ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Alhamisi, 5 Mei 2016

Jipu jipya shule za sekondari zilizopo katika mji mdogo wa ilula -kilolo laanza kuiva

Na mwandishi wetu
, kilolo

























 Image result for nyalumbu sec     Image result for nyalumbu sec
 Picha:( kushoto) wanafunzi wakijisomea       kulia: prof ndalichako akiapa kuwa W/ elimu.(maktaba yetu)
 Utaratibu wa elimu bure unaofanywa na Serikali ambao umefanikiwa kulipa michango yote kwa wanafunzi wa shule za awali msingi na kidato cha kwanza mpaka cha sita, imeonekana kuanza kuvurugwa na walimu wa shule mbalimbali kwa kuanza kutumia mwanya huo kuwavuruga wanafunzi katika utoaji wa elimu bure.
Mwandishi wetu amefuatilia shule hizo zilizopo wilaya ya kilolo kubaini juu ya utekelezaji wa elimu bure amebaini mambo mbalimbali ambayo yameanza kufanywa  na walimu na wakuu wa shule ambayo yanonesha kuwa yana mianya ya kuhujumu wanafunzi kupata elimu bure, haya yamejitokeza katika shule za sekondary zilizopo katika tarafa ya mazombe ambazo zimebuni mbinu mpya ya kurudisha watoto shuleni na kuwaacha bila kuwafundisha huku wakidai kwamba wanataka wanafunzi hawa wajisomee shuleni
Kwanini mwandishi wetu anahisi hili ni jipu?
Hili linaonekana ni jipu kwasababu wanafunzi wanarudishwa shuleni huku kukiwa hakuna mwalimu wakuweza kuwaangalia muda wote wanapokuwa shuleni hivo kuna uwezekano mkubwa kabisa kusababisha wanafunzi wengi kuanza kutumia mda huo kuanza kufanya mambo ambayo ni kinyume na utaratibu wa shule ikiwamo kufika shuleni na kucheza michezo ambayo haina tija, wanafunzi kutumia nafasi hiyo kujihusisha na mapenzi na hata wengine kuaanza kucheza kamali na hata kuharibu miundo mbinu ya shule

Vile hili limeonekana ni jibu kwasababu wanafunzi wanaporudishwa shuleni kwa kigezo cha kujisomea ilipaswa kuwa ni hiari na sio lazima lakini shule hizi zimefanya kurudi shuleni kuwa ni lazima hivo limeonesha nia ya dhati ya walimu kuwabana wototo hao ili wasipate mda wa ziada wa kujisomea nyumbani.

Pia suala la kurudisha wanafunzi shuleni limeonekana kukiuka waraka wa elimu uliotolewa na wizara ya elimu kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI ambayo imetambua mda wa kusoma kwa mwanafunzi wa kutwa na kuzuia walimu kutumia mianya yoyote ile kuhujumu elimu bure
pia inaonekana kabisa kuwepo na mvutano wa chini kwa chini baina ya utekelezaji wa elimu bure kwani kama shule hizi zinaona umuhimu wa wanafunzi kusoma hazikuwa na budi kujitolea kuwalinda watoto pale watakapokuwa wamerudi shuleni kujisomea na ikiwezekana walimu wakubali kupangiwa ratiba maalumu ya kujitolea kufundisha baada ya muda wa kazi
na pia kama ni nia njema kuhakikisha wanafunzi wanajisomea hakukuwa na budi kwa budi kwa utawala wa shule kulazimisha wanafunzi kurudia shuleni ila ingekuwa ni kwa hiari
Nini madhara ya hiki kinachofanywa na shule hizi za kilolo hasa tarafa ya mazombe na mji mdogo wa ilula?
Moja inasababisha wanafunzi kupoteza mda ambao wangeutumia vizuri wakiwa nyumbani kwao hasa tukizingatia wanafunzi wengi wanaishi mbali na makazi yao.
Mbili inawanyima wanafunzi uhuru wa kuchagua mazingira rafiki ya  kujisomea.
Tatu, kuleta migogoro baina ya wazazi, walimu na wanafunzi hasa pale wanapo ondoka kwenda shule na kushindwa kusoma chochote kitu kinacholeta tafsiri mbaya ya uaminifu baina ya mwanafunzi, mzazi na walimu.
wanafunzi wanazungumziaje utaratibu huu ulioanzishwa na shule hizi?
Mwandishi wetu alipohojiana na baadhi ya wanafunzi kwa sharti la kutoandikwa majina yao walisema"hawa walimu si hatuwaelewi kwasababu wao wanasema turudie shuleni kwa lazima afu hawatufundisha sasa hapa ndo watasema tumekuja kusoma? maana hata nyumbani tunasehemu za kusomea na kila mwanafunzi hapa anautaratibu maalumu wa kujisomea mi nafikiri lengo lao ni kutukomesha tu na kutufanya tufeli ili wapate sababu ya kuongea"

Naye mwanafunzi mwingine alieonekana kukereka na utaratibu huu alisema" ivi we mwandishi ungekuwa mwalimu ungesema wanafunzi tufike shule kujisomea wakati unajua wanafunzi wenyewe ndo hawa tukifika shuleni kama hakuna mwalimu wengi wanaanza kucheza mpira na kutushawishi na sisi wengine tushindwe kusoma ebu hawa walimu waache mambo yao ya kushindana na serikali ya hapa kazi "
Na mwanafunzi mwingine alieonekana kufurahishwa na utaratibu wa kurudia lakini kukerwa na utaratibu uliowekwa alisema" kama huyo mkuu wa shule aliposema turudie lengo lake ni zuri lakini wanachokosea kuturudisha shule afu wao kubaki nyumbani huku wanajua sisi tunahitaji kusimamiwa ili kuepuka wanafunzi wengine kutuharibia tusisome kama hao unaowaona wanacheza nje ni vigumu mi kusoma ilihari wanafunzi wengine wanapiga kelele nje.

Na mwandishi wetu alipomtafutaWakuu  wa shule hizi, ambao wameonekana kufanya utaratibu huu. wakuu wa shule hawa wameonekana kutoleta ushirikiano stahiki
Walimu nao walisemaje tulipohojiana na mwalimu mmoja alidai kuwa" mi mwenyewe nimesikia kuwa wanafunzi inabidi warudie kujisomea sasa sijui kuna nini ila si kama walimu mda wetu wa kazi mwisho ni saa tisa na nusu, ko kama tunarudia kutakuwa na extra time na itabidi tulipwe"

Wazazi wanasemaje? mwandishi wetu alipojaribu kuhojiana na baadhi ya wazazi walionesha kukerwa na kitendo cha wanafunzi wao kurudishwa shuleni ilihali hawasomi " mwandishi hawa walimu bwana hata si wenyewe tunashindwa kuwaelewa wanalazimisha watoto warudie shuleni eti kwa kigezo kwamba wakiwa nyumbani hawasomi ivi hii akili kweli maana wanafunzi wengine wanatoka sokoni wanaenda kusoma kiheka na wengine wanatoaka isele wanaenda kusoma nyalumbu au kiheka, sasa huoni kama wanawaumiza watoto wetu kwenda mara mbili kwa siku shuleni ilihali wakitembea umbali mrefu hawa wana lao jambo ngoja tusubiri ila utasikia wanasema sababu za kisiasa"

Mwandishi wetu anaendelea kuwatafuta wakuu wa shule husikaili waweze kutoa ufafanuzi wa suala hili lakini kama waandishi tumeona dhahili hili kuwa ni jipu linalohitaji kutumbuliwa mara moja.
Mkurugenzi, Maafisa wa elimu, pokeeni waandishi wetu tunaowatuma kwenu tumalizie kuaangazia "jicho la mwandishi wetu kutoka kilolo"



Walimu kunolewa wakiwa kazini

WALIMU wa shule za msingi na sekondari nchini watapatiwa mafunzo na Serikali wawapo kazini ili kuongeza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji.
Mafunzo hayo yatahusu matumizi ya stadi za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), sayansi, hisabati na lugha.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya alisema mafunzo hayo ni miongoni mwa mikakati ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha elimu inayotolewa nchini inakuwa na ubora wa hali ya juu.
Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Chadema) aliyetaka kufahamu mikakati ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuinua ubora wa elimu nchini.
Manyanya alitaja mikakati mingine kuwa ni kutoa mafunzo kwa walimu wa darasa la kwanza na la pili katika kuimarisha stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).
“Ili kuimarisha ufuatiliaji na tathmini ya ubora wa elimu itolewayo, ofisi ya uthibiti ubora wa shule kanda na wilaya zinaendelea kuimarishwa kwa kuongeza idadi ya wathibiti ubora wa shule na vitendea kazi,” alisema.

Mabasi 25 yaendayo haraka yagongwa

Imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko MABASI yaendayo haraka jijini Dar es Salaam yanayoendelea na majaribio katika njia zake, zaidi ya 25 yamegongwa na vyombo vingine vya usafiri vilivyopita katika barabara hizo maalumu, licha ya kuzuiwa.
Aidha, ujenzi wa mifumo ya kielektroniki kwa ajili ya ukatishaji tiketi imekamilika kwa asilimia 90 na asilimia iliyobaki inatarajiwa kukamilika wiki hii.
Msemaji wa Kampuni inayoendesha mabasi ya haraka ya UDA RT, Sabri Mabruk alisema kati ya ajali hizo ni moja pekee walifanikiwa kuwakamata wahusika na ajali kupimwa.
Wengine walikimbia baada ya kusababisha ajali. Mabruk alisema kumekuwa na mwingiliano wa vyombo mbalimbali vya usafiri kwenye barabara hizo ikiwamo magari, pikipiki na maguta.
Alisema kutokana na ajali hizo wamesababisha kampuni uharibifu wa magari unaowalazimu kufanya marekebisho kabla hata hawajaanza rasmi kutoa huduma. Aliwataka watumiaji wa vyombo vya usafiri kuzingatia sheria za barabarani kuepusha ajali hizo.
“Pia inatakiwa kusaidiana wadau wote kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya barabara hizo, ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano wa kukamata wale wanaokiuka sheria wanapoonekana wakipita katika njia hizo,” alisema Mabruk.
Alisema miundombinu ya njia hiyo imejengwa kulingana na mahitaji ya mabasi yaendayo haraka, hivyo haipaswi kutumiwa na chombo kingine cha usafiri wala waendao kwa miguu.
Akizungumzia kuanza rasmi kwa mradi huo, alisema kwa sasa wanasubiri kukamilisha kwa suala la nauli kwa kuwa ujenzi wa mifumo ya kielektroniki kwa ajili ya ukatishaji tiketi umebaki asilimia 10 kumalizika na wiki hii utakuwa tayari.
Alisema baada ya kutangazwa kwa nauli ndipo wataweza kutengeneza kadi kulingana na nauli hizo hivyo kuanza kwa huduma hizo.

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza


RAIS John Magufuli amemteua Dk Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu jana mjini Dodoma, Dk Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dk Migiro ataapishwa leo katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Dk Migiro aliteuliwa kuwa Balozi Februari 15, mwaka huu pamoja na wenzake wawili ambao ni aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi la Taifa (NSSF), Dk Ramadhani Dau.
Dk Migiro amewahi kuwa waziri wa wizara mbalimbali katika Serikali ya Awamu ya Nne na pia kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN).
Katika Awamu ya Nne, aliongoza Wizara za Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Katiba na Sheria.

Magazeti ya Leo Alhamisi ya tarehe 05/05/2016



Magazeti haya ya Leo yanaletwa kwenu Kwa hisani ya tigo pata kifurushi cha watsup bure








iliyo imara

uteuzi mwingine wa Rais magufuli