ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumatano, 3 Januari 2018

Taarifa Kutoka Mamlaka Ya Mapato TRA


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanya mabadiliko  ya ulipaji kodi kwa wafanyabiashara wadogo ambao watalipa robo ya kwanza ya malipo ndani ya siku 90 badala ya njia ya awali ya kufanyiwa makadirio.

Mabadiliko hayo yatawasaidia wafanyabiashara kuanzia waliposajiliwa tofauti na utaratibu uliokuwepo wa kulipia kodi hiyo hata kabla mfanyabiashara hajaanza kufanya biashara.

Hayo yameelezwa leo Januari 2  na Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Elijah Mwandumbya wakati wa kuzindua kampeni ya usajili wa walipa kodi ambapo amesema wanatarajia kusajili walipakodi  wapya  milioni moja  kwa mwaka 2017/2018.

Mwandumbya amesema TRA hawana wakala yeyote aliyepewa jukumu la kusajili au hata kutoa fomu ya usajili hivyo amewataka wananchi wajihadhari na vishoka ambao watatumia mwanya na kuharibu kampeni hiyo.

"Hatuna mtu yeyote hivyo ni wazi kupitia vyombo vya habari wananchi wanatakiwa kuwa makini kwani usajili utafanyika katika ofisi za TRA na katika vituo maalumu," amesema Mwandumbya.

Amesema kampeni hiyo na mabadiliko hayo yamekuja kwa nia ya kuongeza hamasa kwa wananchi ili wawe na utaratibu wa kulipa kodi.

Mwandumbya ameendelea kusisitiza azma ya serikali kukusanya kodi na kukuza uchumi wa viwanda na kuleta maendeleo kwa Taifa.

Advertisement

Hakuna maoni: