Matokeo
 ya kidato cha sita kwa mwaka 2017 yametoka leo Jumamosi, Julai 15 huku 
shule ya Wasichana ya Feza Girls ikiibuka kinara kwa watahiniwa wake 67 
kufaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili.
Shule
 nyingine zilizoibuka kidedea katika matokeo hayo ni Marian Boys, 
iliyoshika nafasi ya pili, Kisimiri (Arusha) imeshika nafasi ya tatu na 
Ahmes (Pwani) imeshika nafasi ya nne.
 Shule
 nyingine  ni  Marian  Girls (Pwani) iliyoshika nafasi ya tano, Mzumbe 
(Morogoro) nafasi ya sita, St Marry Mazinde Juu (Tanga) nafasi ya saba, 
Tabora Boys (Tabora) nafasi ya nane, Feza BOYS (Dar es Salaam) nafasi ya
 tisa na Kibaha ya Pwani iliyoshika namba kumi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni