Alhamisi, 22 Desemba 2016
Jumatano, 21 Desemba 2016
Rais wa Gambia: Hakuna wa kunitoa Madarakani, labda Mungu Pekee
Rais
wa Gambia Yahya Jammeh amesema kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi
wa eneo la magharibi mwa Afrika la kumlazimisha kuondoka madarakani
licha ya kushindwa katika uchaguzi na mpinzani wake, Adama Barrow.
Akihutubia
Wanachama wa Muungano nchini humo Bw. Jammeh amesema: ”Waje wajaribu
kuniondoa wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi
kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka
mshindi”.
“Mimi sio muasi, haki yangu haiwezi kuvurugwa. Hii ni nafasi yangu, hakuna mtu anayeweza kuniondoa labda Mungu,” amesema.
Amesema
kuwa alikataa wito wa Muungano wa Viongozi wa Mataifa ya Magharibi
ECOWAS akiwemo Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf
wa Liberia kuondoka nchini Gambia.
“’Wao
ni kina nani wa kuniambia mimi niondoke nchini mwangu,” amesema na
kuwashutumu viongozi hao kwa kuingilia mambo ya ndani ya Gambia.
ECOWAS
tayari imesema kuwa inamtambua Bw. Barrow kama Rais wa taifa hilo na
kwamba litachukua hatua zozote kuhakikisha kuwa matokeo ya uchaguzi
yanaheshimiwa.
Viongozi wa eneo hilo watahudhuria kuapishwa kwa Bw. Barrow mnamo mwezi Januari 18 kulingana na taarifa ya Ecowas.
Rais
Jammeh awali alikuwa amekubali matokeo ya uchaguzi huo mnamo Desemba 1,
2016 lakini baadaye akaitisha uchaguzi mpya utakaoandaliwa na tume ya
uchaguzi inayomcha Mungu kwa madai kuwa matokeo hayo uchaguzi
yaligubikwa na dosari.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)