Mbunge
Tundu Lissu amekamatwa na jeshi la polisi asubuhi hii nyumbani kwake na
kupelekwa ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma.
==>Huu ni Ujumbe wa Tundu Lissu alioutumia mtandaoni
Wandugu
wapendwa. Ninaandika haya nikiwa nyumbani kwangu Dodoma. Najiandaa
kwenda mahakamani kwa ajili ya uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya kesi ya
kutaka kuzuia Uchaguzi wa TLS.
Ninawapa
taarifa kwamba nimefuatwa nyumbani na askari wawili kutoka ofisi ya RPC
Dodoma. Sijazungumza nao bado lakini ni wazi wana maagizo ya kunikamata
na kunizuia kuja Arusha kwenye Uchaguzi wa TLS. Wameshindwa kuzuia
uchaguzi wetu mahakamani. Sasa, kama kawaida ya serikali za kidikteta
kila mahali, wanatumia mabavu ya kijeshi.
Wito wangu kwenu mawakili wa Tanzania:
Nendeni
Arusha mkachague viongozi wa TLS watakaopigania haki za binadamu,
utawala wa sheria na demokrasia. Msipofanya hivyo hakuna mtu yeyote,
hata ninyi mawakili, atakayepona kwenye utawala wa aina hii.
Kumbuka,
kama Nimrod Mkono anaweza kufungiwa ofisi na TRA ni wakili gani
mwingine aliye salama??? Kama wakili anaweza kukamatwa mahakamani kwa
kufanya kazi yake ya uwakili, ni nani miongoni mwetu aliye salama???
Nendeni mkapige kura kukataa mfumo wa aina hii.
Mimi naenda mahabusu, na pengine, gerezani. Nawaombeni kura zenu ili niweze kuwaongoza katika kipindi hiki kigumu.
Hiki sio kipindi cha kuwa na viongozi wanaojipendekeza kwa wanaokandamiza haki za watu wetu na haki za mawakili wetu.
Hiki
ni kipindi cha kuwa na viongozi watakaopigania haki zenu na haki za
watu wetu. Mnanifahamu. Nipeni jukumu hili la kuwaongoza kwenye giza
hili nene. Msikubali kuyumbishwa.
Na wachagueni pia Makamu wa Rais, Mweka Hazina wajumbe wa Governing Council watakaokuwa na msimamo kama wa kwangu.
Nawatakieni
kila la kheri. I'll think of you all wherever they'll take me to,
wherever I'll be incarcerated. This too shall pass. The race of man
shall rise again. It always has. Nimemwambia na mke wangu naye aende
Arusha akapige kura. So, everybody to Arusha. Go vote your consciences.
All the best.
TL
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni