Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya
wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo
vya ufundi kwa mwaka 2017 huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa.
Simbachawene
ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi ws
habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75
ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015.
Waziri
amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la
tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha
tano na vyuo vya ufundi.
Waziri
Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani
wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya
mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa
shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na
asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara.
Simbachawene
alisema kutokana na mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
wa Mei 15, 2017 jumla ya wanafunzi 93,019 ndiyo wenye Sifa za
kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa kuwa
wamefaulu vigezo vyote vya msingi kama vilivyoaibishwa na Wizara ya
elimu sayansi na teknolojia ambapo kati ya hao 92,998 ni wa shule na
wanafunzi 21 ni wale waliosoma taasisi ya elimu ya watu wazima.
Aidha
amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano
kuwasili kwa wakati katika shule walizopangiwa July 17 mwaka huu na
kwamba hakutakuwa na mabadiliko ya shule walizopangiwa.
"Na
kama kuna mwanafunzi ambaye hataripoti kwenye shule aliyopangiwa kwa
muda wa siku 14 nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine," alisema
Simbachawene.
Kuangalia majina ya wanafunzi na shule walizochaguliwa
TAARIFA KWA UMMA
Tafadhali bofya chini Kujua Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha 5 na Vyuo vya Ufundi Mwaka 2017.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni