ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Alhamisi, 2 Machi 2017

Rais Magufuli Amteua Mama Salma Kikwete Kuwa Mbunge

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 01 Machi, 2017 amemteua Mhe. Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Salma Kikwete ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mhe. Salma Kikwete ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zitakazotangazwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Magazeti ya Leo Alhamisi ya tarehe 02/03/2017




















Jumanne, 28 Februari 2017

Mbunge Awaomba Wananchi Wampige Mawe asipotekeleza ahadi

Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu, ametoa ruhusa kwa wakazi wa jimbo lake kumwadhibu kwa kumpiga mawe iwapo atashindwa kutekeleza ahadi alizoahidi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Majimarefu aliyasema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara na wananchi wa Vijiji vya Kwemshai, Ngulu na Mlungui, katika ziara yake jimboni mwake.

Alisema licha ya kuwa nje ya nchi kwa matibabu, lakini baada ya afya yake kuimarika amerejea nchini akiwa tayari kutatua kero za umma.

Aidha, amewaomba wapigakura wake kuendelea kushirikiana naye huku wakimpatia muda kumwezesha kuwatatulia kero hizo.
 
“Nawashukuru kwa kuniombea pale nilipokuwa nikiugua, nilikuwa nje ya nchi kwa matibabu sala zenu zimeniwezesha kuungana nanyi leo," alisema.

Aliwaeleza wananchi wa Kijiji cha Mlungi kuwa tatizo la maji na umeme viko mbioni kutatuliwa ndani ya mwaka huu na kwamba wale wanaoeneza maneno kuwa hakutafanyika kitu wanajidanganya kwa vile mambo yanakwenda sawa.

Majimarefu alisema katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo, ameamua kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhandisi Robert Gabriel kusimamia Mfuko wa Jimbo kusaidia miradi.

Katika hatua nyingine, Majimarefu aliwashukia mahasimu wake wa kisiasa aliodai wanatumia mbinu chafu kumchafua kuhusu afya yake tangu alipougua na kwenda kutibiwa nje.

“Kuna mahasimu wangu wa kisiasa wanapita kila kijiji kuzungumzia afya yangu kwamba nimepoteza fahamu na kukatwa mguu, siyo kweli myapuuze,”alisema.

Majimarefu alisema wananchi wapuuze uzushi huo usiokuwa na msingi kwani una lengo la kuwavunja moyo kwa manufaa yao ya kisiasa.

Hata hivyo, alisema kuwa hatavunjika moyo kwa maneno hayo na badala yake yamekuwa changamoto kwake kutekeleza ahadi zake na hafanyi hayo kwa lengo la kujipatia umaarufu kama inavyodaiwa na baadhi ya watu ila ni moja ya utekelezaji wajibu wake kwa wananchi waliomchagua.

Majimarefu aliwaeleza wananchi hao kuwa wakati wa watu kufanya fitna umekwisha na uliobaki ni ule wa kusema ukweli akiwahimiza kufanya kazi sambamba na kulinda rasilimali misitu.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Gabriel, alisema kwamba kazi yake ni kusimamia rasilimali za umma, hivyo atahakikisha kwamba yale yote yanayoanzishwa na mbunge huyo anayalinda.

Gwajima aelezea sakata zima la Makonda kutumia vyeti vya mtu mwingine

 

Siku kadhaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kusema kuwa hawezi kujibu madai ya mitandao ya kijamii kuwa alitumia vyeti vya mtu cha kidato cha nne, Askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ameibuka na kusema kuwa ni kweli alitumia vyeti hivyo


Askofu Gwajima amesema kuwa anamfahamu sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwa jina lake halisi ni Daudi Bashite na kwamba hilo la Paul Makonda ni la mwenye vyeti hivyo.

Aidha, Askofu Gwajima amedai kuwa anavyovyeti vya Daudi Bashite vinavyoonyesha kuwa hakufaulu na kwamba atashangaa kama Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako atalifumbia macho jambo hili. 
Pia ametishia kuwa, kama mamlaka husika hazitachukua hatua haraka basi yeye atatoka hadharani na vyeti hivyo.

Hapa chini ni sauti ya Askofu Gwajima akihubiri kanisani kwake.