Baadhi ya Wanafunzi wanaofadhiliwa na UKI - Ilula wakiwa na Katibu msaidizi wa UKI-ILULA
Picha: Baadhi ya wajumbe wa UKI-ILULA wakiwa na wanafunzi wanaofadhiliwa UKI-ILULA ni umoja wa wa wanajamii wa ilula ulioanzishwa mwaka 2015, ukijihusisha na kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali kama vile kusaidia watoto wasijiweza kwa kugharamia mahitaji mbalimbali ikiwemo ada, sare za shule, na mahitaji mengine lakini vile vile inahusika na kutoa elimu kwa jamii kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo athari za madawa ya kulevya na madhara ya magonjwa mbalimbali kama UKIMWI. UKI-ILULA ilianzishwa chini ya mwasisi wake Msyangi kama mwenyekiti wa umoja huo na kupata usajiri kutoka serikalini lakini pia inajumuisha viongozi mbalimbali kama Katibu na mhasibu.
Mpaka sasa UKI-ILULA inafadhiri na kutoa mahitaji kwa wanafunzi kumi kutoka shule ya msingi Mtua na Ikuvala lakini pia ina malengo ya kufadhili takribani wanafunzi ishirini na tano kwa mwaka ujao
Picha:Baadhi ya wana UKI-ILULA wakiwa na wanafunzi kutoka shule ya msingi Mtua ambao pia wamepatiwa vifaa mbalimbali ikiwemo masweta ya shule
Picha:wana UKI-ILULA wakiwa pamoja na wanafunzi kutoka shule ya msingi Ikuvala(mbele upande wa kushoto ni katibu mkuu wa UKI-ILULA Michael msola ,katikati ni mjumbe Anjera msola, na mwisho kushoto ni mhadhini wa UKI ILULA Alfa mfilinge)
Baahi ya wana UKI-ILULA wakipita katika mazingira ambayo wanafunzi kutoka shule za ikuvala na Mtua huishi
UKI-ILULA kupitia viongozi na wajumbe wake wote inaendelea kuwaarika wadau mbalimbali katika kusaidia jamii yetu ya ilula hasa wale wanaoishi katika mazingira magumu na waohitaji msaada wa hali na mali Ilula yetu itajengwa na wanailula wenyewe.