Jaji
Mkuu wa Tanzania, Mohammed Chande Othman (katikati), akipewa maelezo na
Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta (kulia) wakati alipotembelea
banda la mahakama hiyo kwenye Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya
Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya maonesho hayo, Barabara
ya Kilwa, Dar es Salaam, jana. Alifuatana na Jaji Kiongozi, Ferdinand
Wambali (kushoto), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage (wa pili kulia) na viongozi wengine. (Picha na Yusuf Badi).
Jumanne, 5 Julai 2016
Jumatatu, 4 Julai 2016
Chadema: Maandalizi ya Kuuzuia Mkutano wa CCM Yameanza
KATIKA
kutekeleza tamko la Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) la kufika
Dodoma kusaidiana na Jeshi la Polisi kuzuia Mkutano Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Bavicha Dodoma wameanza maandalizi ya kupokea vijana
zaidi ya 2000.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Dodoma jana Malambaya Manyanya, Mwenyekiti
wa Bavicha Mkoa wa Dodoma alisema, kwa sasa viongozi wa mkoa wameanza
maadalizi ya kuwapokea wageni wao ambao wanatarajiwa kuanza kuwasili
tarehe 21 na 22 Julai mwaka huu.
Alisema,
maadalizi hayo ni ya kuwapokea vijana ambao watatoka katika mikoa yote
ya Tanzania kwa lengo la kutimiza tamko la Bavicha taifa la kushirikiana
na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuzuia mikutano na vikao vya CCM.
Alisema,
kwa sasa mkoa tayari umeunda kikosi cha kufanya kazi ya maadalizi ya
ugeni huo ambapo kwa nia njema utafika mjini Dodoma kutekeleza kauli ya
Rais John Magufuli ya kuzuia vikao vyote na mikutano ya vyama vya siasa.
Alisema,
maadalizi hayo ya kuwapokea vijana hao ni pamoja na viongozi wa kitaifa
wa Bavicha kwa maana ya kutafuta mahali pa kulala na maandalizi ya
chakula.
“Wapo
watu ambao wanadhani Bavicha wana mpango wa kufanya fujo, sisi tunataka
kurejesha Demokrasia nchini na kutekeleza kauli ya mkuu wa nchi.
“Tumekuwa
tukiona jinsi mikutano ya Chadema inavyozuiliwa, na sasa msimamo wa
Bavicha ni kuzuia mkutano ya CCM unaotarajiwa kufanyika Julai 23 kwa
lengo la kubadilishana uongozi kati ya mwenyekiti wa sasa wa CCM na rais
msitaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete na Rais John Magufuli.
“Tumeandaa
vijana takribani 2000 kutoka mikoa yote nchini watakaokuja Dodoma
kusaidiana na Jeshi la Polisi kutawanya mkutano usio halali wa CCM.
“Kwa
sababau mkuu wa nchi ametoa tamko la kuzuia mikutano yote ya siasa
ikiwa ni pamoja na vikao vya ndani na mikutano ya hadhara hadi 2020.” Alisema Malambaya.
Alisema,
Jeshi la Polisi lilizuia mikutano ya vyama vya siasa vya upinzani na
mahafali ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Chadema (CHASO) na kuwa,
sasa wanashirikiana na polisi kuhakikisha mikutano ya CCM haitafanyika.
UVCCM yanena kuhusu BAVICHA kuzua mkutano Dodoma
Umoja
wa Vijana CCM (UVCCM) umeingia katika mvutano mkubwa na Baraza la
Vijana wa Chadema (BAVICHA) kuhusu Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho
tawala uliopangwa kufanyika Julai 23 mwaka huu mjini Dodoma.
UVCCM
wameionya BAVICHA kuhusu mpango wao wa kutaka kukusanyika mjini Dodoma
siku hiyo kwa lengo la kuzuia mkutano huo kwa madai kuwa unakiuka amri
halali ya polisi ya kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano yote ya
kisiasa nchini.
Onyo
hiyo limetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamda Shaka
ambaye aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa
watawakabili kwa nguvu zote BAVICHA endapo wataamua kuendesha siasa
zinazolenga kuvuruga amani na kuleta hofu katika jamii na kutishia
maisha.
Alisema umoja huo hautaona shaka kutumia mbinu zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau miongo kadhaa iliyopita nchini Kenya.
“Hatutaona
muhali kupita njia zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau wa Kenya ili
kukihami chama, kulinda viongozi wake na kupigania hadhi na heshima
yetu,” alisema Kaimu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM.
CCM
inatarajia kufanya mkutano mkuu maalum Julai 23 mwaka huu ambapo Rais
John Magufuli atakabidhiwa rasmi uenyekiti wa chama hicho kutoka kwa
mtangulizi wake, Dk. Jakaya Kikwete.
Shelukindo Kuzikwa Alhamis Jijini Arusha
MWILI wa Mbunge wa zamani wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), unatarajiwa kuzikwa Alhamis wiki hii.
Taarifa
iliyotolewa jana na kaka wa marehemu, Enock Madimilo, ilisema taratibu
za mazishi zinaendelea kufanywa nyumbani kwa marehemu Dar as Salaam na
Arusha.
“Tunaendelea na mipango ya mazishi hapa Arusha na nyumbani kwa marehemu, Ada Estate jijini Dar es Salaam.
“Mazishi
yatafanyika hapa Arusha Alhamisi wii hii. Kwa hiyo, tunawaomba ndugu,
jamaa na marafiki wa marehemu, waje kumuaga mpendwa na kiongozi wao,” alisema Madimilo.
Shelukindo
alifariki juzi usiku saa 2:30 akiwa nyumbani kwa mama yake mzazi,
katika eneo la Olorien, jijini Arusha baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mwili
wa marehemu Beatrice uliondolewa nyumbani kwa mama yake huyo alipokuwa
akiuguzwa usiku huo huo na kupelekwa Hospitali ya Mount Meru.
Kutokana na msiba huo, tayari waombolezaji mbalimbali wameendelea kufika nyumbani kwa mama wa marehemu kwa ajili ya kutoa pole.
Kesi za mafisadi kutozidi miezi 9
Aidha, wameandaa kozi maalumu kwa majaji 14 watakaofanya kazi katika mahakama hiyo itakayoanza Julai 11 hadi 15, mwaka huu, kwenye Chuo cha Mahakama Lushoto mkoani Tanga, ili kupeana mwongozo juu ya uendeshaji wa mahakama hiyo.
Jaji Mkuu alisema, kesi zitakazoendeshwa katika mahakama hiyo ni zile ambazo upelelezi wake umekamilika ili uamuzi utolewe mapema. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kupambana na uhalifu huo.
Aliyasema hayo jana wakati alipotembelea Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo katika Barabara ya Kilwa, ambayo alisema yamezidi kuwa bora kuliko miaka mingine. Alisema baada ya sheria hiyo ya uhujumu uchumi kupitishwa na Bunge, imekuwa na marekebisho mengi na kuboreshwa kwa kiasi kikubwa.
Jaji Mkuu alisema pia, hatua inayofuata ni Rais kutoa idhini ya sheria hiyo na baadaye kupitishwa kwa kutangazwa katika Gazeti la Serikali ili ianze kutumika.
Alieleza kuwa baada ya kutangazwa katika Gazeti hilo la Serikali, Jaji anatakiwa kutunga kanuni mbalimbali, mojawapo ikiwa ya kulinda mashahidi kutokana na kuwa sheria hiyo inahusu makosa makubwa na hatari ya ugaidi, rushwa na uhujumu uchumi.
“Tuko mbioni kutunga kanuni hizo na kuhakikisha mashahidi wanalindwa. Jengo la mahakama hii litakuwa katika Chuo cha Sheria karibu na Mlimani City na tayari tumepeleka wasajili watendaji,” alisema.
Mwishoni mwa wiki, Jaji Mkuu huyo alisema kuwa majengo ya mahakama hiyo yatakabidhiwa leo. Kutokana na maelezo yake, Mahakama iko tayari kuendesha divisheni hiyo, baada ya kukabidhiwa majengo hayo.
Alisema wataanza kutoa semina kwa majaji na watumishi wengine wa mahakama hiyo juu ya namna divisheni hiyo itakavyoendesha shughuli zake. Aidha, aliweka wazi kuwa hadi sasa hakuna kesi hata moja iliyokwishatambuliwa kwamba itashughulikiwa na mahakama hiyo.
Jumapili, 3 Julai 2016
Michezo:Kikoti Education Centre Cup
Ilula mtua 2 na Ilula Madizini 2
Ilula sokoni 1 na Ilula isele 2
Kwa matokeo hayo timu ya ilula isele inaongoza katika ligi hiyo ikiwa na jumla ya point tatu na magoli mawili ikifuatiwa na ilula Madizini na ilula mtua zote zikiwa na point Moja na magori mawili na nafasi ya mwisho ikishikiliwa na ilula sokoni ambayo haina point
Mdhamini wa mashindano hayo amepongeza wachezaji wote Kwa kuonesha kiwango cha hali ya Juu na kuwaasa kuendelea na mashindano hayo Kwa nidhamu na utulivu mkubwa ili kufanisha zoezi hill
Ratiba za mechi zijazo ni kama zifuatazo
Isele vs Madizini saa name siku ya jumamosi ijayo
Sokoni vs Mtua saa kumi ya jumamosi ijayo
Na siku ya jumapili ijayo
Madizini vs Sokoni saa Nane
Mtua vs Isele saa kumi Jioni
Wapenzi watazamaji mnakaribishwa sana kuangalia vijana wenu wanavoonesha vipaji
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)













































Kikoti education centre cup imeendelea tena Leo Kwa michezo miwili ambapo timu ya zimepata matokeo yafuatayo;