Matokeo hayo yanaipa timu hiyo pointi tatu muhimu zinazoiweka kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 29 nyuma ya Yanga inayoongoza ligi kwa pointi 30 lakini ikiwa mbele kwa mechi moja.
Mabao ya Azam iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo yote yalifungwa katika kipindi cha kwanza. Ame Ali alifunga bao la kuongoza katika dakika ya 10 huku mwenzake Didier Kavumbagu akifunga katika dakika ya 20.
Mchezo huo ulichezwa huku kukiwa na mvua kubwa iliyosababisha mpira kukwama kwenye madimbwi ya maji uwanjani. Ligi hiyo ilichezwa tena kwenye uwanja wa Karume Ilala Dar es Salaam ambapo wenyeji JKT Ruvu walilazimishwa sare ya mabao 2-2 na Coastal Union.
Mabao ya Coastal yalifungwa na Miraji Selema katika dakika ya 20 na Nassoro Kapama dakika ya 75. Wafungaji wa JKT ni Musa Juma katika dakika ya 61 na Samuel Kamuntu katika dakika ya 63.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni