ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumapili, 20 Machi 2016

TATIZO LA MAJI KATIKA MJI MDOGO WA ILULA KUISHA KABLA 2020

 MBUNGE  wa   jimbo la  Kilolo  Venance  Mwamoto ameahidi kuongozana na  wazee  wa mji  wa Ilula kwenda Dodoma kuonana na   waziri  mkuu Kassim Majaliwa  ili  kumfikishia ahadi ya  maji ya Rais Dr John Magufuli kwa  wananchi  wa mji  mdogo  wa Ilula .
  https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEganogblP_gVCgRkG9WDNjiGmgaKAifYWmTa2QBjcrUK3DmNOKvT2dQlSyKamiQbpJZcmDhxihrAM2_xHTsKYSRWFBdFoq4h51s2_Pi4txRVupOtV59XeiXS6613jzzTHtGGiQD7z7auNM-/s640/DSC_0972.JPG


Huku  akiwataka wananchi wa Ilula na Nyalumbu  kutomchagua mwaka 2020  iwapo atashindwa  kutekeleza ahadi ya maji katika mji  huo wa Ilula ndani ya  miaka  yake  mitano ya  ubunge.

Akizungumza  na  wananchi  wa kata ya  Nyalumbu na Ilula  wakati wa  mikutano yake ya  hadhara ya  kuwashukuru  wananchi  wake kwa kumchagua  kuwa mbunge wa  jimbo  hilo la Kilolo jana ,Mwamoto  alisema  kuwa  kero ya maji katika  mji wa Ilula  imekuwa ya muda murefu   jambo ambalo hatataka   kuona   wananchi  hao  wakiendelea kutabika.

Alisema  kuwa   kero hiyo  ya maji imeanza  kuwasumbua  wananchi hao toka nchi ipate  uhuru  wake mwaka 1961  hadi  leo wapo katika mahangaiko ya maji na  baadhi ya  viongozi  wameendelea  kufanya udanganyifu  wa mradi huo kama  ambavyo   mwaka 2010   viongozi  walivyomdanganya aliyekuwa makamu  wa Rais Dr Alli Mohamed  Shein  kwa  kupelekwa  kufungua  mradi wa maji ambao  viongozi  walimdanganya kwa  kujaza maji katika tanki hilo  ili azindue mradi huo.

Hivyo  alisema udanganyifu  huo hautapewa nafasi katika uongozi  wake wa miaka  mitano  lazima kero  hiyo imalizike na  wananchi hao  waweze kupata maji vinginevyo yupo tayari  kuongoza  wananchi  wake kumzuia waziri wa maji kupita Ilula kwenda jimboni kwake Njombe  iwapo  wananchi hao hawatatimiziwa ahadi yao ya maji  safi na salama .

Mbunge  huyo  alisema katika  kikao kijacho cha  bunge kinachoanza mwezi ujao ataomba  wananchi wa Ilula na Nyalumbu  kumteulia wazee watatu ama  wanne   ili kwenda nao bungeni Dodoma  kukutana na  waziri  mkuu ili  kwa ajili ya kumkumbusha ahadi ya Rais ya  maji katika mji  huo wa Ilula .
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhk7WxKewRYdjXwD8lX3crGfa8nBIOAo3SsF0Kg3ruaxfxMEciqaadCRdkopWqNhM03AgYUs8RsDLs9MZqzgf0JjCn8Pxy6UW5N8Q5pK1yZIREUxEtkSekyqD51VvReeSLegJODpoNpmcxU/s640/DSC_0966.JPG

Pia  aliagiza mamlaka ya maji ya mji  mdogo wa Ilula  kuchunguza vema mradi wa maji uliopo kama umejengwa kwa kiwango ama chini ya kiwango maana amesema mradi mdogo  uliopo kwa  sasa  bado umekuwa na kero  kubwa ikiwa ni pamoja na baadhi ya maeneo kuvujisha maji  huku  akiwataka  wananchi kwa  upande  wao kutunza miundombinu ya maji.

Mbunge wa Kilolo Bw  Venance Mwamoto (kushoto)  akisalimiana na mmoja kati ya  wazee wa mji wa Ilula  aliyetoka  kuchota maji


 

Katika  hatua nyingine  mbunge Mwamoto  alimshauri meneja wa maji wa IRUWASA katika mji wa Ilula Teodolah Mvungi  kuangalia uwezekano wa  kuboresha kituo  cha maji eneo la Ilula  ili  kiweze  kunufaisha  wananchi  wengi  na  kuwa iwapo wataanza uboreshaji kwa upande wake ataunga mkono .

Hakuna maoni: