Jumatano, 27 Aprili 2016
Jumanne, 26 Aprili 2016
Iringa mkoa wetu sote: CHANGIA MADAWATI
serikali ya mkoani Iringa yadhamiria kumaliza kadhia ya upungufu wa madawati . Mkuu wa mkoa wa Iringa anawaomba wakazi wa Iringa waishio jijini Dar es salaam kujitokeza kwa wingi tarehe 04/05/2016 kuanzia saa 9:00 Alasiri kwenye ukumbi wa Ubungo external jijini humo kwa mkutadha wa kuchangia madawati.
Binafsi naomba Wanairinga na Watanzania kwa ujumla kujitokeza na kumuunga mkono mkuu huyu wa mkoa mwenye dhamilra ya dhati kabisa kumkomboa mwanafunzi wa kitanzania anayeketi chini ilihali anayaandaa maarifa ya kulitumikia taifa lake.
HONGERA SANA MAMA MASENZA
Tunaamini TUtashirikiana vema na wakazi wa iringa kuitambulisha iringa
CHANGIA MADAWATI, OKOA IRINGA NAKIZAZI CHA BAADAYE
Vyama vyakacha kuwasilisha hesabu NI CUF tu waliowasilisha
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Profesa Mussa Asaad alitaja Chama cha Wananchi (CUF) , ndicho kimewasilisha hesabu zake kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari mwaka 2015 hadi Juni mwaka huo.
Alisema vyama vingine 21 vimeshindwa kufanya hivyo hali ambayo amemshauri Msajili wa vyama hivyo kufuatilia jambo hilo. “Ripoti hii inabainisha kwamba vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ni 22, lakini hadi Juni mwaka 2015, vyama vilivyowasilisha hesabu zao kwa ukaguzi ni chama kimoja tu cha CUF, sasa hivi vingine vimekiuka sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992”, alisema Profesa Asaad.
Akizungumzia udhaifu mwingine ambao umebainika katika ripoti hiyo Profesa Asaad aliweka hadharani Balozi mbalimbali za Tanzania nje, Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA), Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).
Ripoti ya CAG yaanika majipu
Ripoti hiyo inaonesha kati ya halmashauri 164 zilizokaguliwa, 47 pekee ndizo zimepata hati safi, nyingine zilizobakia zina hati zenye mashaka, zisizoridhisha na chafu. Kwa upande wa mashirika ambayo ripoti hiyo imeyagusa, Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) limebainika mauzo ya hisa zake yalikuwa batili, hivyo CAG ameshauri lirudi chini ya usimamizi wa serikali hadi hapo mgogoro wa mgawanyo wa hisa utakapotatuliwa.
Kuhusu Wakala wa Usafiri wa Mwendo wa Haraka Dar es Salaam (DART), ripoti ya CAG imebaini kuwa kwa mwaka wa fedha 2014/15 wakala huyo aliingia mkataba na UDA-RT wa kutoa huduma ya usafiri wa mpito wa kuendesha mabasi 76 kulingana na vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba.
Lakini, Sheria ya Manunuzi ya Umma, mkataba huo ulitoa ongezeko la ununuzi wa mabasi na kufikia 84 ili kulingana na matakwa ya DART. Hata hivyo kwenye ukaguzi wa hesabu zao, CAG alibaini kuwepo na ununuzi wa mabasi 140 ambayo ni sawa na ongezeko la mabasi 56 yasiyo ndani ya mkataba.
Na kwamba pamoja na makosa hayo, pia ilibainika kuwa mabasi hayo yalikuwa na nembo ya UDART badala ya DART, kinyume na vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba na kuiagiza DART kuendesha UDA-RT kwa kuzingatia taratibu zilizoainishwa kwenye mkataba.
Aidha, ripoti hiyo imepigilia msumari kwenye suala la watumishi hewa na kusema tatizo hilo limekuwa sugu na serikali za mitaa zinaongoza kwa kulipa mishahara watumishi waliofariki na waliotoroka huku Sh bilioni 2.7 zikiwa zimetumika mwaka wa fedha 2014/15 kwa malipo hayo.
Jambo lingine ambalo limejitokeza kwenye ripoti ya CAG, ni utoaji wa misamaha ya kodi kwa kiwango cha juu huku ikionesha Sh trilioni 1.6 sawa na asilimia mbili ya pato la ndani la taifa, zilisamehewa katika kipindi kilichoishia Juni 30, 2015.
Madudu halmashauri
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa baada ya ripoti kuwasilishwa bungeni, CAG Mussa Assad alisema wamebaini kasoro nyingi katika taasisi mbalimbali za serikali, huku udhaifu mkubwa ukiwa kwenye serikali za mitaa.
Alisema kwa mwaka unaoishia Juni 30 ,2015, jumla ya hati za ukaguzi 465 zilitolewa kwa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na mashirika ya umma. Ripoti imeonesha kuwa mashirika ya umma na Serikali Kuu yamefanya vizuri kwa kupata hati nyingi safi, huku zile za mashaka zikiwa chache.
Aidha hakuna hati mbaya wala isiyoridhisha. Akifafanua alisema katika ukaguzi huo, halmashauri ndizo zinaongoza kwa kufanya vibaya . Kati ya halmashauri 164 zilizokaguliwa, 47 pekee ndizo zimepata hati safi, nyingine zilizobakia ni zenye mashaka, zisizoridhisha na chafu.
“Mashirika ya umma na Serikali Kuu yamefanya vizuri hakuna wenye hati isiyoridhisha au hati chafu, ila halmashauri bado kuna udhaifu mkubwa kutokana na kutokuwepo na mifumo madhubuti ya kutekeleza mapendekezo ya ukaguzi tunayoyatoa,” alisema Profesa Asaad.
Ripoti hiyo imeweka hadharani udhaifu wa Serikali za Mitaa katika kutekeleza mapendekezo ya CAG kutokana na kubainika kuwa asilimia 63 ya maagizo ya mkaguzi huyo kwa halmashauri nchini hayajatekelezwa.
Misamaha ya kodi
Wakati huo huo, akizungumzia misamaha ya kodi kwa kipindi kilichoishia Juni 30, 2015, Profesa Assad alisema ripoti yao inaonesha kuwa kiasi cha misamaha kilichotolewa ni Sh trilioni 1.6 sawa na asilimia mbili ya pato la ndani la taifa.
Kiwango hicho kwa mujibu wa Profesa Asaad, ni cha juu ikilinganishwa na lengo la serikali la kupunguza misamaha hiyo isizidi asilimia moja ya pato la taifa. Ripoti hiyo pia inabainisha uwepo wa bidhaa zilizohifadhiwa katika maghala kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi ambazo zilipewa misamaha ya kodi ya Sh bilioni 9.1 lakini hakuna ushahidi ulioonesha mauzo hayo kama kweli yalifanywa nje.
Katika misamaha hiyo, pia kuna utata kwenye mafuta yenye dhamana ya kodi ya Sh bilioni tano ambayo yalionekana kwenye mfumo wa forodha wa (TANCIS) kuwa yamesafirishwa nje kupitia nchini lakini hakuna ushahidi wa hilo.
“Sasa ukiangalia hayo na mengine utaona udhaifu mkubwa , tumeshauri serikali iweke mkazo usimamizi wa misamaha ya kodi na itolewe tu kwa mambo yanayostahili na uwepo ufuatiliaji kujua mrejesho wake, ili serikali ikusanye kodi na kujiimarisha kiuchumi”, alisema Profesa Asaad.
Deni la Taifa
Akizungumzia deni la taifa, Profesa Asaad alisema hadi kufikia Juni 30, mwaka 2015, deni la taifa lilikuwa Sh trilioni 33.54. Deni la ndani lilikuwa Sh trilioni 7.99 na deni la nje likiwa Sh trilioni 25.5 hivyo jumla ya deni lote likiongezeka kwa asilimia 27 ikilinganishwa na deni lililoishia Juni 30, mwaka 2014.
CAG ameshauri serikali kuongeza jitihada za ndani za kuhamasisha ukusanyaji wa mapato kujenga wigo mpana wa kulipa madeni na kuwa na mpango wa kupunguza gharama za kuongeza mikopo yenye masharti nafuu.
Zito kabwe anena tena
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemtaka Rais John Magufuli kukabiliana na vikundi vya mafisadi vinavyoiba mabilioni ya fedha za umma kupitia mikataba mibovu waliyoingia badala ya kuishia kutumbua majipu.
Akizungumza katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya chama chake jana, Zitto alisema ACT Wazalendo inaunga mkono
jitihada za Rais Magufuli katika kupambana na ufisadi, lakini bado
hajagusa kiini chenyewe.
Zitto alitolea mfano wa kashfa ya Akaunti
ya Tegeta Escrow kuwa bado kuna kampuni inayolipwa Sh8 bilioni kila
mwezi kwa ajili ya mitambo yake ya umeme.
Pia, alisema kashfa ya hati fungani imeongeza deni la Taifa kwa Sh1.2 trilioni.
“Bado
huo mtambo upo chini ya matapeli na kila mwezi Serikali inawalipa Sh8
bilioni wazalishe au wasizalishe umeme. Hivi ndivyo vikundi masilahi
katika sekta ya nishati. Bila kuvibomoa, Rais ataonekana anachagua watu
katika vita hii,” alisema Zitto.
Alisema: “Ni kweli kuna watu tayari wamefikishwa mahakamani kwa rushwa ya Dola 6 milioni za Marekani zinazohusu hati fungani.
"Serikali
imewafikisha mahakamani madalali wa rushwa lakini waliotoa rushwa hiyo
hawapo mahakamani. Waliopokea rushwa ambao ni maofisa wa Wizara ya Fedha
hawajashtakiwa.”
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, alisema vita ya ufisadi siyo ya kutumbua majipu tu, bali kujenga mfumo madhubuti wa kuzuia mianya ya rushwa.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, alisema vita ya ufisadi siyo ya kutumbua majipu tu, bali kujenga mfumo madhubuti wa kuzuia mianya ya rushwa.
Alisema Rais Magufuli anapaswa kuwaongoza Watanzania katika vita ya kukataa mikopo kama hiyo ambayo inawasababishia umaskini.
Aungana
na hoja za upinzani
Zitto alisema chama chake kinaungana na vyama vingine vya upinzani kwa hoja walizozitoa baada ya kutoka bungeni za kutokuonyeshwa moja kwa moja kwa matangazo ya televisheni kutoka bungeni, matumizi ya Serikali nje ya mpango wa bajeti na Serikali kutokuwa na mwongozo kwa mawaziri wake.
Zitto alisema chama chake kinaungana na vyama vingine vya upinzani kwa hoja walizozitoa baada ya kutoka bungeni za kutokuonyeshwa moja kwa moja kwa matangazo ya televisheni kutoka bungeni, matumizi ya Serikali nje ya mpango wa bajeti na Serikali kutokuwa na mwongozo kwa mawaziri wake.
Akizungumzia kusitishwa kwa
urushaji wa matangazo ya Bunge, Zitto alisema hatua hiyo inatakiwa
kupigwa vita kwa sababu inajenga udikteta katika nchi na kuwanyima
wananchi haki ya kupata habari za Bunge.
“Ina maana TV zinapaswa
kumuonyesha mtu mmoja tu akihutubia bungeni ambaye ni Rais tu... hapana
hii siyo sawa,” alisema Zitto.
Akizungumzia suala la bajeti, Zitto alisema hakuna sheria yoyote inayompa mamlaka Rais kuhamisha fedha kwenda kufanya shughuli nyingine. Lakini alisema tangu Rais Magufuli achaguliwe, amekuwa akihamisha fedha wakati Bunge lilishapitisha bajeti.
Akizungumzia suala la bajeti, Zitto alisema hakuna sheria yoyote inayompa mamlaka Rais kuhamisha fedha kwenda kufanya shughuli nyingine. Lakini alisema tangu Rais Magufuli achaguliwe, amekuwa akihamisha fedha wakati Bunge lilishapitisha bajeti.
“Rais Magufuli kwani amekuwa waziri wa fedha,
waziri wa ujenzi na Rais kwa wakati mmoja? Tunamtaka asiingilie
majukumu ya mihimili mingine, wananchi tumnyooshee kidole na kumwambia
afuate utaratibu,” alisema Zitto.
Mbunge huyo pekee wa chama hicho,
alisema tangu walipoapishwa, mawaziri hawajapewa mwongozo wa kazi na
kutoa wito kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoa miongozo kwa mawaziri.
“Mpaka sasa nchi haina mawaziri kwa sababu hawajapewa miongozo. Kwa
hiyo, Baraza la Mawaziri lina mawaziri wawili tu ambao ni Rais na
makamu wake,” alisema Zitto na kulitaka Bunge kutengeneza mfumo wa
kuisukuma Serikali kutekeleza mambo muhimu kwa Taifa.
Kuhusu hali ya
uchumi, Zitto alisema bajeti ya mwaka huu imeongezeka mpaka kufikia
Sh29 trilioni lakini ana wasiwasi itakwama kwa sababu theluthi moja ya
mapato ya ndani yanatoka bandarini ambako ripoti zinaonyesha kuwa
yamepungua.
Alisema Serikali imepanga kukopa Sh7 trilioni kwa ajili
ya utekelezaji wa bajeti na kwamba hatua hiyo inazidi kuongeza deni la
Taifa ambalo limelalamikiwa pia na Mkaguzi na Mdhibiti wa Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG) katika ripoti yake.
Rais Magufuli Amteua Thobias Andengenye Kuwa Kamishna Mkuu Wa Jeshi La Zimamoto Nchini
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua
Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye kuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la
Zimamoto nchini.
Taarifa
iliyotolewa leo tarehe 25 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Kamishna Andengenye umeanzia leo
tarehe 25 Aprili, 2016.
Kamishna wa Polisi Andengenye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Pius Makuru Nyambacha ambaye amestaafu.
Kabla
ya uteuzi huo Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye alikuwa Kamishna wa
Utawala na Utumishi, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Wakati
huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Donan Mmbando kuwa
Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Dodoma.
Uteuzi wa Dkt. Donan Mmbando umeanza tarehe 24 Aprili, 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam-25 Aprili, 2016
Siwema wa Nay wa Mitego Afungwa Miaka Miwili Gerezani kwa Kutishia Kusambaza Picha za Uchi za Mpenzi Wake
Wiki iliyopita zilianza kusikika taarifa mbalimbali kuhusu kuhukumiwa kwa mpenzi wa zamani na mama mtoto wa msanii Nay wa Mitego aliyehukumiwa kwenda jela miaka miwili jijini Mwanza.
Pamoja na taarifa zote hizo kutoka hakukuwa na taarifa za kina kueleza ni nini hasa kilitokea mahakamani mpaka akahukumiwa jela miaka miwili ila taarifa za awali zilidai kwamba amehukumiwa kwa sababu ya kutukana mtu mtandaoni.
Wakili
wa serikali Moris Mtoi ameongea kwenye exclusive interview na DStv na
kusema ukweli au chanzo cha Siwema kuhukumiwa hakikua kumtukana mtu
mitandaoni bali kumtishia mtu.
Amesema kilichompeleka Siwema jela ni kumtishia mpenzi wake wa zamani kutoa picha za uchi walizopiga,
Siwema alikua akimtishia kwamba asingetoa pesa na kumnunulia gari au
kufata maagizo yake angezisambaza picha hizo kwa mke wake na watu
wengine.
Wakili
huyu wa serikali na mwendesha mashtaka kwenye kesi hii amesema vitu
vingine alivyokuwa akivitaka Siwema ni kununuliwa nyumba na boyfriend
wake huyu wa zamani.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)