ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumanne, 22 Machi 2016

Ukawa kidedea Umeya wa jiji la Dar es Salaam

by kikoti blog




UCHAGUZI wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam ambao unaendele kufanyika muda huu katika ukumbi wa Kareemjee taarifa za ndani kutoka katika uchaguzi huo zimeeleza kuwa mgombea wa vyama vya UKAWA, kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Mh. Isaya Mwita ameibuka kidedea kwa kupata kura 84 huku CCM wao wakipata kura 67 na kati ya jumla ya kura hizo 7 ziliaribikaambapo jumla ya kura za wajumbe wote ni 158.
Umeya jijiHali ilivyo muda huu ndani ya uchaguzi huo wa Umeya wa Jiji la Dar es Salaam muda huu leo Machi 22.2016, ambapo UKAWA wameibuka kidedea
DSCN3491 
Mhe. Issaya Mwita (mbele)  ambaye hadi sasa vyanzo vya ndani kutoka uchaguzi huo ameweza kupata kura 84 dhidi ya mshindani wake kutoka CCM ambaye alipata kura 67 huku kura 7 zikiharibika, hivyo kuibuka na ushindi wa Umeya wa Jiji. (Picha ya Maktaba).

Hakuna maoni: