Watu
12 wamejeruhiwa na watatu kati yao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Iringa baada ya kutokea ajali iliyohusisha magari mawili ya
abiria na lori moja, katika eneo la Mlima wa Kitonga wilaya ya Kilolo
mkoani Iringa.
Akizungumza baada ya kutokea kwa ajali hiyo , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi alisema magari yote matatu yaliyohusika kwenye ajali hiyo yalikuwa yakienda jijini Dar es Salaam.
Ameyataja mabasi yaliyohusika kwenye ajali hiyo kuwa ni ya Kampuni ya Happy Nations, Abood na gari moja la mzigo.
Mjengi
amesema katika ajali hiyo watu 12 walipata majeraha na watatu kati yao
wamefikishwa Hospitali ya Rufaa ya mkoani Iringa kwa matibabu na tisa
kati yao walitibiwa na kuruhusiwa kutoka hospitali.
Kamanda
huyo ametaja chanzo cha ajali kuwa ni dereva wa gari la Abood
lililokuwa nyuma ambaye aliligonga basi la Happy nations ambalo nalo
liligonga gari lilikuwa mbele yake na kusababisha magari yote kuserereka
na kutoka pembeni mwa barabara.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni