ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumatatu, 8 Januari 2018

Matokeo ya darasa la nne na kidato cha pili yatangazwa. Bofya Hapa Kuyatazama

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 22 na 23 mwaka jana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifanya vyema katika mitihani hiyo.

Akitangaza matokeo hayo leo Jumatatu Januari 8, Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani wa darasa la nne wamefaulu  kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo.

Amesema  wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja E, ambao ni ufaulu usioridhisha.

Kuhusu matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde  amesema jumla ya wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa  kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea  na kidato cha tatu.

Dk Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili  51,807 sawa na asilimia 10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu.

Alhamisi, 4 Januari 2018

Mke wa Kingunge afariki dunia mumewe akiwa amelazwa


Mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Peras Kingunge amefariki dunia leo Alhamisi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mtoto wa Kingunge, Kinje Ngombale amethibitisha taarifa hizo na kwamba kifo cha mama yake kimetokea wakati baba yake pia ni mgonjwa.

"Ni kweli mama amefariki na baba amelala kwa sababu ndio kwanza ametoka chumba cha upasuaji aling'atwa na mbwa. Tutamwambia akiamka," amesema

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya tarehe 4/01/2018


        pamoja 2018

Jumatano, 3 Januari 2018

Taarifa Kutoka Mamlaka Ya Mapato TRA


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanya mabadiliko  ya ulipaji kodi kwa wafanyabiashara wadogo ambao watalipa robo ya kwanza ya malipo ndani ya siku 90 badala ya njia ya awali ya kufanyiwa makadirio.

Mabadiliko hayo yatawasaidia wafanyabiashara kuanzia waliposajiliwa tofauti na utaratibu uliokuwepo wa kulipia kodi hiyo hata kabla mfanyabiashara hajaanza kufanya biashara.

Hayo yameelezwa leo Januari 2  na Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Elijah Mwandumbya wakati wa kuzindua kampeni ya usajili wa walipa kodi ambapo amesema wanatarajia kusajili walipakodi  wapya  milioni moja  kwa mwaka 2017/2018.

Mwandumbya amesema TRA hawana wakala yeyote aliyepewa jukumu la kusajili au hata kutoa fomu ya usajili hivyo amewataka wananchi wajihadhari na vishoka ambao watatumia mwanya na kuharibu kampeni hiyo.

"Hatuna mtu yeyote hivyo ni wazi kupitia vyombo vya habari wananchi wanatakiwa kuwa makini kwani usajili utafanyika katika ofisi za TRA na katika vituo maalumu," amesema Mwandumbya.

Amesema kampeni hiyo na mabadiliko hayo yamekuja kwa nia ya kuongeza hamasa kwa wananchi ili wawe na utaratibu wa kulipa kodi.

Mwandumbya ameendelea kusisitiza azma ya serikali kukusanya kodi na kukuza uchumi wa viwanda na kuleta maendeleo kwa Taifa.

Advertisement

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya tarehe 3/01/2018





pamoja 2018