ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Alhamisi, 7 Septemba 2017

Tundu Lissu Apigwa Risasi Akiwa Dodoma

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amekimbizwa hospitali mchana huu  baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana leo mchaa akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa ametoka bungeni na kwenda nyumbani kwakwe kwa ajili ya chakula cha mchana.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba amekimbizwa hospitali na sasa yupo chumba cha upasuaji.

Magazeti ya leo Alhamisi ya tarehe 07/09/2017

Jumatano, 6 Septemba 2017

Viongozi wanne wa CUF wafariki kwa ajari

Watu watatu wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari aina ya Toyota Noah kugongana na lori eneo la Ubena Zomozi mkoani Pwani usiku wa kuamkia leo.

Naibu mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa CUF, Masoud Mhina akizungumzia ajali hiyo, amesema waliokufa ni wanachama wa chama hicho mkoani Tanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema ajali hiyo ilitokea saa 8:30 usiku wa kuamkia leo Septemba 6 baada ya Toyota Noah lililokuwa likitokea Dodoma kuhama njia na kugongana na lori.

Lyanga amesema lori hilo lilikuwa likiendeshwa na Yassin Hamad mkazi wa Dar es Salaam.

Amesema waliokufa katika ajali hiyo ni Uledi Salumaa (32) ambaye alikuwa dereva wa Toyota Noah, Mary Komba (40) na mwingine aliyetambuliwa kwa jina moja la Isack, wote wakazi wa Muheza mkoani  Tanga.

Kamanda Lyanga amewataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Juma Nindi, Chausiku Hassan na Esther Masie ambao pia ni wakazi wa Muheza.

Amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Tumbi mjini Kibaha na majeruhi walipelekwa kwa matibabu katika Kituo cha Afya Chalinze.

Kamanda Lyanga ametoa wito kwa madereva kuacha kuendesha kwa mwendo wa kasi na hasa usiku kwa kuwa madhara yake huwa makubwa.

“Niwatake madereva wote wanaoendesha magari usiku, ukijihisi umechoka weka gari pembeni pumzika. Ukilazimisha utakuwa kama huyu ambaye alihama upande wake na kugongana na lori,” amesema.