Rais
wa Zambia, Edgar Lungu, ametangaza kwamba wananchi wote wanaofika
katika vituo vya afya vya serikali wapimwe virusi vya Ukimwi kwa lazima,
wapatiwe ushauri nasaha na tiba.
Rais
Lungu amesema, sera hiyo mpya inaenda sawia na agenda ya serikali ya
kutokomeza virusi vya HIV nchini humo ifikapo mwaka 2030.
Katika
tangazo hilo, kiongozi huyo amesisitiza umuhimu wa kulinda maisha ya
wale walioathirika na wale ambao wako hatarini kuambukizwa virusi hivyo.
Amesema,
licha ya sera hiyo kukiuka haki ya mtu kupima kwa hiari lakini
akasisitiza kuwa hakuna mtu mwenye haki ya kuweka rehani maisha ya
binadamu mwenzake.
Sera
hiyo inakiuka muongozo wa Shirika la Afya Duniani, WHO, na Shirika la
Ukimwi la Umoja wa Mataifa, UNAIDS, unaohamasisha watu kupima Vvu na
kupata ushauri nasaha kwa hiari.
Zambia ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha maambukizi ya ugonjwa huo kusini mwa bara la Afrika ikiwa na asilimia 11.6 huku watu walio na umri wa miaka kuanzia 15 mpaka 49 wakiishi na virusi vya ukimwi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni