Jumanne, 23 Agosti 2016
Jumatatu, 22 Agosti 2016
Jumapili, 21 Agosti 2016
Jumamosi, 20 Agosti 2016
Watakaochakachua Mitihani Kidato cha Nne Kukiona
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema haafiki uchakachuaji kwenye mitihani na kusema wakuu wa shule watakaobainika kufanya udanganyifu huo hawatapona.
Profesa
Ndalichako alisema hayo kwenye kikao kati ya Ofisi ya Rais, Tamisemi,
Maofisa Elimu wa Mikoa, Wakuu wa shule kongwe na wakuu wa shule
zilizoungua moto.
Alisema
ikiwa imebaki miezi mitatu kwa wanafunzi wa kidato cha nne kufanya
mitihani aliwataka wakuu wa shule kujipanga kupata ufaulu mzuri.
“Bado
siafiki suala la uchakachuaji kwenye mitihani wanafunzi waachwe wafanye
mitihani wenyewe na si kupitia kamati za ufundi, sasa Wizara inaangalia
ubora wa elimu na wakuu wa shule watakaokiuka agizo hilo watachukuliwa
hatua,” alisema.
Alisema
pia matokeo ya mitihani ya shule za sekondari ya mwaka jana
yalimhuzunisha sana lakini anaamini wakuu wa shule watajipanga
kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri zaidi.
“Nilipokuwa
Baraza la Mitihani nilisema nisiulizwe kutokana na matokeo kuwa mabaya
lakini sasa niko Wizara ya Elimu siwezi kukwepa hilo tena,” alisema.
Waziri
Ndalichako alisema watabadilisha mfumo wa namna maofisa elimu
watakavyofanya kazi zao ili kuongeza kiwango cha ufaulu katika shule za
serikali na kuwataka wakuu wa shule na maofisa elimu kila mmoja
ajipange.
Aidha
alisema mkuu wa shule ni mdhibiti wa taaluma katika eneo lake na
hatakiwi kumuogopa mtu anayemuongoza. Waziri huyo pia alisema katika
mtihani wa kidato cha sita uliopita shule 100 za kwanza shule za
serikali zilikuwa tatu na kuwa nafasi ya 53 ndio ilishikwa na Ilboru ya
Arusha.
“Mpaka
namba 100 shule za serikali ni tatu tu, sio kitu cha kawaida hapa ndio
mahali pa kuzungumza kama serikali tunashindwa kuonesha mfano tuachie
sekta binafsi,” alisema
Mfanyabiashara Moshi Ajimwagia Petroli na Kujipiga Kiberiti
lnawezekana
likawa tukio baya lililoacha gumzo na simanzi baada ya mfanyabiashara
wa mjini Moshi, Romani Shirima (74), kujiua kwa kujilipua kwa petroli
nje ya nyumba yake.
Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema mfanyabiashara huyo alijifunika kwa blanketi, kisha kujimwagia petroli na kutumia kibiriti kuwasha moto ambao ulimlipua na kusababisha kifo chake.
Habari kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema mfanyabiashara huyo alijifunika kwa blanketi, kisha kujimwagia petroli na kutumia kibiriti kuwasha moto ambao ulimlipua na kusababisha kifo chake.
Ingawa hakuna taarifa rasmi ya nini kiini cha mfanyabiashara huyo kuchukua uamuzi huo mgumu ulioacha maswali mengi, lakini baadhi walidai ni msongo wa mawazo uliotokana na madeni.
Hili
ni tukio la pili kwa mfanyabiashara mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro, kwani
miaka kadhaa iliyopita, mfanyabiashara anayemiliki hoteli eneo la
Marangu alijilipua kwa petroli akiwa katika gari lake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi, saa 11.25 asubuhi maeneo ya Mjohotoni.
Alisema, mfanyabiashara huyo ni mmiliki wa shule ya sekondari ya Merinyo iliyopo mjini Moshi, na kusema kuwa aliamka asubuhi nyumbani kwake na kujimwagia mafuta hayo na kisha kujilipua na kiberiti.
Kamanda
Mutafungwa alisema chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika ingawa
kuna maneno yanayoongelewa na watu, lakini hawawezi kuyachukua moja kwa
moja na kwamba jeshi hilo linachunguza ili kubaini chanzo chake.
Taarifa
za tukio hilo la aina yake zimekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali ya
mji wa Moshi na vitongoji vyake, hasa njia aliyoitumia kukatisha uhai
wake.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)