Jumatatu, 18 Aprili 2016
Jumapili, 17 Aprili 2016
Jumamosi, 16 Aprili 2016
Magazeti ya Leo jumamosi ya tarehe 16/04/2016
Magazeti ya Leo yanaletwa kwenu Kwa hisani ya kikoti m Pesa ambao wanatoa huduma mbalimbali za kibiashara kama huduma ya mpesa , tigo pesa , wanauza vocha za mitandao yote ya simu pia wanauza vifaa vya shuleni na ofisini Kwa bei rahisi nyote mnakaribishwa
Pia kikoti company inakituo cha tuition kinachojulikana kama New Mwalimu Education Centre kinachofundisha masomo ya ziada kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita kwa masomo yote Muda ni kuanzia saa kumi mpaka saa moja jioni Eneo in majengo ya roman Catholic kigango cha madizini .Njoo upate elimu bora
Pia kikoti company inakituo cha tuition kinachojulikana kama New Mwalimu Education Centre kinachofundisha masomo ya ziada kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita kwa masomo yote Muda ni kuanzia saa kumi mpaka saa moja jioni Eneo in majengo ya roman Catholic kigango cha madizini .Njoo upate elimu bora
Ijumaa, 15 Aprili 2016
Tatizo la maji katika mji mdogo wa ilula laendelea kufanyiwa kazi na mbunge kilolo
Mto huo unaopita mjini Iringa ukijazwa na vyanzo mbalimbali vidogo vya maji vikiwemo vya wilayani Kilolo, upo zaidi ya kilomita 30 kutoka mji huo wa Ilula wenye kata tatu za Lugalo, Nyalumbu na Ilula yenyewe.
Mwamoto alitoa ombi hilo wakati Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Iringa Mjini (IRUWASA) ikikabidhi kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira ya Mji Mdogo Ilula, mradi mdogo wa maji yanayotumiwa na mji huo toka chanzo cha mto Idemle baada ya kusimamia ukarabati wake uliogharimu Sh Milioni 903.
“Ufumbuzi wa tatizo la maji katika mji mdogo wa Ilula ni kutumia maji ya Mto Ruaha Mdogo badala ya pendekezo la kutumia chanzo cha Mgombezi ambalo gharama zake ni kubwa,” Mwamoto alisema.
Alisema endapo serikali itaendelea na mpango wa kutumia chanzo cha Mgombezi wananchi wa Ilula wasitegemee kupata maji ndani ya kipindi kifupi kijacho.
“Kama tutang’ang’ania kutumia chanzo cha Mgombezi, inaweza kuichukua Ilula zaidi ya miaka 10 kupata huduma ya maji safi na salama, ombi langu tutumie chanzo cha mto Ruaha Mdogo kuleta maji Ilula, na nadhani hata gharama zake zinaweza kuwa ndogo,” alisema.
Akitoa taarifa ya ukarabati wa mradi wa maji wa chanzo cha mto Idemle, Mkurugenzi wa IRUWASA, Gilbert Kayange alisema; “baada ya ukarabati huo uliofanywa kati ya mwaka 2013 na 2015, chanzo hicho sasa kinazalisha mita za ujazo 940 kutoka mita za ujazo 600 zilizokuwa zikizalishwa awali wakati mahitaji kwa siku ni mita za ujazo 2,609.”
Ili kutatua tatizo la maji katika mji huo, Kayange alisema serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa chanzo cha Mgombezi ambao gharama yake inaelezwa kuwa ni zaidi ya Sh Bilioni 15.
“Tunaongelea suala la Mgombezi kwasababu mradi huo ulikwishasanifiwa, lakini hiyo haitufanyi wataalamu tusiendelee kutafuta vyanzo vingine mbadala vitakavyosaidia kukabiliana na changamoto ya maji katika mji wetu wa Ilula,” alisema.
Akizungumzia kazi zilizotekelezwa wakati wa ukarabati wa mradi huo wa chanzo cha Idemle, Kayange alizitaja baadhi yake kuwa ni pamoja na kukarabati kidaka maji katika mto Idemele, kukarabati tenki la kuhifadhi maji Mazombe na ujenzi wa vitolea hewa katika bomba kuu la usafirishaji na ukarabati wa njia ya usafirsiahaji maji wenye urefu wa kilomita 14.
Nyingine ni pamoja na ujenzi wa mabomba mapya ya kusambaza maji safi yenye urefu wa kilomita 16.7 ambayo hata hivyo yamekuwa yakihujumiwa kwa kutobolewa na watu wasiojulikana.
Mtendaji wa kijiji cha Mazombe, Joseph Nyoni alisema; “mambomba ya plastiki yamekuwa yakitobolewa nay ale ya chuma yamekuwa yakibondwa sehemu za maungio na kusababisha kuvuja na kupoteza maji mengi yanayotakiwa kwa matumizi ya wananchi.”
Nyoni alisema katika kukabiliana na changamoto hiyo, wamefanya mikutano ya hadhara ili kuwashirikisha wananchi kuwafichua waharibifu wa mitandao ya maji.
Mbunge wa Kilolo ameliomba jeshi la Polisi kuwasaidia kuwabaini watu hao ili wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa uharibifu huo.
Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Ilula, Enock Ngoinde amesema wanahitaji zaidi ya Sh Milioni moja kukarabati mabomba hayo.
TAKUKURU yakabidhiwa Kampuni ya Lugumi
picha :Mkurugenzi Mkuu Takukuru-Valentino Mlowola
Sakata
la kampuni ya Lugumi iliyoingia mkataba wa Sh37 bilioni na Jeshi la
Polisi wa kufunga mashine za kielektroniki za kuchukua alama za vidole
nchi nzima, sasa limetua Takukuru baada ya taasisi ya kupambana na
rushwa kuchukua faili lake la usajili.
Kampuni
hiyo ilibainika kutotimiza matakwa ya mkataba wake baada ya kufunga
mashine 14 tu kati ya 108 ilizotakiwa kufunga, licha ya kulipwa
asilimia 99 ya fedha kwa mujibu wa mkataba.
Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) ya mwaka 2013/14 ndiyo iliyofichua udhaifu huo.
Wakati
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikitaka nguvu itumike ili
Jeshi la Polisi liwasilishe mkataba huo, utata umeibuka katika umiliki
wa kampuni hiyo kutokana na kuwepo tuhuma kuwa baadhi ya vigogo wa
Polisi na wanasiasa ni wanahisa wa Lugumi Enterprises.
Jana,
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela),
Frank Kanyusi alisema kuwa Takukuru inashughulikia suala hilo, huku
akibainisha kuwa kwa sasa Brela hawana takwimu za kina za kampuni hiyo.
“Kampuni
hii ilisajiliwa kihalali na kupewa cheti cha usajili. Ila ninachoweza
kukueleza kwa sasa ni kwamba jalada la usajili la Lugumi lipo Takukuru
kwa ajili ya uchunguzi zaidi,” alisema Kinyusi jana.
Kanyusi,
ambaye hakutaka kuzungumzia kiundani kuhusu usajili wa kampuni hiyo,
alisema: “Waandishi wa habari wamekuwa wakiniuliza maswali mengi kuhusu
suala hili ila kwa sasa hali ndiyo hiyo. Jambo hili lipo Takukuru.”
Alisema
kwa sasa kampuni zilizosajiliwa na Brela zipo 120,000 na zinakaribia
kufika 130,000 na kwamba kampuni lazima zitoe taarifa zake kila mwaka,
kinyume na hapo zinaweza kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufutwa.
Habari
za uhakika kutoka ndani ya Brela zilieleza kuwa taarifa za usajili wa
kampuni hiyo zilitoweka takribani miezi miwili iliyopita.
Mwandishi
alipofika katika ofisi za wakala huyo kwa ajili ya kupata ukweli wa
usajili, alielezwa na mmoja wa watumishi ambaye hakutaka jina lake
kuwekwa wazi kwamba ni vigumu kupata hilo jalada kwa sababu ya mvutano
ulioibuka.
Hata
baada ya kufuata taratibu za kupewa jalada hilo kwa ajili ya kupitia
masuala mbalimbali, alijibiwa kuwa jalada hilo halionekani ingawa
baadaye Kanyusi alisema limechukuliwa na Takukuru.
Sakata
la Lugumi liliibuka wiki iliyopita wakati PAC ilipokutana na Jeshi la
Polisi kupitia taarifa ya hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na
CAG.
Katika
hesabu hizo ilibainika kuwa mwaka 2011, Polisi iliingia mkataba na
Lugumi kwa ajili ya kufunga mashine hizo katika vituo 108 vya polisi kwa
gharama ya Sh 37 bilioni.
Hata hivyo, ilibainika kuwa kampuni hiyo imefunga mitambo hiyo kwenye vituo 14 tu, huku ikilipwa asilimia 99 ya fedha hizo.
Kutokana
na ukakasi huo, PAC ambayo ilibaini viashiria vya ufisadi katika
mkataba huo, iliagiza watendaji wa Polisi kuwasilisha taarifa za mkataba
huo pamoja na vielelezo vyake ili kamati hiyo iweze kuupitia na
kujiridhisha.
Lakini
hadi sasa Jeshi la Polisi halijawasilisha mkataba huo, jambo ambalo
huenda likazua mjadala mkali katika mkutano wa Bunge unaoanza Jumanne
ijayo.
Anne kilango malecela atoa ya moyoni
Aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango Malecela, ameibukia kanisani na
kutoa ya moyoni, ikiwa siku tano baada ya Rais Dk. John Magufuli
kutengua uteuzi wake.
Kilango,
Jumatatu wiki hii uteuzi wake ulitenguliwa baada ya Machi 20, mwaka
huu, kudai kuwa mkoa wa Shinyanga hauna mtumishi hewa wa serikali hata
mmoja.
Hata
hivyo, Ikulu ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa katika taarifa za awali
kuna watumishi hewa 45, huku kazi ya uhakiki ikiendelea katika wilaya
za Ushetu na Shinyanga.
Rais
Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa wote, alipokuwa akiwaapisha kuwa
wafanya uchunguzi kuhusu uwapo wa watumishi hewa katika mikoa yao na
kutoa taarifa.
Kutokana
na kutoa taarifa hizo zisizo za kweli, Jumatatu wiki hii, Rais Magufuli
alitangaza kutengua uteuzi wake, akiwa amekaa kwenye nafasi hiyo kwa
siku 27. Kilango amekuwa mkuu wa mkoa wa 19 tangu kuanzishwa kwa mkoa
huo.
Mbali
na Kilango, Rais Magufuli pia alimsimamisha kazi Katibu Tawala wa Mkoa
wa Shinyanga, Abdul Dachi, kutokana na taarifa hizo za kutokuwapo
watumishi hewa katika mkoa.
Alivyosema Kanisani
Akiwasalimia
waumini wenzake juzi, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, mjini Shinyanga,
baada ya kupewa fursa ya kusema neno, Kilango alisema anamshukuru Mungu
kwa kila jambo kwa yote yaliyomtokea.
“Ndugu
waumini wenzangu, hili ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu. Hata mtu
unapojifungua mtoto akafariki dunia, unamshukuru Mungu kwani hayo ni
mapenzi ya Mungu.
"Ukiona mzazi wako kafariki dunia pia, unamshuruku Mungu. Tunao wajibu wa kumshukuru Mungu kwa kila jambo,” alisema kwa maneno mafupi na kisha kuketi, huku akiacha simanzi miongoni mwa waumini wenzake, wakiwamo viongozi wa kanisa.
Alivyoanza Kazi
Mbele
ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), muda mfupi baada ya
kuanza kazi, Kilango alisema Shinyanga ni mkoa wenye changamto nyingi
ambazo atazishughulikia, lakini atakuwa akilazimika kukimbia Dar es
Salaam kumwona mwenzi wake, Mzee John Malecela ambaye ni mgonjwa, na
pindi hali yake ikiimarika wataungana naye mjini Shinyanga.
Hayo aliyasema Machi 22, mbele ya wajumbe wa kikao cha kamati hiyo na Ijumaa Machi 25, alisali kanisani hapo.
Sambamba
na hayo, aliahidi kupambana na watumishi wazembe na wale wanaoendekeza
rushwa na ufisadi na kurejesha hadhi ya mkoa wa Shinyanga kimaendeleo.
Kilango
ambaye yuko mjini Shinyanga, akisubiri kukabidhi ofisi kwa mrithi wake
kwa mujibu wa utaratibu, bado anaishi hotelini kwa vile aliyekuwa Mkuu
wa Mkoa huo, Ally Rufunga, hajaondoka katika nyumba ya serikali iliyoko
Ikulu ndogo, eneo la Lubaga.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)