
Mwanzilishi
 wa tovuti ya JamiiForums, Maxence Melo amekamatwa na Polisi jijini Dar 
es Salaam kwa kukataa kutoa taarifa za watumiaji wa mtandao huo.
Taarifa
 kutoka kwenye tovuti hiyo zinaeleza kuwa Melo amenyimwa dhamana hivyo 
atalazimika kukaa rumande mpaka kesho atakapofikishwa mahakamani.
Jeshi
 la Polisi linadai kuwa Melo amekataa kuonyesha ushirikiano kwa Jeshi 
hilo ambapo walikuwa wakihitaji majina ya baadhi ya watumiaji wa mtandao
 huo.
JamiiForums
 wameeleza kuwa kiongozi huyo (Maxence) alikataa kutoa taarifa hizo kwa 
kile alichoeleza kuwa kufanya hivyo ni uvunjwaji wa Sheria na Haki za 
wananchi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni