ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Alhamisi, 31 Agosti 2017

15,473 tu ndio waliokamilisha maombi Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu

 
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa wanafunzi kuwasilisha maombi ya mikopo.

Hatua hiyo imeelezwa inalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi walioshindwa kufuata masharti kuyakamilisha.

Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema muda huo umeongezwa hadi Septemba 11 badala ya Septemba 4.

"Tumesogeza mbele kwa siku saba zaidi ili walioshindwa kufuata vigezo wakati wa kujaza fomu wafanye hivyo," amesema.

Amesema hadi kufikia jana Agosti 29, wanafunzi waliojitokeza walikuwa 49,282 lakini ni 15,473 waliokamilisha maombi kwa njia ya mtandao. 
Aidha, Badru amewasisitiza waombaji wa mikopo kuzingatia mwongozo uliotolewa na Bodi unaowataka kuambatanisha nyaraka zote zilizothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamimi (RITA), makamishina wa viapo, mawakili na serikali za mtaa na kuziwasilisha kwenye mtandao wa Bodi.
Maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018, yanayofanyika kwa njia ya mtandao olas.heslb.go.tz  yalifunguliwa Agosti 6, 2017.
Mpaka kufikia Agosti 29, 2017, maombi ya mkopo zaidi ya 50,000 yalikuwa yametumwa Bodi ya Mikopo kwa ajili ya uhakiki na baadaye kupangiwa mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
 

Magazeti ya Leo Alhamisi ya tarehe 31/08/2017