Jumanne, 9 Januari 2018
Jumatatu, 8 Januari 2018
Matokeo ya darasa la nne na kidato cha pili yatangazwa. Bofya Hapa Kuyatazama
Baraza
la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji
wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 22 na 23 mwaka
jana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifanya vyema katika mitihani
hiyo.
Akitangaza
matokeo hayo leo Jumatatu Januari 8, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk
Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani
wa darasa la nne wamefaulu kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo.
Amesema
wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D
wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja
E, ambao ni ufaulu usioridhisha.
Kuhusu
matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde amesema jumla ya
wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa
kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea
na kidato cha tatu.
Dk
Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili 51,807 sawa na asilimia
10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha
tatu.
Alhamisi, 4 Januari 2018
Mke wa Kingunge afariki dunia mumewe akiwa amelazwa
Mke
wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Peras Kingunge
amefariki dunia leo Alhamisi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mtoto
wa Kingunge, Kinje Ngombale amethibitisha taarifa hizo na kwamba kifo
cha mama yake kimetokea wakati baba yake pia ni mgonjwa.
"Ni
kweli mama amefariki na baba amelala kwa sababu ndio kwanza ametoka
chumba cha upasuaji aling'atwa na mbwa. Tutamwambia akiamka," amesema
Jumatano, 3 Januari 2018
Taarifa Kutoka Mamlaka Ya Mapato TRA
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imefanya mabadiliko ya ulipaji kodi kwa
wafanyabiashara wadogo ambao watalipa robo ya kwanza ya malipo ndani ya
siku 90 badala ya njia ya awali ya kufanyiwa makadirio.
Mabadiliko
hayo yatawasaidia wafanyabiashara kuanzia waliposajiliwa tofauti na
utaratibu uliokuwepo wa kulipia kodi hiyo hata kabla mfanyabiashara
hajaanza kufanya biashara.
Hayo
yameelezwa leo Januari 2 na Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Elijah
Mwandumbya wakati wa kuzindua kampeni ya usajili wa walipa kodi ambapo
amesema wanatarajia kusajili walipakodi wapya milioni moja kwa mwaka
2017/2018.
Mwandumbya
amesema TRA hawana wakala yeyote aliyepewa jukumu la kusajili au hata
kutoa fomu ya usajili hivyo amewataka wananchi wajihadhari na vishoka
ambao watatumia mwanya na kuharibu kampeni hiyo.
"Hatuna
mtu yeyote hivyo ni wazi kupitia vyombo vya habari wananchi wanatakiwa
kuwa makini kwani usajili utafanyika katika ofisi za TRA na katika vituo
maalumu," amesema Mwandumbya.
Amesema kampeni hiyo na mabadiliko hayo yamekuja kwa nia ya kuongeza hamasa kwa wananchi ili wawe na utaratibu wa kulipa kodi.
Mwandumbya ameendelea kusisitiza azma ya serikali kukusanya kodi na kukuza uchumi wa viwanda na kuleta maendeleo kwa Taifa.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)