Mbunge
wa Kawe, Halima Mdee, anatarajia kufikishwa mahakamani Jumanne Aprili
3, kuungana viongozi wengine wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), akiwamo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, wanaoshtakiwa kwa
makosa manane yakiwamo uchochezi, kuhamasisha maandamano na uasi.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hayo
leo na kuongeza kuwa mbunge huyo amekiuka masharti yaliyomtaka kuripoti
kituo cha polisi pamoja na viongozi wengine saba wa chama hicho kabla
ya kufikishwa mahakamani.
Halima
alikamatwa leo Jumapili Aprili Mosi, saa tisa alfajiri katika Uwanja wa
Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), alipokuwa akirejea nchini
akitokea Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu.
Aidha,
alipoulizwa ni kwanini Halima amekamatwa wakati mawakili wake walikuwa
wakitoa taarifa zake, Mambosasa amesema: “hayo ni maneno tu, anafahamu
taratibu zikoje, anafahamau sheria zinasemaje kwa sababu wanatunga
wenyewe huko bungeni hilo si suala la kujadili na mimi, asubiri atajibu
hayo mahakamani.
Mambosasa
amesema hayo muda mchache baada ya Chadema kulitaka Jeshi la Polisi
kumpatia dhamana Mbunge ili aweze kuendelea na matibabu.
Mkurugenzi
wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje ya chama hicho, John Mrema
amesema licha ya kwamba Mbunge huyo kuwa mgonjwa ambaye hivi punde
ametoka hospitali, lakini pia dhamana ni haki yake na lawama zote
zitakuwa juu yao endapo afya ya mbunge huyo itatetereka.
“Hadi
mchana wa leo Aprili Mosi, Jeshi la Polisi limeendelea kumshikilia
Katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam na hajapatiwa dhamana pamoja
na daktari wake kuwathibitishia polisi kuwa Mheshimiwa Halima ni
mgonjwa.
“Tunasikitishwa
na kulaani kitendo hiki cha polisi kuendelea, kumshikilia mgonjwa
ambaye alikuwa amelazwa hospitalini, , tumetuma mawakili daktari wake
lakini hawajafanikiwa mwisho, Jeshi la Polisi litawajibika kwa
Watanzania endapo afya ya Halima Mdee ikitetereka au ikidhoofu zaidi na
lawama zote zitakuwa juu yao,” amesema Mrema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni