ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumatatu, 13 Machi 2017

Siri vigogo kutimuliwa CCM yavuja

 


WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimechukua maamuzi magumu katika historia ya chama hicho tangu kizaliwe kwa kuwafukuza viongozi wa juu wengi kwa wakati mmoja baada ya kubainika kukiuka misingi ya Katiba ya chama hicho, gazeti hili limebaini sababu zaidi za kufukuzwa kwa viongozi hao.
CCM jana ilitangaza uamuzi mzito wa kuwafukuza uanachama, kuwavua uongozi na kuwapa onyo kali vigogo 22 ambao wamechangia kukihujumu na kukifanya chama hicho kinuke mbele ya jamii.
Kupitia Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), CCM imeamua kuchukua hatua hiyo ya kuadhibu viongozi wake baada ya kupokea ripoti kutoka kwa Kamati Kuu (CC) iliyokutana jana asubuhi ambayo nayo ilipokea ripoti kutoka kwenye Kamati Ndogo ya Maadili naNidhamu ya chama iliyoketi mjini hapa juzi.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamprey Polepope ndiye aliyeutangazia umma uamuzi huo na kusema adhabu hizo zimeanza jana. Muda mfupi baada ya kutangazwa kwa uamuzi huo, chanzo cha kuaminika kutoka Dodoma (jina kapuni) kililidokeza gazeti hili kuwa hatua hiyo imetokana na usaliti mkubwa uliofanywa na viongozi hao wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015.

Wajumbe wa CCM wapitisha mabadiliko ya Katiba ya CCM

 
Wajumbe 2,356 wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM leo wamepitisha mabadiliko ya Katiba ya CCM kwa kauli moja chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli

Vigogo wa CHADEMA watimkia CCM. Yumo pia msaidizi wa Mbowe

Wakati Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ulipokuwa ukiendelea mkoani Dodoma, baadhi ya waliokuwa wachama na viongozi wa ngazi za juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na ACT-Wazalendo wamepokelewa rasmi na CCM baada ya kutangaza kujiunga na chama hicho.

Magazeti ya Leo jumatatu ya tarehe 13/03/2017


Jumamosi, 11 Machi 2017

CCM yawatimua makada 12

 
By Mwandishi Wetu, Mwananchi
Dar es Salam. Chama cha Mapinduzi kimewafukuza makada 12 wa chama hicho wakiwemo wanachama mkongwe kama, Sophia Simba, Ramadhan Madabida na Jesca Msambatavangu.
Wakati wanachama hao wakifukuzwa wengine wanne wamepewa onyo kali, sita wamevuliwa uongozi na kuwekwa chini ya uangalizi mkali wa miezi 30, huku mwenyekiti wa chama hicho Dodoma, Adam Kimbisa akisamehewa.
Uamuzi huo umetolewa baada wa kikao cha Nec kilichofanyika Dodoma leo (Jumamosi) na kuongozwa na mwenyekiti wake, Rais John Magufuli.

SOURCE:MWANANCHI

Magazeti ya Leo jumamosi ya tarehe 11/03/2017