nikiwa nimekaa leacture room
nikimuangalia msichana aliyekaribu yangu,niliyekuwa nikimuita
"Bestfriend"nilikuwa nikimuangalia nywele zake nzuri na sura yake ya
upole huku nikitamani awe wangu,lakini yeye hakuwa akitamani hilo na nilikuwa nikilitambua hilo.
Baada ya leacture,alikuja kwangu na kuniomba notes za siku ya nyuma kwa
sababu hakuweza kuingia darasani hiyo siku iliyopita.baada ya kumpa
akasema "asante" na kushikana mikono na mimi.I wanted to tell her,i want
her to know that i don't want us to be just friends,i love her but i'm
just to shy,and i don't know why
2nd year
Simu yangu
iliita,kupokea alikuwa yeye alikuwa akilia akinielezea jinsi gani
boyfriend wake broke her heart,she asked me to come over because she
didn't want to be alone,kwa kuwa ni rafiki yangu kipenzi ilinibidi
kwenda kumfariji,as i sat next to her on the sofa,nilikuwa nikimuangalia
Machoni nikitamani awe wangu.Baada ya masaa mawili baada ya kuangalia
nae movie mbili tatu na kula nae chakula pamoja akarudi katika hali yake
ya kawaida,hivyo akaamua kwenda kulala,before akaniangalia na kuniambia
"asante" na kunipa tabasamu tamu,i want to tell her to know that i
don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont
know why.
3rd year
Siku moja kabla ya Tamasha la
muziki chuoni alikuja kwenye meza yangu leacture room na kuniambia
"Boyfriend wangu amepata udhuru hivyo naomba unipe campan katika tamasha
la muziki leo usiku" kwa kuwa tuliwekeana promice kwamba ikitokea kila
mmoja wetu amekosa mtu wa ku-date nae basi tutaenda pamoja just as
"bestfriends".hivyo tukaenda. katika tamasha baada ya kila kitu
kuisha na muziki kufungwa,nilikuwa nimekaa nje ya ukumbi nikimuangalia
jinsi alivyokuwa akicheka na rafiki zake,she saw me looking to her she
smiled at me,i want her to be mine lakini yeye alikuwa hafikirii hilo
kabisa na nilikuwa nikilitambua hilo,then she said to me "nimekuwa na
muda mzuri na wewe asante sana" and she gave me a sweet smile.I want to
tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm
just too shy,and i dont know why.
Graduation Day
siku,wiki kisha mwezi ukapita ilikuwa ni mahafali yetu tukimaliza masomo
ya chuo,akiinuka kwenda kutunukiwa shahada yake ya uchumi nilikuwa
nikimuangalia akiwa amependeza sana siku ile,i wanted her to be mine,but
she didn't notice me like that,and i knew it. kabla watu
hawajatawanyika kwenda makwao,alikuja kwangu akiwa na vazi lake la
mahafali,na kulia pale nilipomkumbatia akainua kichwa chake na kuniambia
"you are my bestfriend asante sana" i want to tell her to know that i
don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont
know why.
Miaka michache baadae
Nikiwa kanisani Yule
Msichana akiwa anaolewa sasa,nilimuangalia akisema "ndiyo nakubali " and
drive off to new life,kaolewa na mwanaume mwingine,i wanted her to be
mine,but she didn't see me like that,and i knew it. but before she
drove away,alikuja kwangu na kusema "asante sana" and kissed me on the
cheek.I want to tell her to know that i dont us to be just friends,i
love her but i'm just too shy,and i dont know why.
Kwenye Mazishi
Miaka ilipita i looked down katika jeneza lilokuwa na msichna ambaye
alikuwa ni "bestfriend" wangu,Katika Service ya mazishi wakasoma diary
ya Bestfriend ambayo alikuwa akiiandika enzi za maisha ya chuo'
Diary yake ilikuwa Ilikuwa ikisomeka hivi
I stare at him napenda awe wangu,but he doesn't notice me like that,and
i know it,i want to tell him,i want him to know that i dont want us to
be just friends,i love him but i'm just to shy,and i dont know why.I
wish he would tell me he loved me!
Nilipiga magoti huku nikilia
nikijisemea moyoni i wish ningemwambia tu ukweli,nimeshachelewa sipo
nae tena katangulia mbele za haki i cried!!
KAMA Mzazi inapenda kuanza mwaka huu mpya wa 2016 kwa kuwapongeza
wote waliobahatika kwa mapenzi ya aliyetuumba kuwa hai na salama na
kuendelea kuomba Mungu awalinde kwa mwaka huu tangu mwanzo hadi mwisho
wake.
Tunawajibika kushukuru kwa sababu kuna wenzetu hawakubahatika kuuona
mwaka huu kutokana na sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wetu. Lakini
kubwa kwa Januari hii ya 2016 ni zawadi ya Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa wazazi na walezi kwa kuanzisha
elimumsingi bila malipo kwa vitendo.
Elimumsingi inajumuisha elimu ya awali,ya msingi na sekondari, kuwa
bure kwa gharama za serikali kwa shule za ngazi hiyo zinazomilikiwa na
serikali ispokuwa shule 11 tu nchi nzima. Hongera sana serikali ya Rais
Magufuli kwa kuishi kwa vitendo.
Kwa mujibu wa waraka wa serikali uliotolewa katikati ya Desemba mwaka
jana, uliainisha wazi majukumu ya serikali katika utekelezaji wa
elimumsingi bila malipo lakini pia ulioanisha majukumu ya wazazi katika
utekelezaji wa jambo hili ili watoto waweze kusoma bila kupata
changamoto zisizo za lazima.
Kama Mzazi nataka kuwakumbusha majukumu ya wazazi na walezi katika
utekelezaji wa jambo hili kwani yale ya serikali, yenyewe inayajua
vilivyo na tayari imeshaanza kutekeleza kwa kutenga fedha za kugharimia
elimu hiyo.
Wazazi na walezi kwa mujibu wa waraka wa serikali wanatakiwa kununua
sare za shule na vifaa vya michezo,vifaa vya kujifunzia ikiwa ni pamoja
na daftari na kalamu, vifaa vya usafi binafsi, chakula kwa wanafunzi wa
kutwa na bweni na gharama za matibabu.
Gharama nyingine kwa wazazi na walezi ni kulipia nauli ya kwenda na
kurudi shule kwa wanafunzi wa kutwa na wanafunzi wa bweni kwa wakati wa
likizo, kununua magodoro, shuka na vifaa vya usafi.
Ili kuhakikisha kwamba hayo yanafanyika bila kuleta manung’uniko kwa
kutumbukiza gharama zisizokuwemo katika orodha hiyo, wazazi na walezi
wanatakiwa kukemea na kutoa taarifa kwa vyombo husika juu ya mienendo
inayokwenda kinyume na utaratibu wa elimumsingi bila malipo.
Kwa uhalisia wake kila mzazi na mlezi anatakiwa kuwa macho kwa kuwa
msimamizi wa utekelezaji wa sera hiyo ya serikali ya elimumsingi bila
malipo huku watoto wakibakiwa na jukumu la kusoma kwa bidii na uwezo
waliojaliwa kwa ajili ya kujipatia ufunguo wa maisha yaani elimu.
Visingizio na figisufigisu zisipewe nafasi katika hili ili tuweze
kunufaika vilivyo.
Visingizio vya watoto kutokwenda shule kwa sababu ya wazazi au walezi
kushindwa kumlipia ada mwanafunzi katika ngazi hizo tatu visipewe
nafasi kama ilivyokuwa kabla ya utaratibu huu mpya. Kila mmoja wetu,
hususan ni wazazi na walezi wajiandae kwa gharama zilizoorodheshwa ili
watoto wetu wote waingie madarasani kwa kazi moja ya kujifunza. Hapa
Kazi Tu sasa!
WAZIRI
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako ametoa siku saba kwa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
limpe sababu za kubadili mfumo wa utunuku viwango vya ufaulu wa awali(
Division) na kwenda wa wastani wa pointi (GPA) unaotumika sasa Kidato
cha Nne na Sita.
Aidha, ametaka litoe maelezo ya kitaalamu juu ya sababu za kuanzisha
mtihani wa pili kwa watahiniwa wa kujitegemea na kwamba zisipomridhisha,
mwaka huu wasifanyishwe mtihani huo.
Mfumo wa GPA ulianza kutumika kwa wanafunzi waliofanya mtihani wa mwaka
2014 ambao matokeo yao yalitoka mwaka jana.Vile vile mitihani miwili kwa
watahiniwa wa kujitegemea, ilianza mwaka 2014 na 2015.
Ndalichako ambaye aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa baraza hilo kwa miaka
tisa, alitoa maagizo hayo jana ambako pamoja na masuala mengine,
alishuhudia namna alivyojaribiwa na kuletewa vishawishi jambo ambalo
alisema, alilishinda kwa kusimamia taaluma.
Maagizo hayo aliyatoa alipotembelea na kuzungumza na viongozi,
wafanyakazi wa NECTA ambako hakuridhishwa na maelezo yaliyotolewa na
Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde.
Alisema tangu alipoteuliwa kuwa Waziri, amepokea malalamiko mengi kutoka
kwa wadau wa elimu na wananchi juu ya mfumo wa sasa wa upangaji matokeo
wa GPA ambao umekuwa haueleweki na kwamba hawakushirikishwa katika
mabadiliko hayo.
“ Nataka nijue sababu za kitaalamu za kubadilisha mfumo wa upangaji wa
matokeo kutoka kwenye ule wa Division (madaraja) kwenda kwenye ule wa
GPA na kama huo mfumo una tija kwa elimu yetu,” alisema.
Awali , Dk Msonde alisema mfumo huo ulipitishwa baada ya vikao kati
yake, Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Baraza la Vyuo vya Ufundi (Nacte) na
Wizara.
Alisema baraza lilitakiwa kuendesha mfumo huo ili kwenda na mifumo
mingine ya elimu ya juu katika kurahisisha udahili wa wanafunzi kwenda
sanjari na mfumo wa serikali mtandao na ajira.
Watahiniwa kujitegemea
Kuhusu uanzishwaji wa mtihani wa pili kwa watahiniwa wa kujitegemea,
Ndalichako alisema, “Nataka sababu za watahiniwa wa kujitegemea kupewa
mtihani wa pili ambao unachukuliwa kama alama upimaji endelevu kwa
mwanafunzi.
“ Kama baraza ambalo ndio wataalamu, mnasema mmeamua kutoa mtihani wa
pili kutokana na kupokea malalamiko ya kufeli na mtihani mgumu, basi
hatuwezi kuendelea nao, nataka nipate sababu za kitaalamu na kama sababu
haziridhisha basi mwaka huu wasifanyishwe mtihani wa pili,” alisema.
Alisema kwa kawaida, mtihani wa pili kwa watahiniwa wa kujitegemea
hauwezi kuwa mbadala wa alama endelevu kwa wanafunzi. Alisema unaongeza
mzigo kwa watahiniwa na gharama za kulipa wasimamizi na wasahihishaji wa
mitihani hiyo.
Ashuhudia alivyojaribiwa
Ndalichako aliwataka viongozi wa baraza hilo kutokukurupuka katika kutoa
uamuzi na kufanya mabadiliko yasiyo na tija kwa taifa. Badala yake,
alisisitiza watumie utaalamu wao kushauri na kukataa maagizo yasiyo na
tija kusaidia katika kuboresha elimu.
Katika hatua nyingine, Ndalichako aliwataka watendaji wa Baraza hilo
kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu na kuepuka vishawishi. “ Baraza
la Mitihani ni sehemu ngumu sana, hasa kutokana na kuhudumia watu na
hasa katika suala zima la mitihani.
"Na ni eneo ambalo lina vishwishi vingi, hata mimi nilijaribiwa kuletewa
vishawishi lakini nilisimama misimamo ya taaluma,” alisema.
Ndalichako pamoja na kuwapongeza Baraza kwa kutoa vyeti mbadala, ametaka kuwa makini katika suala hilo kuzuia udanganyifu.
Alisisitiza watoe tathmini ya kina katika matokeo ya wanafunzi ambayo
yatasaidia wizara kufanya uboreshaji. “Nilipokuwa hapa, kuna wakati
nilikuwa nakosa usingizi linapokuja suala la kutangaza matokeo, unakuta
matokeo ya wanafunzi 30 yote ni mbaya, sasa hapa si kuwa wanafunzi wote
walikuwa hawafundishiki ila kuna tatizo la ziada, na hilo ndio
tunatakiwa kushughulikia,” alisema.
Alisema, “ Nilikuwa naumia sana na ubora wa elimu iliyokuwa ikitolewa
kwa baadhi ya shule, sasa nimepewa kazi ya kuhakikisha elimu inakuwa
bora, tunaondoa watu wa kuchora mazombi na ule wakati wa shule kugeuka
vituo vya kulelea watoto badala ya kutoa elimu umefika mwisho.”
KOCHA wa timu wa Yanga, Hans Van Pluijm amesema kuwa ameridhishwa na
kiwango kinachoendelea kuoneshwa na wachezaji wake katika michuano ya
Kombe la Mapinduzi mjini hapa.
Yanga imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kumaliza michezo ya
makundi wakiwa na pointi saba na kushika nafasi ya kwanza katika msimamo
wa kundi A huku Mtibwa Sugar ikishika nafasi ya pili ikiwa na pointi
nne.
Akizungumza baada ya kumaliza mchezo baina yake na Mtibwa, Pluijm
alisema kuwa wachezaji wake wanacheza kwa jinsi alivyowaelekeza.
“Naridhika na kiwango chao hasa kwa vile wanafuata maelekezo yangu na
wanacheza vile ninavyotaka wacheze,”alisema.
Hata hivyo, alisema kuwa mashindano hayo ya Kombe la Mapinduzi ni
mazuri kutokana na kuwa na ushindani ambao unazidi kuongeza uimara wa
timu yake. Katika mchezo huo, Yanga ilishinda mabao 2-1 na mabao yake
yalifungwa na Yussuf Abubakar dakika ya 42 na Mwalimi Busungu dakika ya
82, wakati lile la Mtibwa lilifungwa na Shiza Kichuya katika dakika ya
10. I