ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Ijumaa, 23 Septemba 2016

Mhadhiri chuo kikuu mbaroni kwa kumkashfu Rais Magufuli


Idadi ya watu wanaokamatwa kwa tuhuma za kumkashfu Rais John Magufuli kupitia mitandao ya kijamii imezidi kuongezeka baada ya polisi kumkamata Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa (Muce), Dk Oscar Magava (48).

Dk Magava amekuwa mtu wa kumi kukamatwa na polisi katika kampeni za jeshi hilo kudhibiti uhalifu chini ya sheria ya uhalifu wa mtandaoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi alisema Dk Magava alikamatwa akiwa Sumbawanga na alirudishwa mkoani Iringa.

Mjengi alisema Septemba 15, mwaka huu walipata taarifa kuwa mhadhiri huyo anatumia mitandao ya kijamii kumkashfu Rais. Alisema waliamua kumsaka na walipopata taarifa kuwa Dk Magava amekwenda Sumbawanga waliwasiliana na polisi wa huko wakamkamata na kumrudisha Iringa.

Hata hivyo, Kamanda Mjengi hakuyataja maneno aliyotumia Dk Magava kumkashfu Rais kwa madai kuwa bado wanaendelea na uchunguzi na kwamba ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Kamanda Mjengi aliwatahadharisha wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kuitumia kwa ajili ya maendeleo na si kutukana wala kukashfu viongozi au watu wengine.

Watu mbalimbali wamekuwa wakikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kumkashifu Rais au jeshi la polisi.

Magazeti ya leo ijumaa ya tarehe 23/09/2016























Alhamisi, 22 Septemba 2016

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU UDOM 2016/2017

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU UDOM 2016/2017

<<<DOWNLOAD HAPA  MAJINA HAYO>>> BONYEZA HAPA KUONA MAJINA YA  VYUO VINGINE ...

MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA SELECTION YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017

  
Habari yako, Maswayetu blog,tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hapa...
Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI 337 WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU ARUSHA UNIVERSITY 2016/2017

  Click the link below to download/view the Names2016-2017 NACTE First Selection...
Share:

UDOM:APPLICANTS SELECTED FOR ADMISSION INTO PhD DEGREE PROGRAMMES

  APPLICANTS SELECTED FOR ADMISSION INTO PhD DEGREE PROGRAMMES  APPLICANTS SELECTED FOR ADMISSION INTO PhD DEGREE PROGRAMMES The University of Dodoma (UDOM) wishes to announce the names of candidates selected for admission into various PhD programmes...

Basi laua watu 13 Mwanza


MAISHA ya Watanzania yameendelea kupotea katika ajali za barabarani baada ya ajali nyingine, iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Super Shem kugongana na daladala (Hiace) na kusababisha watu 13 kufa na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa.
Ajali hiyo ilitokea jana saa 12 asubuhi katika kijiji cha Mwamaya, kwenye makutano ya barabara kuu ya Mwanza na ya kutoka Misasi, katika eneo la Hungumalwa.
Basi hilo lililokuwa linatoka Mbeya kwenda Mwanza, liligongana hiace na kuharibika vibaya. Rais John Magufuli amemtumia salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kufuatia vifo vya watu hao 13 na majeruhi wa ajali hiyo.
Mapema wiki hii, basi lingine la New Force linalofanya safari kati ya Dar es Salaam na Songea mkoani Ruvuma, liliacha njia na kupinduka katika kijiji cha Lilombwi Kata ya Kifanya wilayani Njombe, mkoani Njombe na kuua watu 12 huku wengine 30 wakijeruhiwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema imesababishwa na mwendo kasi usio na tahadhari.
Alisema mbali na vifo hivyo 13, watu watatu kati ya majeruhi 10, wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando na hali zao ni mbaya. Msangi akiwa eneo la tukio pamoja na Mongela ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati za Ulinzi na Usalama ya Mkoa, alisema ajali hiyo ni ya saa 12:15 asubuhi na dereva wa hiace akiwa katika mwendo kasi, alishindwa kumudu gari.
Msangi aliyataja magari yaliyohusika katika ajali hiyo kuwa ni la kampuni ya Supa Shem lenye namba za usajili T 874 CWE, lililokuwa linaendeshwa na Anthony Shirima na hiace namba T368 CWQ iliyokuwa ikiendeshwa na dereva ambaye jina lake halijafahamika na hali yake ni mbaya.
Alisema miili ya marehemu tisa, imekwishatambuliwa na ndugu zao, ambapo miili mitatu ya mama na mtoto, haijatambuliwa na imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba; na mwili mmoja umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi.
Aliwataja waliokufa katika ajali hiyo, waliotambuliwa na ndugu zao na makazi yao katika mabano kuwa ni Monica Shiji, Christian Emanuel, Thereza Majengwa (Gulumwa), Lwinzi Kope (Chasalawe) na Mabula Magi (Rukwa).
Wengine ni Isaya Deogratias (Mande), Moses Kamel mkazi wa Dodoma-Kwimba na mama na mtoto ambao kwa sasa bado hawajatambuliwa. Kamanda Msangi alisema ajali hiyo imetokea wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani, hivyo watatumia fursa hiyo kutoa elimu kwa madereva kujua na kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Aliwataja majeruhi watatu, kati ya kumi, waliotambulika kuwa ni Faustine Emmanuel ambaye ni konda wa Hiace, Shija Roketi na mtoto mdogo aliyejulikana kwa jina moja la Martin.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mongela ambaye aliongozana na kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mkoa, alimuagiza Msangi kukamata madereva wazembe ambao hawaheshimu sheria za usalama barabarani.
Salamu za Rais Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam jana, ilieleza kuwa Rais John Magufuli amepokea taarifa ya ajali hiyo ya Mwanza kwa mshituko, kwa kuwa ni siku moja imepita tangu Watanzania wengine 12 kufa katika ajali ya basi la New Force iliyotokea Njombe.
"Nimesikitishwa sana na vifo vingine vya Watanzania wenzetu, waliopoteza maisha katika ajali huko Mwanza, nakuomba Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella unifikishie salamu za pole kwa familia zote zilizopoteza ndugu, jamaa na marafiki katika ajali hii.
Nawaombea wote waliotangulia mbele za haki wapumzishwe mahali pema na pia wote walioguswa na msiba wawe na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi kigumu cha majonzi ya kuondokewa na jamaa zao," alisema Magufuli.
Rais Magufuli pia aliwaombea majeruhi wote wa ajali hiyo, wapone haraka ili waungane na familia zao na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.

Mikutano ya ndani vyama vya siasa ruksa

Imeandikwa na Mroki Mroki
JESHI la Polisi nchini limeondoa katazo lake la mikutano ya ndani kwa vyama vya siasa kuanzia leo.
Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Mssanzya ametangaza kuondoa zuio hilo leo na kusema kuwa makatazo mengine ya mikutano ya vyama hivyo yako pale pale.
Kamishna Mssanzya amesema mikutano ya hadhara na maandamano bado hairuhusiwi lakini wabunge wanaruhusiwa kufanya mikutano yao katika majimbo yao kwa mujibu wa katiba. Polisi imesema imeamua kuruhusu mikutano hiyo ya ndani baada ya kuridhishwa na mwenendo wa shughuli za kisiasa nchini.
Soma Habarileo Septemba 23 kwa habari zaidi

Tundu Lissu Aponea Chupuchupu Dhamana Yake Kufutwa

 Image result for tundu lissu  
Hofu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumfutia dhamana Tundu Lissu ambaye ni mtuhumiwa wa kesi ya uchochezi, imetoweka baada ya mahakama hiyo kukubaliana na utetezi wa  wadhamini wake kuwa, Lissu yupo Ujerumani kwa matibabu.

Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, alishindwa kuhudhuria mahakamani siku ya juzi na hivyo wadhamini wake kutakiwa kufika mahakamani jana kujieleza, kwanini mtuhumiwa huyo asifutiwe dhamana. 

Kesi ya uchochezi inayomkabili Lissu ni kesi Na. 208 katika gazeti la MAWIO akiwa ni mtuhumiwa namba nne sambamba na Jabir Idrissa, Simon Mkina, na Ismail Merhaboob.

Jabir ni mwandishi mwandamizi wa MAWIO, Mkina ni mhariri wa gazeti hilo na Merhaboob ni meneja wa kampuni ya uchapishaji magazeti inayojulikana kwa jina la Flint.
Jana, wadhamini wa Lissu Ibrahim Ahmed na Robert Katula walisimama mbele ya Hakimu Thomas Simba anayesimamia kesi hiyo, na kusema kuwa Lissu hakutokea  mahakamani kwa sababu amesafiri nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Hata hivyo, upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Mutalemwa Kisheruji uliiomba mahakama kuzuia hati ya kusafiria ya mshitakiwa Lissu pamoja na kumuwekea sharti la kuiomba mahakama kibali cha kusafiria endapo atarudia tena kosa hilo kutokana kwamba hakufuata sheria kwa sababu alitakiwa kutoa taarifa mapema kabla ya siku ya shtaka kusikilizwa.

Lakini Hoja hiyo ilipingwa na Wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala na kuiomba mahakama kutenga siku nyingine ambapo alimuahidi hakimu kuwa kosa hilo halitajirudia tena na siku husika ya kusikilizwa shitaka mshatikiwa atakuja mahakamani.

Baada ya kusikiliza maombi ya pande zote mbili, Hakimu Simba alitoa onyo kali kwa mshitakiwa na kuwaambia wadhamini wa Lissu kuwa, endapo siku nyingi mshitakiwa huyo hatakuja mahakamani, wadhamini watalipa dhamana.

Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba, 4, 2016 baada ya mawakili wa pande zote mbili kuiridhia tarehe hiyo iwe siku ya kusikilizwa shtaka hilo.

Magazeti ya Leo Alhamisi ya tarehe 22/09/2016