Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema wikendi iliyopita alitumia muda wake
kufanya mazungumzo na kada mpya wa chama hicho, Wema Sepetu ikiwa ni
siku mbili tangu aachiwe kwa dhamana baada ya kukaa gerezani kwa
takribani miezi minne.
Lema alimtia moyo na kumpa somo mrimbwende huyo, akimtaka kuwa imara na kujitoa bila kujali ni watu wangapi wanaomuunga mkono.
“Hatuhitaji
taasisi kupigania righteousness (haki), tunahitaji watu makini ndani ya
taasisi. hauhitaji kampani kubwa sana, unahitaji commitment (dhamira),
sacrifice (kujitoa) na determination (uamuzi wa ari).
Lema alimtaka Wema kufikiria vitu vikubwa zaidi na kuwa na ndoto kubwa hata ya kuwa rais wa nchi siku moja.
“Wewe unaweza kuwa kitu cha ajabu, unaweza hata kuota kuwa Rais wa nchi hii… nani ajuaye?” alisema.
Mbunge
huyo machachari alimtaka Wema kujichukulia kama mwanamke shupavu na
kusahau yaliyopita huku akimtia moyo kuwa hata kesi aliyofunguliwa
mahakamani itakwisha pia.
Wema
alitangaza kujiunga na Chadema akitokea CCM siku chache baada ya kutoka
katika selo za polisi jijini Dar es Salaam alipokuwa akishikiliwa kwa
siku zaba akituhumiwa kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya aina ya
bangi.
Alifunguliwa kesi baada polisi kudaiwa kukukuta msokoto wa bangi nyumbani kwake baada ya kumfanyia upekuzi.
==>Msikilize Lema Akimpa Ujumbe hapo Chini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni