ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Ijumaa, 24 Juni 2016

wanafunzi waliochaguliwa kidato cha tano ilula sec school




wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2016.

 Tumia link hii kupata matokeo Waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi 2016

24-JUNI-2016.
OR-TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2016. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali. Jumla ya wanafunzi 65,720 wakiwemo wasichana 29,457 na wavulana 36,263 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 34,064 wakiwemo wasichana 13,466 na wavulana 20,598 sawa na asilimia 52 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 30,897 wakiwemo wasichana 15,445 na wavulana 15,452 sawa na asilimia 47 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara na wanafunzi 759 wakiwemo wasichana 220 na wavulana 539 sawa na asilimia 1 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya Ufundi.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2016 wataanza muhula wa kwanza tarehe 11 Julai, 2016 na hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 24 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi mwaka 2016 pamoja na fomu za kujiunga (joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
Imetolewa na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI

Tumia link hii kupata matokeo Waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi 2016

Magazeti ya Leo ijumaa ya tarehe 24/06/2016



















Kwa Matangazo ya biashara au uchumi wasiliana nasi Kwa namba +255769694963

Alhamisi, 23 Juni 2016

Breaking News: Rais Magufuli aonya wanasiasa wanaomchelewesha kufanya kazi

Imeandikwa na Selemani Nzaro
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amewaonya wanasiasa wanaomchelewesha kufanya kazi ya kuwatumikia Watanzania.
Rais Magufuli ameyasema hayo muda mfupi uliopita baada ya kupokea ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kutoka kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Amesema haiwezekani uchaguzi umepita na mshindi amepatikana lakini wanasiasa hao wanaendeleza siasa ilhali wananchi wanataka watumikiwe wapate maendeleo.
Rais amesema hatawavumilia viongozi wa siasa wenye lengo baya na nchi na kuwataka waweke maslahi ya Taifa mbele badala ya vyama vyao. Amewataka kufanya siasa baada ya miaka mitano ambapo wananchi watawapima kile walichokifanya kwa muda wote huo.
Awali Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva alisema suala la Kura ya Maoni halikusitishwa kama baadhi ya watu wanavyosema bali iliahirishwa kwa kuwa wakati kura hiyo ilipotakiwa kupigwa Aprili Mwaka jana, Tume ilikuwa na jukumu kubwa la kuandaa uchaguzi Mkuu.
Kutokana na hali hiyo, Jaji Lubuva alisema Tume haikuwa na uwezo wa kubeba mambo mawili makubwa kwa wakati mmoja. Jaji Lubuva amesema kutokana na zoezi la Uchaguzi Mkuu kumalizika rasmi, Tume iko tayari kuanza mchakato wa kura ya maoni.
Kuhusu suala hilo la Kura ya Maoni, Rais Dk Magufuli amemhakikishia Jaji Lubuva kuwa serikali italiamualia mara baada ya Tume kulifikisha serikalni.

TCU yaita wenye kero

Imeandikwa na Lucy Ngowi
TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetoa fursa kwa wananchi wenye kero, maoni na changamoto kuhusu masuala ya elimu ya juu hususani udahili na uendeshaji wa vyuo vikuu, wayawasilishe kwao.
Ofisa Habari Mwandamizi wa tume, Edward Mkaku alisema jana mkakati huo umefanyika kutekeleza agizo kutoka Ofisi ya Rais –Menejimenti na Utumishi wa Umma, lililotaka taasisi hiyo iadhimishe wiki ya utumishi wa umma kwa kusikiliza kero, maoni na changamoto.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mkaku alisema tangu jana saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana, walipokea wananchi 44 waliowasilisha maoni yao.
Wengi wao ni waliokuwa wakiulizia mwongozo wa kudahiliwa vyuo vikuu ambao kwa mwaka huu haujatoka.
Pia waliulizia mfumo wa kuhama kutoka chuo kimoja kwenda kingine, mfumo wa udahili unavyofanya kazi na utambuzi wa vyeti.
Hata hivyo, alisema wamebaini wananchi wengi wamekuwa wakichanganya kazi za tume na za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Serikali yataja kodi mpya zitakazokatwa

Imeandikwa na Joseph Lugendo, Dodoma

WAKATI muswada wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2016 ukitarajiwa kuanza kujadiliwa bungeni leo ambao unaoipa serikali mamlaka ya kisheria kutoza kodi na kutumia fedha hizo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, ametaja kodi ambazo zitalazimika kukatwa.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi kufafanua hoja ambazo hakuzielezea kwa kina bungeni, Dk Mpango alisema miongoni mwa kodi hizo ambazo baadhi ya wabunge na vyombo vya habari vilitetea zisikatwe ni pamoja na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika utalii.
Nyingine ni kutoza kodi katika migahawa na maduka katika majeshi baada ya kufuta msamaha wake na kuhamisha jukumu la utozaji kodi za majengo kutoka halmashauri kwenda katika Mamlaka ya Mapato (TRA).
Akizungumzia VAT katika utalii, Dk Mpango alisema kodi hiyo haihusiani na ongezeko au kupungua kwa watalii nchini kwa kuwa watalii hao hawatazami kodi hiyo kama kigezo kikuu cha kwenda kuangalia vivutio vya utalii.
Alitoa mfano wa idadi ya watalii waliotembelea mbuga za wanyama kwa kipindi 2011 hadi 2014 katika nchi za Tanzania, Kenya na Afrika Kusini, ambayo inaonesha Tanzania licha ya kwamba haikuwa ikitoza VAT, bado ilitembelewa na watalii wachache kuliko nchi hizo ambazo zilikuwa zikitoza kodi.
Aliendelea kusisitiza kuwa mpaka kabla ya hotuba yake ya Bajeti ya Serikali ya 2016/17, nchi zote wanachama wa Jumuiya Afrika Mashariki zilikuwa zikitoza kodi hiyo kwenye huduma ya utalii isipokuwa Tanzania ambayo imependekeza kutoza katika bajeti yake ya mwaka 2016/17.
Kuhusu uamuzi wa serikali kuhamisha jukumu la kukusanya kodi za majengo kutoka katika halmashauri kwenda TRA, Dk Mpango alisema mamlaka hiyo ya kodi ndiyo yenye uzoefu wa kutosha katika ukusanyaji kodi za serikali na ndiyo yenye vituo vya ukusanyaji kodi katika wilaya na mikoa yote Tanzania.
Kuhusu viwango vya kodi ya majengo, alisema Waziri wa Fedha na Mipango ataweka viwango vya kodi ya majengo baada ya kushauriana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kuweka uwazi na kujumuisha maoni ya wadau wote muhimu zikiwemo halmashauri husika.
Katika msisitizo mwingine alisema kuwa, mapato kutokana na kodi ya majengo yataingizwa katika mfuko mkuu ambao mawaziri wenye dhamana ya fedha na Tamisemi, ndio watakaoshauriana kuhusu mgawanyo wa fedha hizo kwa kuzingatia bajeti za halmashauri husika.
Kuhusu madai kwamba kuondolewa kwa misamaha ya kodi katika maduka na migahawa ya vyombo vya ulinzi na usalama kunaondoa motisha katika taasisi hizo, alisema uamuzi huo wa serikali upo palepale kwa kuwa misamaha hiyo ilikuwa ikitumika vibaya.
“Ili kuondoa kasoro hiyo, serikali imeamua kuweka utaratibu wa kuwalipa posho watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama ili wanufaike moja kwa moja kama walengwa. Kiasi cha posho atakayolipwa askari kitakokotolewa baada ya mashauriano na vyombo husika,” alisisitiza.
Kuhusu ushuru wa bidhaa kutozwa kwenye ada ya miamala ya uhawilishaji wa fedha, kama utaathiri mtumiaji wa mwisho, Dk Mpango alisema ushuru huo hautakatwa kwenye fedha zinazotumwa au kupokewa, bali katika ada inayotozwa na benki au kampuni ya simu.
Alifafanua kuwa kwa sasa sheria inatamka kwamba ada hiyo itatozwa katika kutuma fedha tu, hivyo baadhi ya kampuni za simu na benki zilikuwa zikitumia mwanya wa sheria hiyo kupunguza wigo wa kodi kwa kutoza ada wakati wa kupokea tu.