Jeshi
la Polisi nchini linamshikilia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Lissu
aliachiwa leo asubuhi na Hakimu Mkuu Mkazi, Huruma Shahidi baada ya
upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Paul Kadushi kuwasilisha hati ya
kuondoa shtaka hilo.
Kadushi
aliwasilisha hati hiyo chini ya kifungua namba91 (1) cha makosa ya
jinai akionyesha DPP hana haja ya kuendelea na kesi, mahakama ikaridhia
na kumuachia.
Muda
mfupi baada ya kuachiwa na kutoka nje ya mahakama alikamatwa tena na
askari waliokuwapo mahakamani hapo na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi.
Lissu
alikuwa anashtakiwa kwamba Januari 11, mwaka huu katika kampeni za
uchaguzi jimbo la Dimani aliwashawishi watu wasiridhike na wawe na nia
ovu dhidi ya utawala.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni