ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Jumamosi, 6 Mei 2017

Katibu mkuu wa CCM yupo Mapumunziko

 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kimempa mapumziko ya muda ambao hakijautaja Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana.

Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, kiongozi huyo ameruhusiwa kupumzika ili kuangalia afya yake hadi hapo itakapoimarika.

Polepole alitoa kauli hiyo jana, alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara yake iliyolenga kukagua uhai wa CCM mkoani Arusha, ikiwa ni eneo linalotajwa kuwa ngome ya chama kikuu cha upinzani, Chadema.

Kauli hiyo ya Polepole imekuja ikiwa ni muda sasa Kinana hajaonekana hadharani, hatua ambayo imezusha maneno mengi, huku baadhi wakienda mbali na kuhusisha kitendo hicho na mgomo kutokana na uamuzi wa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli kumvua uwaziri wa Habari, Vijana Sanaa na Michezo ‘kijana wake’, Nape Nnauye.

Kuwapo kwa hisia za namna hiyo kunatokana na kile ambacho CCM ilidai kuwa ni uvumi, kwamba Kinana alitaka kuitisha mkutano na wanahabari siku moja baada ya Nape kuondolewa kwenye wadhifa huo na saa chache baadaye wakati akielekea kuzungumza na vyombo vya habari kutishiwa kwa bastola na mtu ambaye haijajulikana anafanya kazi wapi.

Ni wakati huo Rais Magufuli alilazimika kuzungumzia mahali alipo Kinana, akisema alikuwa amemtuma kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu.

Rais Magufuli alitoa ufafanuzi huo wakati akiwaapisha Mawaziri Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na Dk. Harrison Mwakyembe aliyechukua nafasi ya Nape.


 Hadi sasa hakuna picha yoyote inayomwonyesha kiongozi au mtu yeyote amefika nyumbani kwa Kinana kwa ajili ya kumjulia hali, jambo ambalo limezidi kuzua maswali.

 “Hili swali la Katibu wetu Mkuu ndugu Komrade Abdulrahmani Kinana limesemwa sana na mimi ninafurahi kwamba tunaanza kurejesha utamaduni ambao maisha ya viongozi wetu yanakuwa sehemu na maslahi ya umma wa Watanzania,” alisema Polepole na kuongeza:

“Lakini unapoona Katibu wetu Mkuu wa CCM anaulizwaulizwa yuko wapi na hata watu wasiokuwa wana CCM, hii inaonyesha kiwango cha imani cha Watanzania kinarejea kwa kasi kubwa, hasa katika kipindi hiki tunapofanya mageuzi makubwa ndani ya chama chetu.

“Na kwa hakika najua viongozi wa vyama vingine wasioonekana hawauliziwi na mtu yeyote, kwetu sisi ni dalili njema sana. Nipende tu kuwaambia jana nimeongea na Komrade Kinana bado yuko kwenye mapumziko ya kujitizama afya yake.

“Ninyi wote ni mashahidi mzee wetu huyu alifanya kazi kubwa ndani ya CCM na kwenye Serikali na pia kwenye wigo wa kimataifa, hasa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

“Lakini amefanya kazi kubwa zaidi kwenye chama ya kukijenga na kukiimarisha, hasa kwenye uongozi na utendaji kama Mtendaji Mkuu wa Chama.

“Leo labda niseme kwa sehemu mpaka wakati tunamaliza Mkutano Mkuu Maalumu ambao ulipitisha marekebisho na mabadiliko ya Katiba Ndugu Komrade Kinana alikuwa anafanya yote haya, lakini akiwa mgonjwa, akiugulia na sisi kwenye chama tuna utaratibu na tunawapenda viongozi wetu.

“Kwa hiyo ikakubalika achukue muda wa kutosha wa kuitazama afya yake nje ya nchi na kiongozi wa aina yake anaporejea, mgonjwa akitoka hospitali hakimbilii kazini au shambani moja kwa moja, inashauriwa kitaalamu atumie muda wa kupumzika ili kuimarisha afya yake.

“Na jana (juzi) nimezungumza naye anaendelea vizuri, yuko madhubuti kabisa kuliko jana, kwa hiyo nashukuru wale wote wanaofuatilia habari zetu za CCM na iwe mfano kwa vyama vingine,” alisema.   .
Wanafunzi zaidi ya 20 wanahofiwa kupoteza maisha katika ajali ya basi iliyotokea wilayani Karatu leo asubuhi.
Habari zinaarifu kuwa , basi hilo limeanguka kabla ya kuingia karatu mjini na kuua watoto wengi .
Inaarifiwa kuwa Wanafunzi hao  ni wa shule inayoitwa Lucky Vicent ya Arusha ambao walikua wanaenda karatu kufanya mitihani ya mashindano na shule za karatu.
 
 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMwwTTuaqtVINgFQJD9NjZpBqHfPtqjPvogkIyna8MBoWM2ie-PoYV-YfkOmfRh7RQNhoLhnruqu95QIr6349buZ85R5f4BMLtZy_qtXKT0t3wr-zvHJRnySFoRnw6Acd2VNjbcDEwPSM3/s1600/5.jpg

wasanii msitumike vibaya

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi6jyyDE8_DpqkWbNfMKF4al1aGGUcfjqdTDyjng_elByDdA5gS3pViyNg9UDzNYwowPe88P7xMw8I-jItpYdCGN0LdQodmq8c7rEJpL81IofXwsfRFUihJ_nttW4gk6a3cfY_EgCr_NER0/s1600/1.pngMbunge wa mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), amewataka wanasiasa kutowatumia vibaya wasanii kwa manufaa yao binafsi. Amesema Bashite ni mtu aliyekataliwa na jamii, hivyo wasanii wasikubali kutumika kumsafisha.

Ameyasema hayo jana Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akisoma hotuba ya kambi rasmi ya upinzani kuhusu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Aidha, Sugu amemtaka msanii ‘Roma’ kujitokeza hadharani kusema ukweli ni kipi kilichotokea na ni nani aliyehusika katika tukio hilo la utekwaji wake na wenzie.

“Wanasiasa tunatakiwa tuwaheshimu wasanii kwani ni kioo cha jamii, kuwatumia na kuwaterekeza mtakuwa hawatendei haki,”amesema Mbilinyi.

Magazeti ya Leo jumamosi ya tarehe 06/05/2017




















Ijumaa, 5 Mei 2017

Sakata la Vyeti Feki laongeza uhaba wa watumishi katika idara mbalmbali

 
Uamuzi  wa Serikali wa kuwafukuza kazi watumishi wanaodaiwa kughushi vyeti, umezidi kuchukua sura mpya, baada ya watumishi sita wa Halmashauri ya Kilwa mkoani Lindi kufungwa jela mwaka mmoja kila mmoja kwa kosa la kughushi vyeti vya kidato cha nne na kujipatia ajira.

Taarifa nyingine zinasema Katibu Tawala wa Wilaya ya Tandahimba (DAS), Mohamed Azizi naye ameguswa na sakata la vyeti feki baada ya kutajwa katika orodha ya watumishi wenye vyeti feki akiwa namba 5356.

Chanzo cha uhakika kutoka ofisi ya DAS kimesema  kuwa, tayari kiongozi huyo ameshaondoka Mtwara kuelekea Dar es Salaam kupeleka malalamiko yake katika mamlaka za juu kwamba jina lake limeingizwa kimakosa katika orodha hiyo.

Taarifa nyingine kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini zinasema zahanati mbili zimefungwa baada ya watumishi wote waliokuwapo kukumbwa na sakata la vyeti feki.

Madereva hao, walihukumiwa jana na Mahakama ya Wilaya  ya Kilwa, baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ya kufoji vyeti vya kidato cha nne.

Hukumu hiyo, imetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo, Gabriel Ngaeje baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

Madereva waliohukumiwa ni Juma Sungura, Issa Juma Abdurahamani, Abdull Chubi, Dactuce, Ahamadi Selemani na Abdallah Kilolopera.

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Hakimu Ngaeje aliwauliza washtakiwa kama wana sababu zitakazoishawishi mahakama isiwape adhabu kali.

Kila mmoja kwa wakati wake, aliomba mahakama iwaonee huruma, kwani wana familia zinazowategemea, hivyo iwapo watapewa adhabu kali kuna hatari ya kukosa matunzo yao.

Naye mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Emmanuel Camilius aliiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watuhumiwa na watu wengine wenye tabia ya aina hiyo ndani ya Mkoa wa Lindi na Taifa kwa ujumla.

“Tabia ya aina hii si ya kuifumbia macho, kazi wanazozifanya zinahusu usalama wa watu, kugushi vyeti kwa ajili ya kujipatia ajira ni hatari,”alisema Camulius.

Hakimu Ngaeje, akitoa hukumu katika kesi hiyo namba 07/2014, alisema amesikiliza maombi ya pande zote mbili, hivyo akawahukumu kila mmoja kifungo cha nje cha miezi (12) kwa kila kosa na kufanya idadi ya miezi (196).

“Kwa vile adhabu inakwenda pamoja, mtatumikia kifungo cha nje miezi 12,”alisema.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwanasheria Camilius, kuwa  watumishi hao wakijua wanachokifanya ni makosa, walifoji vyeti vya kidato cha nne na kujipatia ajira kinyume na sheria ya nchi.

Naye Mbunge wa  Mchinga, Hamidu Bobali (CUF), alisema  zahanati mbili katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini mkoani Lindi, zimefungwa baada ya watumishi wake kutajwa katika orodha ya watumishi wa umma wenye vyeti feki.

Bobali alitoa taarifa hiyo bungeni mjini Dodoma  jana, alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwa mwaka wa fedha 2017/18.

“Mheshimiwa mwenyekiti, hili suala la vyeti feki limeleta shida katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini kwa sababu kuna zahanati mbili zimefungwa, baada ya watumishi wake wote kubainika wana vyeti feki.

“Kwa hiyo, namwomba mheshimiwa waziri, achukue hatua haraka,” alisema Bobali wakati alipokuwa akihitimisha mchango wake.

Pamoja na kusema hayo bungeni, nje ya bunge Bobali alisema a zahanati zilizofungwa ziko katika Jimbo la Mtama katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini.

“Zahanati zilizofungwa ni za Mkanga 2 na Sudi ambazo zote ziko pembezoni kabisa ya mji, kiasi kwamba kitendo cha kuzifunga, kitaathiri mno wananchi.

“Kwa hiyo, ndiyo maana nilimwomba mheshimiwa waziri afanye kila analoweza kuhakikisha zinafunguliwa haraka ili kunusuru maisha ya wananchi,”alisema Bobali.

Kwa mujibu wa Bobali, zahanati hizo zilikuwa na watumishi watatu watatu kila moja.

Taarifa zaidi kutoka Lindi, zinasema watumishi  236 wa Serikali wamegundulika kutumia vyeti feki.

Katika sakata hilo, halmashauri za wilaya za Nachingwea na Kilwa zinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mkoa  wa Lindi, Godfrey Zambi alizitaja wilaya na idaidi ya watumishi kwenye mabano, kuwa ni Nachingwea (72), Kilwa (53), Ruangwa (45),Lindi Vijijini (25), Ofisi ya Katibu Tawala (RAS) (23), Manispaa (11) na Liwale (7).

Alisema  katika idadi hiyo, idara za afya na elimu  zinaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watumishi wa vyeti feki.