Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba.
Jumla
ya watahiniwa 385, 767 walisailiwa kufanya mtihani kidato cha nne
mwaka 2017, kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio wamefaulu
ambapo wasichana ni 143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985
sawa na asilimia 79.06.
Akitangaza matokeo hayo leo Januari 30,
2018 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema mwaka 2016
watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09.
Amesema
matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na
kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo
mwaka huu.
"Watahiniwa 77 wa shule ambao walipata matatizo ya
kiafya na kushindwa kufanya mtihani watapata fursa mwaka 2018," amesema
Dk Msonde.
Dk Msonde amesema watahiniwa 265 waliobainika kufanya
udanganyifu katika mitihani matokeo yao yamefutwa huku mtahiniwa mmoja
akiandika matusi katika karatasi yake ya majibu.
==>Yatazame Matokeo hapo chini
Link 1: Matokeo Ya Mtihani Wa Kidato Cha Nne (Csee) 2017
Link 2: Matokeo Ya Mtihani Wa Kidato Cha Nne (Csee) 2017
Link 1: Matokeo Ya Mtihani Wa Maarifa (Qt) 2017
Link 2: Matokeo Ya Mtihani Wa Maarifa (Qt) 2017
Link 2: Matokeo Ya Mtihani Wa Kidato Cha Nne (Csee) 2017
Link 1: Matokeo Ya Mtihani Wa Maarifa (Qt) 2017
Link 2: Matokeo Ya Mtihani Wa Maarifa (Qt) 2017