Jumatano, 17 Agosti 2016
Jumanne, 16 Agosti 2016
Watu Watano Akiwemo Askari wa JWTZ Watiwa Mbaroni kwa tuhuma za Kutengeneza Vyeti Feki
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema kuwa pamoja na vyeti hivyo vya uuguzi vilivyokamatwa, pia katika operesheni hiyo walikamata vyeti 37 vya wataalamu wa maabara na vyeti tisa vya ufamasia.
Alisema
kuwa katika operesheni hiyo iliyofanywa kwa pamoja na maofisa kutoka
Baraza la Wafamasia nchini, walikamata jumla ya vyeti 936 vikiwa kwenye
hatua ya ukamilishaji vikiwa bado havijaandikwa majina, miongoni mwake
vikiwemo vyeti 667 vya wauguzi wasaidizi, vyeti 126 vya wataalam wa
maabara, cheti kimoja cha mafunzo ya afya ya jamii na vyeti viwili vya
utoaji huduma ya kwanza.
Katika
kuhakikisha wanakuwa na uthibitisho wa tuhuma hizo, Kamanda Mtui
alisema kuwa pia wamekamata mihuri 25 ya taasisi mbalimbali ikiwemo
nyundo mbili, ambazo hutumika kutengenezea mihuri mbalimbali ya moto.
Aliwataja
watu waliokamatwa katika operesheni hiyo ambayo inahusisha mtandao wa
watu mbalimbali kuwa ni askari wa JWTZ, Mgeni Nyamubozi ambaye ni mume
wa mmiliki wa Duka la Vifaa vya Ofisi la Upendo, lililopo Mwanga mjini
Kigoma, ambalo linatuhumiwa kuhusika na utengenezaji wa vyeti hivyo.
Katika
duka hilo, Kamanda huyo wa polisi alisema polisi walikamata kompyuta
mpakato moja, ikiwa na nakala za vyeti mbalimbali za vyuo na idara za
serikali.
Mwingine
aliyekamatwa ni Dickson Mshahili, muuguzi katika Hospitali ya Mkoa
Kigoma ambaye katika upekuzi nyumbani kwake, alikutwa na nyaraka
mbalimbali ikiwemo madaftari 12 yakiwa na kumbukumbu za vyeti
anavyotengeneza na mihuri ya waganga wakuu wa mikoa ya Kigoma, Kagera,
Mwanza, Singida na Tabora.
Sambamba
nao alikamatwa Zawadi James, muuguzi wa Kituo cha Afya Ujiji ambaye
baada ya kupekuliwa nyumbani kwake, alikutwa na vyeti vitatu na kabuleta
ya pikipiki ambayo hutumika kutengeneza mihuri ya moto.
Wengine
waliokamatwa ni Johnson Nyabuzoka, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari
Mlole ya mjini Kigoma, ambaye ni mtaalam wa kompyuta aliyekuwa akitumika
kufanya kazi hiyo; na Stephano Erasto ambaye alikamatwa katika siku
yake ya kwanza tangu ajiunge na duka hilo kwa ajili ya kusaidia kazi.
Mihuri iliyokamatwa katika tukio hilo.
Kompyuta mpakato,Laptop,Printer na Scarner pamoja na mihuli ni vifaa vilivyokamatwa katika Steshanari hiyo
Jumatatu, 15 Agosti 2016
KIKOTI EDUCATION CENTRE
Picha: wanafunzi wa shule ya msingi ilula wakiwa na walimu wa kikoti education centre walipotembelewa shuleni kwao tarehe 15/06/2016
picha: wanafunzi wa shule ya msingi isoliwaya kikoti education centre walipowatembelea shuleni hapo
picha: wanafunzi wa shule ya msingi isoliwaya kikoti education centre walipowatembelea shuleni hapo
KIKOTI EDUCATION CENTRE (K.E.C)
MAHALI:
ILULA MADIZINI KARIBU MAJENGO YA KANISA KATORIKI
Mzazi/Mlezi wa
………………………………………………,kikoti education centre inapenda kukutarifu kuwa
inatarajia kuaanza kutoa elimu ya pre-form
one kwaajili ya maandalizi ya kidato cha kwanza. Kuanzia tarehe
09/09/2016.Kwa gharama ya shilingi elfu ishirini(20,000) tu kwa muda wa
miezi mitatu(3), ambapo mwanafunzi atapewa vitu vifuatavyo:-
1)
Tisheti yenye jina la
kituo
2)
Daftali, peni na pensel
3)
Vitabu vya masomo husikaVitakuwepo
4)
Mitihani kila wiki kupima maendeleo ya mwanafunzi
5)
Masomo yatakayopewa kipaumbele ni masomo yote ya
sayansi(biology, chemistry,physics, mathematics na English ,GEOGRAPHY)
-
Mlete mwanao apate elimu bora kutoka kwa walimu bora na wenye
taaluma na maadili ya ualimu kutoka vyuo vikuu bora Tanzania
Pia kikoti
education centre wanaendelea na kutoa tuition kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha sita
kama kawaida
OUR MOTTO: EDUCATION FOR LIFE
Kwa mawasiliano
zaidi tupigio kwa namba 0769694963, 0625682117 au 0757927380 au fika kikoti
education centre kwa maelezo zaidi:
MUDA:kuanzia saa moja na nusu (JUMATATU MPAKA JUMAMOSI)
MAHALI : ilula madizini- majengo ya kanisa katoriki, mita 50 kutoka soko la TASAF.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)