ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumatano, 14 Februari 2018

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yawajibu CHADEMA

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imezijibu hoja sita za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuhusu uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Kinondoni.

Majibu hayo yametoka baada ya Chadema kuilalamikia tume na watendaji wake walioteuliwa kusimamia uchaguzi huo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, NEC ilidai haijapokea barua yoyote kutoka Chadema licha ya chama hicho kikuu cha upinzani bungeni, kuvieleza vyombo vya habari kwamba kimeiandikia barua tume kuhusu wakuu wa wilaya kushiriki mikutano ya kampeni za kuwanadi wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na tume haijachukua hatua zozote.

Taarifa ya NEC ilibainisha kuwa hoja ya pili ya Chadema ni tume kuhamisha vituo 46 vya kupigia kura katika kata tatu za Kigogo, Mwananyamala na Kijitonyama bila kuishirikisha Chadema.

Hoja nyingine ni Msimamizi wa Uchaguzi kutoa uamuzi dhidi ya Chadema kwenye Kamati ya Maadili kwa uonevu na Chadema kuadhibiwa na Kamati ya Maadili kwa makosa yanayotuhumiwa kutendwa na mwanachama wa Chadema na kuwa makosa hayo ni ya kijinai na yalipaswa kushughulikiwa kijinai na si kukipa adhabu chama hicho.

Pia Chadema ilisema kikao hicho kiliendeshwa na mtu asiyepaswa kuwa Mwenyekiti wa Kamati.

Taarifa ya NEC ilieleza kuwa hoja nyingine ni kitendo cha malalamiko ya Chadema dhidi ya wakuu wa wilaya kushiriki kampeni za uchaguzi na Kamati za Maadili kutotenda haki kwa kuwa wenyeviti wake ni makatibu tawala wa wilaya.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani, ilifafanua kuwa tume haijapokea barua au karatasi yoyote kutoka Chadema inayoelezea malalamiko yao.

“Ukweli ni kwamba, Chadema hawajawasilisha barua kwa tume. Hata kama wangewasilisha barua za malalamiko yao, tume ingewaelekeza kusoma na kuelewa Maadili ya Uchaguzi, kwa kuwa lalamiko namba mbili hadi sita waliyoyataja kwenye vyombo vya habari yangeweza kushughulikiwa na Kamati za Maadili ambazo Chadema kama chama chenye wagombea ni sehemu ya wajumbe wa kamati husika,” alisema.

Kailima katika taarifa hiyo, alisema uhamishaji wa vituo umezingatia matakwa ya Kanuni ya 21 ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura za mwaka 2008 kama zilivyorekebishwa mwaka 2014.

“Kanuni hiyo ikisomwa pamoja na kipengele cha 9.2(c) cha Kitabu cha Maelekezo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ya mwaka 2015, vituo vya kupigia kura havitakiwi kuwa kwenye maeneo ya Kambi za Jeshi, Polisi, maeneo ya kuabudia kama vile misikiti na makanisa, nyumba za viongozi au mashabiki wa vyama vya siasa,” alifafanua katika taarifa hiyo.

Kailima pia alisema kuwa kwa kuzingatia matakwa ya kanuni na kipengele tajwa, Januari 31, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Uchaguzi la Kinondoni, aliitisha mkutano wa vyama vya siasa vyenye wagombea ubunge na ajenda ilikuwa ni kuhamisha vituo vya kupigia kura.

“llifanyika hivyo kwa sababu mbalimbali zikiwamo baadhi ya vituo kuwa kwenye maeneo ya kuabudia, kuwa jirani mno na ofisi ya chama cha siasa, nyumba za watu binafsi, kwenye maeneo finyu,” alisema.

Alidai kuwa kikao hicho kilishirikisha wawakilishi 16 kutoka vyama 11 vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Kinondoni.

Mustapha Muro na Katibu wa Chadema wa Wilaya, Shabani Kirita,” Kailima alieleza katika taarifa hiyo.
“Chadema kiliwakilishwa na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kinondoni,

Kuhusu malalamiko kwamba Msimamizi wa Uchaguzi alitoa uamuzi wa uonevu dhidi ya Chadema kwenye Kamati ya Maadili, Kailima alisema uamuzi hufanywa na Kamati ya Maadili na si Mwenyekiti wa Kamati.

“Tunaikumbusha Chadema sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi hayampi Mamlaka Msimamizi wa Uchaguzi kutoa maamuzi kwenye Kamati ya Maadili. Msimamizi wa Uchaguzi ni Mwenyekiti wa Kikao cha Maadili tu, na kwamba, maamuzi hufanywa na Kamati ya Maadili na siyo Mwenyekiti wa Kamati,” alieleza Kailima katika taarifa hiyo.

Kuhusu Chadema kuadhibiwa kwenye Kamati ya Maadili kwa makosa ya kijinai, Kailima alisema tume imekitaka chama hicho kama hakikuridhika na maamuzi kufuata taratibu zilizoainishwa kwenye Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015.

Kuhusu malalamiko dhidi ya wakuu wa wilaya kushiriki kampeni za uchaguzi, Kailima alisema tume inaitaka Chadema kuwasilisha malalamiko yake kwenye mamlaka husika kwa kuwa sheria na kanuni zimebainisha mamlaka zinazoshughulikia masuala hayo

Jumanne, 30 Januari 2018

Breaking News: NECTA Watangaza Matokeo ya Kidato Cha Nne 2017....Bofya Hapa Kuyatazama

Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba.

Jumla ya watahiniwa  385, 767 walisailiwa kufanya mtihani kidato cha nne mwaka 2017, kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio wamefaulu ambapo wasichana ni  143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985 sawa na asilimia 79.06.

Akitangaza matokeo hayo leo Januari 30, 2018 Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09.

Amesema matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo mwaka huu.

"Watahiniwa 77 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani watapata fursa mwaka 2018," amesema Dk Msonde.

Dk Msonde amesema watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani  matokeo yao yamefutwa huku mtahiniwa mmoja akiandika matusi katika karatasi yake ya majibu.

==>Yatazame Matokeo hapo chini

Advertisement