Kufuatia
tukio la mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni Askari kumtishia Mbunge Nape
Nnauye kwa kutumia bastola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema
tukio lile halikuwa sahihi na kuagiza hatua zichukuliwe.
Waziri
Mwigulu Nchemba ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusimamia usalama wa
raia na mali zao amesema kuwa, Nape Nnauye si jambazi, hakuwahi kuwa na
taarifa za uhalifu, sasa kwanini mtu amtishe kwa bastola tena mbele ya
umati mkubwa uliojaa waandishi wa habari?
“Mh.Nape
Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa
CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha
kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza
kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro
angefanya nini.”
Aidha,
Waziri Nchemba amesema kuwa amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
(IGP), Ernest Mangu kumbaini mtu huyo aliyefanya kitendo hicho na
kumchukulia hatua stahiki.
“Nahusika
na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha
kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya
uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika
zichukue mkondo wake.”
Nape
Nnauye alitishwa na bastola hiyo jana alipofika katika Hoteli ya Protea
Dar es Salaam kwa lengo la kuzungumza na waandishi wa habari baada ya
Rais Dkt John Pombe Magufuli kumvua Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni