Mbunge
wa Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa amewataka wananchi wa Iringa Mjini
kumchomea nyumba anayoishi pamoja na magari yake endapo atahama Chama
cha Demokrasia na Maendeleo na kuhamia CCM.
Msigwa
amefunguka hayo wakati akituma salamu kwa wale ambao wamekuwa
wakimrubuni kuhamia CCM na kusema kwamba heshima na dhamana aliyopatiwa
na wananchi wa Manispaa ya Iringa ni kubwa mno hivyo kufanya hivyo ni
kuuza hadi utu wa wapiga kura.
Msigwa
ameweka wazi kwamba amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka upande wa
chama tawala wakimtaka akubali kupokea ofa yao ya kuhama chama na bila
hivyo basi hataweza tena kurudi bungeni baada ya kufika 2020.
"Nikihamia
CCM wananchi wa Iringa wachome nyumba yangu na magari yangu. Sikuingia
bungeni kwa sababu nataka hela ila nimeingia kwa sabu kuna hoja kuna
agenda na kozi kama chama tunapigania. Mkome kabisa kunipigia simu mimi
sina bei itakayonihamisha CHADEMA," amefunguka Msigwa
Akizungumzia
kuhusu alivyokuwa akirubuniwa, Msigwa amesema "Walianza kunipigia kwa
kujifanya marafiki zangu na baadae wakaanza kunipanga na kunirubuni
kwamba Mzee ananikubali na wala hana shida na mimi hivyo nikiingia CCM
nitapata nafasi, nimewakemea na nimeonya wasinipie simu na sasa hivi
wameacha ila naahidi wakinipia tena nitawarekodi niwaanike hadharani" I
am not that 'cheap' wakatafute wengine," Msigwa ameweka wazi
Aidha
Msigwa amefafanua kwamba hakuuingia bungeni kwasababu anahitaji pesa
kwani hata kama asingekuwa Mbunge angeweza kuwa Mkurugenzi wa makampuni
na kuongeza kwamba alikuwa na maisha hata kabla ya kuwa mwanasiasa na
mbunge.
"Sikuingia
Bungeni kwa ajili ya pesa, sipo tayari kurubuniwa kwa maneno matamu
wala fedha au ushawishi kuuza utu ambao wananchi wa manispaa ya Iringa
wamenipa. Ukiniangalia kwani nashindwa kuwa CEO, naweza kuwa Mkurugenzi
wa kampuni yoyote. Mimi nilikuwa na maisha kabla ya kuingia hta
bungeni. Sisi bado tupo imara....wacha hivi vivulana viondoke sisi
ambao tunajua nini tunakutaka bado tupo imara ndani ya chama" Msigwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni