa kwa mashoga, ameb...

    Chapisho Lililosomwa sana

    Jipu jipya shule za sekondari zilizopo katika mji mdogo wa ilula -kilolo laanza kuiva

    Na mwandishi wetu , kilolo         Picha:( kushoto) wanafunzi wakijisomea       kulia: prof ndalichako akiapa kuwa W/ elimu.(maktaba y...

    -

    -
    --

    Habari mchanganyiko

    • ▼  2018 (42)
      • ▼  Septemba (4)
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya...
        • Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya...
        • Msukuma Asema Lowassa Anampango wa Kurudi CCM
      • ►  Julai (2)
      • ►  Aprili (8)
      • ►  Machi (5)
      • ►  Februari (6)
      • ►  Januari (17)
    • ►  2017 (357)
      • ►  Desemba (13)
      • ►  Novemba (7)
      • ►  Oktoba (10)
      • ►  Septemba (16)
      • ►  Agosti (27)
      • ►  Julai (31)
      • ►  Juni (27)
      • ►  Mei (41)
      • ►  Aprili (32)
      • ►  Machi (59)
      • ►  Februari (53)
      • ►  Januari (41)
    • ►  2016 (593)
      • ►  Desemba (36)
      • ►  Novemba (31)
      • ►  Oktoba (37)
      • ►  Septemba (58)
      • ►  Agosti (57)
      • ►  Julai (82)
      • ►  Juni (75)
      • ►  Mei (95)
      • ►  Aprili (80)
      • ►  Machi (17)
      • ►  Februari (6)
      • ►  Januari (19)
    • ►  2015 (62)
      • ►  Desemba (11)
      • ►  Agosti (3)
      • ►  Julai (6)
      • ►  Juni (7)
      • ►  Mei (21)
      • ►  Aprili (14)

    Wikipedia

    Matokeo ya utafutaji

    Jisajili kikoti m blog

    Machapisho
    Atom
    Machapisho
    Maoni Yote
    Atom
    Maoni Yote

    Tafuta katika Blogu Hii

    Translate

    we are strong

    To fight for
    Powered By Blogger

    matukio yenye uhakika

    ubora sanifu ndani yake

    Kunihusu

    Unknown
    Tazama wasifu wangu kamili
    kikoti. Mandhari ya Alama maalum. Inaendeshwa na Blogger.