Alhamisi, 6 Julai 2017
Jumatano, 5 Julai 2017
Jumanne, 4 Julai 2017
Mbunge CCM ( Juliana Shonza ) nusura achapane na wabunge wa Chadema
Wabunge
wa Chadema jana walipambana kwa maneno na mbunge wa viti maalumu (CCM),
Juliana Shonza, ambaye baadaye alienda polisi kuripoti sakata hilo.
Wabunge
hao walidai Shonza aliwatukana kwa kuwaita wapumbavu baada ya kumwambia
kuwa anachokifanya bungeni, hasa kuwasilisha mapendekezo ya adhabu
dhidi ya wabunge wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda
Mjini) ni chuki binafsi ya kuondoka upinzani.
Mzozo
huo ulizuka jana mara baada ya kikao cha mchana wakati wabunge wa Ukawa
wakisubiri kukaguliwa kuingia jengo la utawala kwa ajili ya kikao chao
na waandishi wa habari.
Shonza, ambaye aliwahi kuwa mwanachama wa Chadema, alikuwa akitoka jengo la utawala na kukuta wabunge hao wakisubiri ukaguzi.
Mbunge
huyo alisikika akisema, “hamuwezi kunipangia cha kusema, kwa sababu
hamkunileta bungeni,” huku akimfuata kwa karibu mbunge wa Ubungo
(Chadema), Saed Kubenea. Sekunde chache baadaye, Shonza alisikika
akisema “mnataka kunipiga” (huku akielekeza mkono kwa Suzan Kiwanga
(mbunge wa Mlimba, Chadema), ambaye alisikika akimtaka Shonza amtaje
aliyetaka kumpiga.
Baadaye wabunge wa upinzani walisikika wakihoji sababu za Shonza kuwatukana.
“Wengine hapa sisi ni mama zako,” alisikika Suzan Lyimo (viti maalum, Chadema).
Hata
hivyo, baadaye wabunge wa CCM waliokuwa jirani walisogea na kumsihi
Shonza kuachana na ugomvi huo, lakini mbunge huyo aliendelea kuwa eneo
hilo, lakini baadaye walimchukua na kwenda naye jengo la Pius Msekwa.
Wakati wakiondoka naye, Pauline Gekul (Babati Mjini, Chadema), alimtaka Zainabu Vullu (viti Maalumu (CCM), kumfunda mbunge wao.
Alipoulizwa
chanzo cha ugomvi huo, Kubenea alisema Shonza aliwatukana kwa kuwaita
“wapumbavu” baada ya Joseph Selasini (Rombo, Chadema) kumwambia Shonza
anachokifanya bungeni ni chuki.
Spika
Job Ndugai alisema baadaye kuwa alipata taarifa za tukio hilo na
kumshauri Shonza aliripoti polisi kwa kuwa ni la jinai na kwamba
atawafikisha wabunge nane mbele ya Kamati ya Maadili kwa hatua zaidi.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa, Ernest Kimola alisema suala hilo limefunguliwa jalada la shambulio la kudhuru.
“Hatua
inayofuata baada ya kuletwa kwa taarifa hii ni kuwatafuta wahusika ili
tuweze kupata taarifa ya upande wa pili,” alisema Kamanda Kimola.
Credit: Mwananchi
Credit: Mwananchi
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)