ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumapili, 4 Septemba 2016

TAARIFA KWA UMMA - ILULA

                                             

KIKOTI EDUCATION CENTRE ILULA – MADIZINI
             TAARIFA KWA UMMA

Mkuu wa kituo cha tuition cha KIKOTI EDUCATION CENTRE  kwa niaba ya uongozi wa TUITION CENTRE  na watumishi wote, anapenda kukanusha taarifa iliyoenezwa na mwalimu wa kituo cha MWALIMU EDUCATION CENTRE-Diginayo Kwamba walimu wake wote wameondoka kuelekea masomoni Pamoja na maneno ambatishi na tunaomba endeleeni kuleta na kuandikisha wanafunzi kama kawaida na hatua zaidi za kisheria zinaendelea kuchukuliwa na wanasheria wetu kujua lengo la mwalimu huyo: lakini pia tunaomba umma wa wanailula utambue mambo yafuatayo kutoka mmliki wa kituo hicho kinachojiita MWALIMU EDUCATION CENTRE:
- Hana madarasa ya kufundisha hivo analazimika kufundishia wanafunzi kwenye ukumbi ambao ulikua unatumika kama bar au sehemu ya kuuzia vinywaji ambayo ni kinyume na sheria na taratibu za wizara ya elimu 
- Pia mmliki huyu ni mtumishi wa umma anayepaswa kuwepo kazini mda wote ambapo wanafunzi wenu watakuwa wakipata elimu kwenye ukumbi huo.
- Ameshindwa kufuata sheria na taratibu kwa kusambaza taarifa za uongo kwa wanafunzi alipokuwa akifanya promosheni kwenye shule mbalimbali tena mdaaliopaswa kuwepo kazini yaani kati ya saa nne asubuhi mpaka saa tisa na nusu 
Kama kituo tumefanya mambo yafuatayo,
- Tumemwandikia barua Afisa wa elimu wilaya yenye kumbukumbu no K.E.S/0012/2016 kumjulisha anachokifanya mtumishi wao na kumtaka kupitia Mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi kufanya yafuatayo:
  • kueleza sababu za kusambaza taarifa za uongo  kwa maandhishi.
  • mkurugenzi kutathimini kuona kama ni haki kwa mwajiri wake kufanya tuition mda wa kazi tena katika mazingira hatarishi.
  • mwisho tumemtaka mwalimu huyo kufuta kauli hizi kupitia vyombo hivi vya habari kama tulivofanya sisi.
MWISHO:Tunapenda kuomba radhi kwa wazazi wote mliokuwa mmekwisha kuandisha wanafunzi toka mwezi wa nane kwa hofu mlioipata mda wote na tunaendelea kuwakaribisha wazazi wote kuleta wanafunzi KIKOTI EDUCATION CENTRE -ILULA MADIZINI MAJENGO YA KANISA KATORIKI aweze kupata elimu bora kutoka kwa walimu bora
  Our moto: education for life

MWANASHERIA                                         MKUU K.E.C
 ..........
Alfonce jackson kisoma                                Misael Benitho kikoti
NAKALA,                                                  Tarehe 29/08/2016
mkuu wa Mwalimu Education,           
Mtendaji wa kijiji cha Dinginayo,
Afisa elimu wilaya ya kilolo,
Katibu tawala wilaya na mkoa(DAS&RAS)
Vyombo vya habari Iringa.