Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya leo amepokea vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalumu vyenye thamani ya Shilingi bilioni 3.6 ambavyo vinalenga kutatua changamoto ya upungufu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia .
Akizungumza wakati wa makabidbiano hayo, mhandisi Manyanya amesema baadhi ya vifaa Vilivyopokelewa leo ni pamoja na mashine za kuandika maandishi ya nukta nundu 932, karatasi za kuandikia maandishi ya nukta nundu ream 2548,karatasi ya kurudufishia maandishi ya nukta nundu ream 1150,shime sikio ( hearing Aid) 1150, vifaa vya upimaji kielimu.
Naibu waziri manyanya amewataka maafisa Elimu nchini kote kuhakikisha walimu waliopata mafunzo ya watu wenye mahutaji maalumu wanakwenda kufundisha katika shuke hizo na si vinginevyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni