ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Ijumaa, 10 Februari 2017

BREAKING: FREEMAN MBOWE AKATAA KWENDA KITUO CHA POLISI

 Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikaeli Mbowe amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hana mamlaka ya kumuita kwenda Kituo cha Polisi.
Mbowe ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma kufuatia kutajwa katika orodha ya watuhumiwa 65 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kutakiwa kufika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo saa tano asubuhi.
Mbowe amekanusha vikali tuhuma hizo za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kusema kuwa anachokifanya RC Makonda ni kuwaepusha watuhumiwa wa kweli wa dawa za kulevya na mikononi mwa sheria.
Aidha, Mbowe amesema kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi muda wowote endapo njia sahihi zitakapofuatwa. Pia amesema atamfungulia mashtaka RC Paul Makonda kwa kumchafulia jina lake kufuatia kumtuhumu kwa biashara ya dawa za kulevya.
Kiongozi huyo wa Kambi ya Upinzani Bungeni amesema kuwa wao hawana ugomvi wowote na Jamhuri bali Paul Makonda binafsi.
Wakati huo huo, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa jimbo la Hai, Freeman Mbowe amekutana na kufanya mazungumzo na Wabunge kutoka Bunge la Ulaya, David Martin, Gerrard Quille, Balozi wa Umoja wa Ulaya Tanzania, Roeland Van De Beer na Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Kikanda,Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, mjini Dodoma leo Ijumaa 10/02/2017.

Magazeti ya Leo ijumaa ya tarehe 10/02/2017
































Alhamisi, 9 Februari 2017

Tundu Lisu kagoma kula mpaka afikishwe mahakamani.

Wakati Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akigoma kula hadi afikishwe mahakamani, wakili wake amepeleka maombi Mahakama Kuu kuomba apewe dhamana baada ya polisi kuendelea kumshikilia kwa siku ya tatu.

Wakili wa mbunge huyo, Peter Kibatala alisema mteja wake amefikia hatua hiyo, baada ya Jeshi la Polisi linalomshikilia kumnyima dhamana bila sababu.

“Hakuna sababu za msingi za kumnyima dhamana na tangu jana Lissu hajala na amesema hatakula hadi afikishwe mahakamani,” alisema Kibatala na kuongeza:

“Kosa analodaiwa kulifanya lilifanyika Januari 4 na hadi Februari 6 ni mwezi, kama ni muda wa kuchunguza kosa hata hati ya mashtaka ingekuwa tayari,” alisema Kibatala.

Alisema mteja wao (Lissu) analalamikia kuanzia ukamatwaji wake ulipoanza, alipokamatwa eneo la Bunge bila Spika kuwa na taarifa.

Kibatala alisema polisi waliokwenda kumkamata aliwatambua njiani na alikamatwa bila kuwapo kibali cha kukamata (arrest warrant).