Wakati
Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ulipokuwa ukiendelea mkoani
Dodoma, baadhi ya waliokuwa wachama na viongozi wa ngazi za juu wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na ACT-Wazalendo
wamepokelewa rasmi na CCM baada ya kutangaza kujiunga na chama hicho.
Viongozi
hao waliojiunga na CCM leo wamesema sababu kubwa iliyopelekea na
kufikia uamuzi huo ni utendaji kazi wa Rais na Mwenyekiti wa CCM, Dkt
John Pombe Magufuli.
Miongoni
mwa wengi waliopokelewa leo ni pamoja na, Moses Machali Mbunge wa
zamani wa Kasulu Mjini kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi na baadae kuahimia
ACT Wazalendo. Alitangaza kujiunga CCM Novemba mwaka jana ambapo leo
amepokelewa rasmi. Dkt Yared Fubusa, Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya
CHADEMA Mkoa wa Kigoma na Mgombea Ubunge jimbo Kigoma Kaskazini
(CHADEMA).
Mwingine
ni aliyetangaza kujiunga na CCM na kupokelewa na Mkutano Mkuu leo ni,
aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Said Arfi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni