Jumamosi, 25 Machi 2017
Ijumaa, 24 Machi 2017
Maneno ya na Nape Nnauye hapo jana
Aliyekuwa
Waziri wa Habari, Nape Nnauye amezungumza na Waandishi wa habari akiwa
juu ya gari lake leo maeneo ya St. Peter Osterbay Dar es salaam ikiwa
ni saa chache baada ya taarifa kutoka Ikulu kutangaza kwamba uteuzi wake umetenguliwa.
Hali
hiyo imetokana na Jeshi la Polisi kuuzuia mkutano huo ambapo RPC
Kinondoni alifunga barabara kwa gari kuzuia Gari ya Nape huku akiwataka
waandishi wa habari watawanyike mara moja.
==> Haya ni machache ambayo Nape kayaongea
1.Nia ya mkutano wangu haikuwa mbaya. Nilitaka kuzungumza na waandishi wa habari lakini Polisi wanakuja kunizuia.
2.Mnajua ni kiasi gani nimepigana kuirudisha CCM madarakani? Miezi 28 nimelala porini leo mtu anakuja kunitolea bastola.
3.Jana nilisema kuwa kuna gharama za kulipa wakati unatetea haki za watu. Na nilisema kuwa nipo tayari kuilipa gharama hiyo.
4.Sina kinyongo na serikali wala chama changu. Sikumuuliza Rais siku aliniteua na sitamlaumu kwa kuamua kuniondoa.
5.Niliikuta CCM iko shimoni nikaitoa huko. Uzalendo wangu ndani wa CCM si wa kutiliwa shaka.
6.Kina Kawawa walikuwepo wakapita, sisi tutapita, lakini tujiulize tutawaachia watoto wetu Tanzania ya namna gani?
7.Namshukuru Rais kwa mwaka mmoja alioniamini. Nampongeza kaka yangu Dkt Mwakyembe. Nawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe.
8.Nawaomba mtulie maisha yaendelee. Nape ni mdogo sana kuliko nchi. Kuna mambo mazuri mbele hivyo tuiunge mkono serikali.
9.Nilitamani sana kuendelea kufanya kazi na ninyi waandishi wa habari lakini muda wa aliyeniweka umefika akaamua niondoke.
10.Mimi niliwahi kufukuzwa CCM kwa kusimamia nilichokiamini. Ili mbegu iote na kuchanua, sharti ioze kwanza
11.Vijana naomba msimamie haki yenu
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba Aagiza aliyemtolea bastola Nape Nnauye Achukuliwe Hatua Kali za Kisheria
Kufuatia
tukio la mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni Askari kumtishia Mbunge Nape
Nnauye kwa kutumia bastola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema
tukio lile halikuwa sahihi na kuagiza hatua zichukuliwe.
Waziri
Mwigulu Nchemba ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusimamia usalama wa
raia na mali zao amesema kuwa, Nape Nnauye si jambazi, hakuwahi kuwa na
taarifa za uhalifu, sasa kwanini mtu amtishe kwa bastola tena mbele ya
umati mkubwa uliojaa waandishi wa habari?
“Mh.Nape
Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa
CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha
kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza
kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro
angefanya nini.”
Aidha,
Waziri Nchemba amesema kuwa amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
(IGP), Ernest Mangu kumbaini mtu huyo aliyefanya kitendo hicho na
kumchukulia hatua stahiki.
“Nahusika
na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha
kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya
uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika
zichukue mkondo wake.”
Nape
Nnauye alitishwa na bastola hiyo jana alipofika katika Hoteli ya Protea
Dar es Salaam kwa lengo la kuzungumza na waandishi wa habari baada ya
Rais Dkt John Pombe Magufuli kumvua Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo.
Alhamisi, 23 Machi 2017
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)