ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumatatu, 9 Mei 2016

Magazeti ya Leo jumatatu ya tarehe 09/05/2016.

Magazeti yamebeba habari za kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni













katika nyanja za kitaifa, kimataifa na michezo

Jumamosi, 7 Mei 2016

Magufuli kutaifisha sukari iliyofichwa

Imeandikwa na Waandishi Wetu SAKATA la ufichaji sukari lililoanzishwa na wafanyabiashara wasio waaminifu nchini, limechukua sura mpya baada ya Rais John Magufuli kutaja baadhi ya maeneo sukari hiyo ilikofichwa na kuagiza ikamatwe, itaifishwe na kugawiwa bure kwa wananchi.
Kwa sasa sukari imeshaanza kuadimika, ambapo katika maduka ambayo ilikuwa kawaida kukuta bidhaa hiyo katika makazi ya wananchi, haipatikani kabisa na inakopatikana, bei yake iko juu maradufu zaidi ya bei elekezi ya Sh 1,800 kwa kilo.
Takwimu za bei zimekuwa zikibadilikabadilika katika maeneo ya Dar es Salaam ambako wiki hii ilishafikia Sh 2,500 huku mikoani ikiongezeka na kuzidi Sh 3,000.
Walioficha Dar, Moro
Akizungumza jana na wananchi katika mji wa Katesh wilayani Hanang mkoani Manyara akiwa njiani kwenda mkoani Arusha, Rais Magufuli alisema taarifa alizokuwa nazo mpaka jana kuna baadhi ya wafanyabiashara wameficha sukari tani 7,000.
“Kuna mmoja alienda kununua sukari Kilombero (mkoani Morogoro) zaidi ya tani 3,000 na kuiacha iko pale pale na mwingine ana godown (ghala) Mbagala (jijini Dar es Salaam), akiwa na tani 4,000 na hataki kuitoa ili wananchi wakose sukari, lakini nataka kuwaambia sukari huwezi kuficha kama sindano,” alisema huku akitoa mifano.
“Tutachukua sukari ile na kugawa bure na hawatafanya biashara maishani hapa nchini Tanzania, hivyo kama wapo wafanyabiashara wanaonisikia ambao wanataka kucheza na Serikali hii wanacheza na maisha yao,” alionya Rais Magufuli, ambaye uongozi wake umejivunia sifa ya kuchukua maamuzi ya kijasiri.
Kiwango hicho cha sukari iliyofichwa katika maghala mawili tu ya Morogoro na Dar es Salaam, kinatosheleza kulisha nchi nzima kwa wiki moja, kwa kuwa mahitaji ya siku ya sukari nchini ni tani 1,150 sawa na tani 420,000 kwa mwaka.
Salama la ambao hawajagundulika kwa mujibu wa Rais Magufuli, ni kutoa sukari waliyoficha kwa wananchi na kuiuza kadri walivyokuwa wamepanga. Kwa watakaokaidi, Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola kufuatilia wafanyabiasha wote walioficha sukari, kwani ni wahujumu uchumi na sukari waliyoficha itachukuliwa na kugawiwa bure.
Sababu ya kudhibiti
Akielezea sababu za kuzuia uagizaji wa sukari nje ya nchi, Rais Magufuli alisema wakulima nchini wanalima miwa, lakini haitengenezi sukari kwa kuwa kuna sukari ya magendo inayoingizwa kutoka nje ya nchi.
Mbali na kuwa ya magendo, Rais Magufuli alisema wafanyabiashara hao wanaoingiza sukari ya magendo, wana tabia ya ajabu kwenda nchini Brazil na maeneo mengine kunakouzwa sukari inayokaribia kuisha muda wake wa matumizi na kutaka kutupwa na kuinunua wao.
Alisema sukari hiyo ambayo katika nchi husika hutakiwa kumwagwa baharini, wafanyabiashara wenye tamaa ya fedha wa hapa nchini, huichukua na kuweka kwenye magunia tofauti na kuileta ndiyo maana wananchi wanapata magonjwa ya kila aina ambayo haijulikani yametoka wapi.
“Tunataka kudhibiti biashara hii ya sukari kwani tatizo ni dogo niwaambie ni la muda, kwani Serikali ya Magufuli haiwezi kushindwa kununua sukari hata kama ni mabehewa elfu ngapi,” alisema. Alisema ameshamuagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na sukari ya kutosha italetwa na watu watapata bei ya sukari iliyo nafuu.
*Uagizaji kukomeshwa
Pamoja na uhaba uliopo ambao kwa sehemu kubwa umetengenezwa na wafanyabiashara hao baada ya kuzuiwa kuagiza sukari kutoka nje, tayari Serikali imeshachukua hatua za uzalishaji zaidi, zitakazokomesha kabisa biashara ya uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.
Wiki iliyopita wakati Waziri Mkuu Majaliwa akijibu maswali ya papo kwa hapo bungeni kuhusu pia bei ya sukari, alisema Tanzania ina uwezo wa kuzalisha tani 300,000 za sukari kwa mwaka wakati mahitaji ya bidhaa hiyo kwa mwaka ni tani 420,000 na hivyo upungufu kuwa tani 120,000 kila mwaka.
Jana Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, alielezea hatua hizo za kukomesha uagizaji wa sukari, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilango (CCM), aliyetaka kufahamu lini Mkoa wa Kigoma wenye rasilimali nyingi kutajengwa viwanda.
Kwa mujibu wa Mwijage, kiwanda kipya cha sukari kinatarajiwa kujengwa katika mkoa huo na tayari Serikali imeshampa mwekezaji wa kiwanda hicho, hekta za ardhi 47,000 kwa ajili ya mradi huo.
Mwijage alisema kiwanda hicho kitakapoanza uzalishaji, kitazalisha tani 120,000 za sukari kwa mwaka, ambazo ndizo zinazopungua katika uzalishaji wa sasa.

Shule binafsi wasema ada elekezi yatishia elimu

Imeandikwa na Sifa Lubasi, Dodoma SHIRIKISHO la wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya kiserikali Tanzania (TAMONGSCO) limesema ipo haja kwa serikali kutangaza ada elekezi mapema ili kuondoa utata uliopo unaotishia kukwamisha maendeleo ya elimu.
Shirikisho hilo limesema kwamba mambo mengi ya maendeleo katika shule hizo yamekwama kutokana na kusubiri ada elekezi.
Akizungumza kumkaribisha Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, katika mkutano wa shirikisho hilo mjini hapa, Mwenyekiti wa Shirikisho Mrinde Mzava, alisema walifurahishwa na kufika kwake Waziri, kwani waliamini kupata maelekezo ya ada elekezi ili kumaliza shida zilizopo sasa za uendeshaji.
Alisema mwenyekiti huyo kwamba kuna hatari katika elimu kama hali ya ucheleweshaji wa uchambuzi wa gharama za ada elekezi itaendelea.
Alisema pamoja na serikali kukiri kuwa suala hilo lipo mezani kwa ajili ya mazungumzo, hivi sasa shule na vyuo binafsi vimejikuta vikiweka viwango visivyotakiwa kisheria ambapo kwa upande wao kuna madhara makubwa.
Mwenyekiti huyo alisema kutokana na suala la ada elekezi kuwa kwenye mazungumzo wanaiomba serikali iliangalie kwa haraka ili lipunguze mzigo wa gharama za uendeshaji na ukubwa wa ada kwa lengo la kufanikisha utoaji wa elimu bora.
Katika mkutano huo serikali imeelezea kusikitishwa kwake na baadhi ya shule na vyuo kugeuza elimu kama sehemu ya kufanyia biashara. Aidha imesema kuwa bado haijapitisha ada elekezi kwa wamiliki wa shule na vyuo vya watu binafsi kutokana na jambo hilo kuwa kwenye meza ya mazungumzo kati serikali na wamiliki hao.
Kauli hiyo ambayo imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof Joyce Ndalichako, wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa shirikisho la wamiliki na mameneja wa shule na vyuo visivyo vya kiserikali Tanzania (TAMOMGSCO) mjini Dodoma.
Alisema baadhi ya shule na vyuo hivyo binafsi hivi sasa wakati majadiliano kuhusu ada elekezi yanaendelea, wamiliki wake wameweka maslahi zaidi ya kibiashara na kuwaumiza wananchi na wizara kamwe haitavumilia.
Alisema Wizara yake inasisitiza wamiliki kufuata miongozo ya serikali, na wale ambao hatawafuata haitawavumilia. Waziri Ndalichako alilazimika kutoa ufafanuzi huo kutokana na shirikisho hilo kutaka kufahamu kuhusu ada elekezi na kutaka kupatiwa maelekezo kutoka serikalini juu ya shule na vyuo binafsi.

DC akabidhiwa ushahidi wa kupigwa mwalimu

CHAMA cha Walimu (CWT) Rukwa, kimemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mathew Sedoyeka ushahidi wa maandishi unaoelezea kitendo cha Ofisa Elimu, Shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Peter Fusi, kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao akiwa darasani.
Ushahidi huo ulikabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Rukwa, Hance Mwasajone.
Ushahidi huo wa kimaandishi wa tukio hilo umeandikwa na mwalimu mwenyewe, Jacob Msengezi (25) ambaye alisema alipigwa mbele ya wanafunzi wake akiwa darasani shule ya msingi Kianda kabla ya kuamuru walimu wengine kufanya usafi kwa kuokota mbigili ‘miba’ iliyotapakaa katika eneo la shule hiyo akidai kuwa huo ni uchafu.
Sedoyeka aliwaruhusu viongozi hao kumtembelea mwalimu na kusisitiza kuwa anafuatilia kwa karibu mkasa huo ili sheria ichukue mkondo wake .

Magazeti ya Leo jumamosi ya tarehe 07/05/2016

Headline hizi za magazeti ya Leo zimeletwa Kwa hisani kubwa ya Airtel jipime kifurushi cha yatosha na kampuni ya uuzaji na utengenezaji wa simu za mokononi za techno Kwa bei poa.












Ijumaa, 6 Mei 2016

Snura aomba radhi

Imeandikwa na Rahel Pallangyo
MSANII Snura Mushi, ameomba radhi kwa umma wa Watanzania kutokana na kosa la kutengeneza, kuzindua na kuweka mtandaoni video ya udhalilishaji wa mwanamke na isiyozingatia maadili ya kitanzania ya muziki unaoitwa Chura.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Snura aliyekuwa amefuatana na Meneja wake, Hemed Kavu `HK’ aliomba radhi vyombo vya serikali vinavyosimamia sekta ya sanaa kwa kutofuata sheria, kanuni na taratibu katika uendeshaji wa sanaa nchini.
“Mimi na Meneja wangu tunaahidi kutorudia tena kufanya tukio hilo la udhalilishaji na iwapo tutarudia basi tupewe adhabu kali kwa mujibu wa sheria za nchi,” alisema Snura.
Pia aliahidi kuwa mfano na balozi kwa wasanii wenzake na jamii katika kutunza na kufuata maadili na utamaduni wa kitanzania pamoja na sheria za nchi.
Wakati akijibu maswali ya wandishi wa habari juu ya sababu za kutengeneza video hiyo, alijitetea kwa kusema; “Kwa upeo wetu wa kufikiri tuliona tumpeleke chura maeneo yake ambayo ni kwenye maji na walivaa mitandio na miziki mingi watu wanacheza na mitandio. “Tulipoona mitandio imelowa tukaona tuweke yotube kwani huko mtu akiingia atakuwa ametaka mwenyewe na sidhani kama mtoto hawezi kuacha kwenda maktaba na kuingia yotube”, alisema Snura huku meneja wake akijitetea kuwa walirekodi wakati mvua inanyesha.
Snura aliahidi kutekeleza maazimio na maelekezo yaliyotolewa katika kikao cha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA) na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kuhusu video hiyo.
Tayari ameshajisajili BASATA kama sharti la kuruhusiwa kufanya maonesho, ameiondoa kwenye mtandao video ya Chura hivyo ataifanya upya video ya muziki wa chura.