ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumanne, 26 Julai 2016

Mtuhumiwa kesi ya Mwangosi atiwa hatiani kwa kuua bila kukusudia


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmpnDZn_lC00nOhC3EOpD3F74leljmp9L29_c6IwS6ZA2E-xGWe5Hr0R4DFljtBHE5FYKicxILTkPGPHNsiH6VvnvGt-oHRTkNpU__e_YCIzxkkDjv0iUmDvC_hx9KXKKQZnnJYwo0JpQ/s1600/1.jpg

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Iringa imemtia hatiani askari Polisi, Pacificius Cleophace Simoni, kwa kosa la mauaji ya bila kukusudia ya mwanahabari Daudi Mwangosi yaliyotokea Septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Kwa mara ya kwanza Simoni alifikishwa mahakamani hapo Septemba 12 mwaka 2012 akituhumiwa kufanya kwa kukusudia mauaji hayo wakati mwandishi huyo alipokuwa akiwajibika katika kazi zake za kutafuta habari kwenye ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa Jamhuri umeilazimisha mahakama hiyo chini ya Jaji Kihwelo kuibadili kesi hiyo kutoka kwenye mauaji ya kukusudia na kuwa mauaji ya bila kukusudia ambayo hukumu yake ameisogeza mbele hadi kesho Jumatano.

Baada ya mabadiliko hayo, wakili wa upande wa Jamhuri, Adolph Maganga, aliiomba mahakama hiyo imhukumu mtuhumiwa huyo kifungo cha maisha jela kwa mujibu wa Kifungu cha 198 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu huku wakili wa utetezi, Lwezaula Kaijage akiiomba mahakama hiyo impunguzie adhabu kwa kumfunga kifungo cha nje.

Wakati akitetea hoja yake ya kuiomba Mahakama itoe adhabu ndogo ya kifungo cha nje kwa mtuhumiwa huyo, Lwezaula aliisihi mahakama hiyo imuonee huruma mtuhumiwa huyo kwa kosa alilolifanya bila kukusudia kwa sababu ni kijana mdogo mwenye miaka 27 anayetegemewa na Taifa kama nguvu kazi.

“Na alishiriki operesheni iliyosababisha maafa hayo bila ridhaa yake, amekaa mahabusu kwa miaka minne na katika kipindi hicho atakuwa amejutia sana kosa lake, amefiwa na wazazi wake wote wawili, ana wadogo zake watano wanaomtegemea na ana mke na mtoto mmoja mdogo,” alisema wakili huyo wakati akitoa ombi hilo.

Kwa msingi huo, wakili huyo alitumia Kifungu cha 38(11) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kuomba Mahakama imhurumie mtuhumiwa huyo na kumfunga kifungo cha nje.

Akisoma maelezo ya kesi hiyo kabla ya kuibadili na kuwa na mauaji ya bila kukusudia, Jaji Kiwehlo alisema upande wa Jamhuri ulileta mashahidi wanne ambao kati yao watatu walitoa ushahidi ulioshindwa kuithibitishia moja kwa moja Mahakama kama mtuhumiwa huyo alikusudia alipofanya mauaji hayo.

Huku akishangaa kwa nini Jamhuri pamoja na kuwa na rasilimali za kutosha ilishindwa kuwaleta mashahidi wengine muhimu kama Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa wa wakati huo, Michael Kamuhanda na Ofisa Upelelezi wa Mkoa Wankyo, aliwataja mashahidi hao kuwa ni Said Mnuka, Azel Mwampamba na Lewis Obado ambao pia wote walikuwa askari Polisi wa vyeo tofauti.

Alisema ushahidi pekee uliomtia hatiani mtuhumiwa huyo ni ushahidi uliotolewa na shahidi namba tatu ambaye ni mlinzi wa amani, Flora Mhelela. 
Mlinzi huyo wa amani aliwasilisha mahakamani hapo ungamo la mtuhumiwa huyo lililomhusisha na mauaji hayo na ambalo wakati likiwasilishwa upande wa utetezi haukulikana pamoja na kwamba ulikuja kulikana baada ya ungamo hilo kuwasilishwa mahakamani hapo.

Kwa kupitia ungamo hilo ambalo Mahakama imejiridhisha bila shaka yoyote kwamba maelezo yake yalitolewa kwa hiari na mtuhumiwa huyo; mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na mauaji hayo japokuwa alisema yalikuwa ni ya bahati mbaya.

Sehemu ya ungamo hilo lililosomwa mahakamani hapo kwa mara nyingine tena na jaji huyo linasema; “Niliondoka kutoa msaada nikiwa na long range ambayo ni silaha inayotumika kupigia mabomu ya kishindo na machozi kama inavyoonesha katika gazeti la Mwananchi la Septemba 3, 2012.”

“Pale katika eneo la tukio bila kujua wala kufikiria likafyatua bomu, likafunguka likamuua mwandishi Daudi Mwangosi na kumjeruhi OCS ambaye alikumbatiwa na marehemu, pia kuwajeruhi askari wengine watatu waliokuwa karibu yangu na marehemu.”

Watu mbalimbali walijitokeza kusikiliza kesi hiyo ni pamoja na Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deo Nsokolo na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deudatus Balile. 
Wengine waliojitokeza kuhudhuria kesi hiyo ni pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu, wanahabari wa Mkoa wa Iringa na wananchi wa Manispaa ya Iringa.
ADVATISMENT   kikoti education centre
KIKOTI EDUCATION CENTRE (K.E.C)
MAHALI: ILULA MADIZINI KARIBU MAJENGO YA KANISA KATORIKI

Mzazi/Mlezi wa ……………………………………………….kikoti education centre inapenda kukutarifu

Mchungaji Anthony Lusekelo Adai Lowassa ni Tishio CCM......Asema Uchaguzi Umekwisha

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhzBXBLoQ41aNJay6Njhz8MmvFkBMVm53SAfi47l3NpjmwR832oJX8aSsKjdqSCoqqEzyagVW0g9IoDKvdDcxwc-J_t9UqnL7IJ_fAx4w5Pp9GHYwaVjhiE9wnEnAGZDyqWIgjTI2m9Gmg/s1600/1.jpg
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo maarufu ‘Mzee wa Upako’ amesema kitendo cha viongozi wa CCM kulitaja zaidi jina la Edward Lowassa katika Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho ni ishara kuwa Waziri Mkuu huyo wa zamani ni tishio.

“Nani! Lowassa…. jina lake kutajwa sana katika vikao vya CCM. Hiyo inaashiria kuwa ni mtu tishio. Ndiyo ni tishio,” alisema Lusekelo jana katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
Lusekelo ambaye hivi karibuni, Rais John Magufuli alishiriki ibada katika kanisa lake, alimzungumzia Lowassa baada ya kuulizwa swali juu ya mtazamo wake kuhusu Mkutano Maalumu wa CCM ambao jina la mgombea huyo wa urais kupitia Chadema na Ukawa lilitajwa na makada wengi wa chama hicho tawala. 
Alisema hilo lilidhihirika hata katika mchakato wa CCM kupata mgombea wake wa urais, kutokana na Lowassa kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa. 
Alisema kitendo cha Waziri Mkuu huyo wa zamani kuzua mjadala katika Mkutano Mkuu wa chama hicho tawala sambamba na wimbi la makada wanaohama vyama vyao, si mambo yanayopaswa kuwa mjadala kwa sababu uchaguzi ulishapita. 
Huku akisema: “Sizungumzi haya kwa ajili ya kujipendekeza, sihitaji ukuu wa wilaya,” Lusekelo aliwataka viongozi kukataa kuendeleza uhasama wa kisiasa na chuki kwa maelezo kuwa mwaka huu uwe maalumu kuzika tofauti hizo, kufanya kazi kulijenga Taifa na kuhubiri amani na umoja. 
Katika mkutano huo, Lusekelo alipongeza kuimarika kwa vyama vya upinzani akaponda mvutano ulioibuka bungeni akisema kukosa uzoefu kwa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kulichangia huku akiunga mkono kauli ya Rais kuzuia shughuli za siasa na kubainisha jinsi Rasimu ya Katiba ya Tume ya Jaji Joseph Warioba, ilivyopendekeza kupunguzwa kwa madaraka ya Rais. 
Jumamosi iliyopita, katika Mkutano Mkuu wa CCM mjini Dodoma, uliomalizika kwa Rais Magufuli kuchaguliwa kuwa mwenyekiti, mzimu wa Lowassa ulitawala kutokana na kila aliyepewa nafasi ya kuzungumza ama kumtaja kwa jina au kwa mafumbo. 
Mwenyekiti wa CCM aliyemaliza muda wake, Jakaya Kikwete ndiye aliyeanza kuzungumzia hali ya mchakato wa chama hicho kupata mgombea wake wa urais, kuwa ulikuwa mgumu na majaribu makubwa na kwamba wazee walifanya kazi kunusuru hali hiyo.
Katika mchakato huo, CCM ilikata jina la Lowassa katika hatua za awali, jambo lililosababisha kiongozi huyo kuhama na kundi la wanaCCM na kujiunga na Chadema ambayo ilimteua kuwa mgombea wake wa urais. 
Hata hivyo, katika mkutano wake wa jana, Lusekelo alisema katika mchakato wa chama hicho tawala kupata mgombea wake wa urais kulikuwa na watu wenye majina makubwa, akiwamo Lowassa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe. 
“Niliwaambia CCM, Membe huwezi kumpuuza, Lowassa naye huwezi kumpuuza maana wanataka madaraka na kwa vyovyote lazima mtapata mtikisiko. Nikawaomba waahirishe suala la kupata Katiba Mpya maana wasingelimaliza na muda ulikuwa mfupi,” alisema na kuongeza: “Kama mwaka huu hautatumika kutibu majeraha yaliyotokea huko nyuma, tutaharibikiwa sana.” 
Alisema mchakato wowote wa uchaguzi na kura ya maoni ndani ya vyama huacha mpasuko na watu hutumia dini na ukabila kubaguana, hivyo lazima baada ya uchaguzi mambo hayo yamalizwe. 

“Tunapaswa kukumbuka kuwa wote ni Watanzania tusahau uchaguzi. Sasa ni wakati wa kuijenga nchi. Amani inatengenezwa, na Mungu huwapa hekima maana kujenga ni kazi na kubomoa ni rahisi, huu ni mwaka wa uponyaji na kurejesha Taifa pamoja,” alisema Lusekelo. 
Alisema kuanza kubagua watu kwa sababu walitoka CCM kwenda Chadema au kutoka Chadema kwenda chama tawala si jambo sahihi huku akitolea mfano mataifa yaliyovurugika kwa kuendekeza siasa za chuki na uhasama. 
Yaliyotokea bungeni 
Akizungumza yaliyotokea bungeni na kusababisha wabunge wa Ukawa kususia vikao vya Bunge vilivyoongozwa na Dk Tulia, Lusekelo alisema Mtanzania anayejua historia ya nchi yake hawezi kufumbia macho suala hilo. 
“Binafsi nawalaumu waliotoka (wabunge wa upinzani) na waliobaki (wabunge wa CCM). Kushindana si kuzuri. Mbatia (James Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi) na wenzake wanapaswa kujua kuwa naibu spika ni mchanga katika siasa waende naye taratibu maana kapewa ubunge tu na kuwa naibu spika,” alisema. 
Huku akiponda uamuzi wa Serikali kufuta urushwaji wa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge alisema: “Nashangaa wazee kama Salim (Ahmed Salim – Waziri Mkuu mstaafu), Pinda (Mizengo – Waziri Mkuu mstaafu) na Warioba. Sijui walishindwa nini kukaa na wabunge hawa ili kumaliza tofauti zao.”
Alisema si jambo jema kuongoza nchi kwa mabavu na kusisitiza kuwa hata uhuru ulipatikana kwa mazungumzo. 

Mchungaji huyo aliusifu utawala wa Rais Magufuli kuwa una kasi kubwa na kwamba licha ya wananchi kulia ukata, watacheka baada ya mwaka mmoja huku akiwananga wanaomponda Kikwete kuwa hawajui mazuri aliyoyafanya. 
Awapongeza wapinzani 
Akizungumzia nguvu ya vyama vya upinzani, Lusekelo alisema ushindani wa kisiasa umekuwa mkubwa kutokana na kuimarika kwa upinzani: “Chadema ya sasa si ile ya miaka ya 1990. Wanaongoza miji mikubwa na ukiona chama kina wabunge 40 usikipuuze. Hata nguvu ya mfalme ni watu.” 
Mikutano ya siasa
Kuhusu kauli ya Rais kusitisha shughuli za siasa hadi mwaka 2020, alisema jambo hilo linaweza kuonekana baya lakini lina unafuu mkubwa, kwamba Kenya wamelifanya na kufanikiwa kumaliza tofauti za kisiasa. 
“Hivi watu 10,000 wakiandamana na kusema Magufuli aliiba kura itakuwaje? Tuna askari wa kuwazuia! Nadhani wanasiasa wafanye kazi ya utawala katika vyama vyao. Tutulie kwanza tutibu majeraha. Hakuna jambo baya kama kuwaongoza watu wenye njaa maana hawana la kupoteza,” alisema. 
Hata hivyo, Lusekelo alisema Rasimu ya Katiba ilipendekeza Rais kupunguziwa madaraka na huenda madaraka makubwa aliyonayo Rais yakawa sababu ya nchi kuendelea kuwa na amani. 
“Kenya kuzuia maandamano ni ngumu sana lakini hapa kwetu hadi Zitto (Kabwe-Kiongozi wa ACT-Wazalendo) alizuiwa kufanya mkutano wa ndani. Kwetu rais ana madaraka makubwa sana,” alisema huku akiwataka polisi kutekeleza wajibu wao vyema, wakikumbuka kuwa nao ni binadamu. 
ADVATISMENT   kikoti education centre
KIKOTI EDUCATION CENTRE (K.E.C)
MAHALI: ILULA MADIZINI KARIBU MAJENGO YA KANISA KATORIKI

Mzazi/Mlezi wa ……………………………………………….kikoti education centre inapenda kukutarifu

Magazeti ya Leo jumanne ya tarehe 26/07/2016


















ADVATISMENT   kikoti education centre
KIKOTI EDUCATION CENTRE (K.E.C)
MAHALI: ILULA MADIZINI KARIBU MAJENGO YA KANISA KATORIKI

Mzazi/Mlezi wa ……………………………………………….kikoti education centre inapenda kukutarifu

Jumatatu, 25 Julai 2016

NI VEMA UKAYAJUA HAYA KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA:


1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa ni ya maisha yote.
2. Mwanamume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada ya Ndoa.
3.Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema.
4. Ukikitaka ambacho hakijawahi milikiwa na mtu yeyote, ni lazima ufanye jambo ambalo halijawahi fanywa na mtu yeyote.
5. Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na Shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu.
6. Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa ama kuolewa na mtu asiye sahihi.
7. Aina tatu za wanaume wakuepukwa:
(a) Walevi
(b) Wazinzi
(c) Wagomvi.
Aina tano za wanawake wa kuepukwa;
(a) Walevi
(b) Wazinzi
(c) Wachawi
(d) Wagomvi
(e) wasio tii
8 .Kuolewa na Mchekeshaji hakutakufanya uwe na Ndoa yenye furaha.
9. Maneno matatu yanayojenga amani katika Ndoa:
(a) Nakupenda.
(b) Samahani.
(c) Asante.
10. Kupiga punyeto kwa mwanaume na kujichua kwa mwanamke ni kuharibu mwili wako mwenyewe.
11. Kuoana kabla ya kuwa marafiki ni kama gari bila mafuta. Hamuwezi kufika popote.
12. Mafanikio ya Ndoa siku zote ni pembetatu:
>Mungu mmoja
> Mume mmoja
> Mke mmoja.
13. Furaha ya kudumu maishani hutegemea na chaguo lako la mwenzi ktk Ndoa.
14. Usioe/kuolewa na pesa au mali. Oa/Olewa na mtu. Pesa/Mali hufilisika lakini utu hudumu milele.
15. Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko Ndoa isiyo na amani wala furaha.
16. Usiweke kipaumbele chako kwa muonekano mzuri wa mwanamke. Hakuna mwanamke mbaya, bali anahitaji kupendezeshwa.
17. Mapenzi si upofu. Upofu ni kuoa ama kuolewa na mwanamume/mwanamke kwa sababu tu anakidhi haja zako kingono.
18. Ukiwa rafiki mwema, utawavutia marafiki wema. Vivyo hivyo kwa marafiki wabaya (Bad company corrupt good character)
19. Asili ya mikono inayojali ni moyo unaojali.
20. Iepuke Ndoa mbaya kabla haijaanza...
""Mungu awabariki Sana"".

Askofu Gwajima amjibu Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba aliyemuita muongo

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemjibu katibu mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtuhumu kuwa ni mwongo akisema leseni yake ni ya kuendesha magari makubwa na siyo vibajaji na maguta. 
Akihubiri katika kanisa lake jana, Gwajima bila kutaja jina la Makamba, alisema: “Siwezi kushughulika na vigari vidogovidogo nyie mnanifahamu, mimi nina leseni ya kuendesha semi trailer …nadhani mmenielewa,” alisema huku waumini wake wakimshangilia. 
Juzi, Makamba aliwaeleza wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM kuwa Askofu Gwajima ni kiongozi wa dini lakini ni muongo na kuwa uongo wake unawaudhi hata waumini wake ambao ni wanachama wa chama hicho. 
Alisema Gwajima amekuwa akisema uongo kuwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete hataki kuachia madaraka ya uenyekiti wa chama hicho, kitu ambacho Rais huyo mstaafu alikanusha akisema ni yeye alikwenda kumshawishi Dk John Magufuli kuchukua nafasi hiyo kabla ya muda wa uliopangwa kikatiba. 
Katika mahubiri hayo, Gwajima pia alisema mafunzo aliyoyapata tangu akiwa mdogo ni kuogopa kugombana na watu wa aina tatu, walevi, wazee na wagonjwa. 
“Baba yangu alinifundisha nisigombane na walevi, wazee na wagonjwa kwani ukimpiga kidogo mtu wa aina hiyo anaweza kufa,” alisema Gwajima. 
“Hata nyie waumini wangu nawaomba msigombane na watu wa aina hiyo kwani mnaweza kupata matatizo,” alisema. 
Kiongozi huyo aliongoza mamia ya waumini wake kumuombea Rais Magufuli kwa kushinda uenyekiti wa CCM akisema kofia hizo mbili zimempa meno ya kung’ata na zitamwongezea kasi ya kutatua matatizo ya wanyonge nchini.
Rais Magufuli juzi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM baada ya kupata kura zote 2,398 alizopigiwa na wajumbe wa mkutano huo. 
Kutokana na ushindi huo, Gwajima alisema Magufuli amepewa meno ya `kung’ata’ kila upande tofauti na alipokuwa na kofia moja ya urais. 
Alisema kwa muda mfupi aliokaa madarakani, elimu ya msingi na sekondari zimeanza kutolewa bure kitendo ambacho maskini na wanyonge wa nchi hii wameanza kuuona mwanga. 
Alisema ataendelea kumwombea Magufuli kwa sababu kazi anazozifanya zinawanufaisha wanyonge na maskini ambao kwa muda mrefu walipuuzwa katika nchi yao.
“Kuchaguliwa kwake kuwa mwenyekiti ni zawadi kwetu Watanzania, tuendelee kumwombea kila siku ili aendelee kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi,” alisema. 
Alisema nafasi hiyo mpya itamwezesha kupambana na rushwa tatizo ambalo ameonyesha kuwa `atalivalia njuga’ hata ndani ya chama hicho. 
Mbali na Rais Magufuli, Gwajima aliwaombea pia Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri na Spika wa Bunge kwamba Mungu awalinde ili wamsaidie Rais kutekeleza majukumu yake. 
Kwa mwezi mzima, Askofu Gwajima amekuwa akitafutwa na Polisi baada ya kusambaa kwa sauti inayosikika kama yake ikitaka Rais mstaafu Kikwete afikishwe mahakamani kwa makosa yote yaliyofanyika katika utawala wake. 
Katika mkanda huo, sauti hiyo inadai baadhi ya viongozi wa CCM wametuma watu mikoani kupiga kampeni ya kutaka Magufuli asipewe uenyekiti ambao umekuwa ukishikiliwa na Kikwete. 
Baada ya sauti hiyo, Gwajima aliondoka nchini kwenda Japan lakini Polisi waliendelea kumsaka hadi Julai 12 walipomkamata katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), aliporejea. Alihojiwa na kuachiwa siku hiyohiyo.

Magazeti ya Leo jumatatu ya tarehe 25/07/2016