Waziri wa TAMISEMI amesema ajira mpya za walimu mwaka huu zitatoka pale bajeti hiyo itakapopitishwa ili kuepuka usumbufu ameyasema hayo alipokuwa katika mahojiano na clouds tv leo tar 30/03/2016
Jumatano, 30 Machi 2016
Breaking news: Ajira za walimu kutolewa baada ya bajeti kupitishwa
Waziri wa TAMISEMI amesema ajira mpya za walimu mwaka huu zitatoka pale bajeti hiyo itakapopitishwa ili kuepuka usumbufu ameyasema hayo alipokuwa katika mahojiano na clouds tv leo tar 30/03/2016
Jumamosi, 26 Machi 2016
Kificho ang’oka uspika
Badala yake wajumbe wateule wa Baraza la Wawakilishi, wamemchagua Zubeir Ali Maulid, kuwa Spika mteule wa baraza hilo, baada ya kupata kura 55 na kumuacha kwa mbali Kificho aliyeambulia kura 11 katika uchaguzi uliofanyika jana katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar.
Aidha katika uchaguzi huo ambao wawakilishi 72 walipiga kura, Janeth Nora Sekihola ambaye ni hakimu mstaafu akipata kura 4 wakati kura mbili ziliharibika.
Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuangushwa katika uchaguzi huo, Kificho alisema amekubali kushindwa na yupo tayari kutoa ushirikiano akitakiwa kufanya hivyo.
“Hiyo ndiyo demokrasia, nimekubali kushindwa na nipo tayari kutoa ushirikiano mkubwa nikitakiwa kufanya hivyo kwa sababu ni ukweli kwamba ninao uzoefu mkubwa katika nafasi hiyo kwa zaidi ya miaka 20,” alisema.
Naye Spika mteule wa baraza hilo, Maulid alisema anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuleta maendeleo na mabadiliko makubwa katika chombo hicho ambacho ni moja ya mihimili ya dola katika utekelezaji wa majukumu yake.
Amesema atatumia uzoefu alioupata kufanya kazi katika taasisi za kutunga sheria, kwa ajili ya kuleta mabadiliko hayo kwa kuhakikisha kwamba Baraza la Wawakilishi linafanya kazi inayotakiwa ya kuisimamia Serikali kwa mujibu wa Katiba.
“Nimekuwa Mwakilishi Shauri Moyo na Waziri mwaka 2000, pia nimekuwa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa miaka miwili na nusu kwa hivyo uwezo wa kufanya kazi katika mabunge ya Jumuiya ya Madola ninao mkubwa,” alisema.
Aliwaomba wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wateule kumpa kila aina ya ushirikiano utakaomwezesha kutekeleza na kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba, kwani chombo hicho ni moja ya mihimili ya dola.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliozungumza na gazeti hili, wamesema kwamba mabadiliko hayo ni ishara na ujumbe tosha kwa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kwamba wawakilishi wanataka mabadiliko makubwa kwa Serikali kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.
“Mabadiliko makubwa tuliyoyafanya sisi wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kumchagua Zubeir Ali Maulidi kuwa Spika mteule mpya, ni dalili tosha kwamba sasa tunataka mabadiliko makubwa ndani ya Serikali kwa kuwa na viongozi watakaowatumikia wananchi moja kwa moja,” alisema Rashid Ali Juma mwakilishi mteule wa jimbo la Amani.
Kificho ameweka historia kuwa Spika wa Kwanza katika Baraza la Wawakilishi la mfumo wa vyama vingi kuanzia mwaka 1995, ambapo kabla ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo, alikuwa mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi kuanzia 1988.
Zubeir Ali Maulid mwaka 2000 alichaguliwa kuwa Mwakilishi wa Shauri Moyo kwa tiketi ya CCM na kuteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, chini ya Serikali ya Rais mstaafu Amani Abeid Karume, ambapo alidumu katika wadhifa huo kwa miaka mitatu.
Mwaka 2005, Zubeir alichaguliwa kuwa Mbunge wa Kwamtipura kwa tiketi ya CCM ambapo akiwa bungeni katika kipindi cha miaka miwili na nusu, alikuwa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na kuongoza vikao mbali mbali kwa kusaidiana na spika na naibu spika.
Katika hatua nyingine, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, amemteua Said Hassan Said, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Uteuzi huo ndio wa kwanza kufanyika, tangu Rais Shein alipokula kiapo cha kuongoza Zanzibar kwa miaka mitano ijayo Alhamisi ya wiki hii.
Jumanne, 22 Machi 2016
Ukawa kidedea Umeya wa jiji la Dar es Salaam
by kikoti blog
Mhe. Issaya Mwita (mbele) ambaye hadi sasa vyanzo vya ndani kutoka uchaguzi huo ameweza kupata kura 84 dhidi ya mshindani wake kutoka CCM ambaye alipata kura 67 huku kura 7 zikiharibika, hivyo kuibuka na ushindi wa Umeya wa Jiji. (Picha ya Maktaba).
UCHAGUZI
wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam ambao unaendele kufanyika muda huu
katika ukumbi wa Kareemjee taarifa za ndani kutoka katika uchaguzi huo
zimeeleza kuwa mgombea wa vyama vya UKAWA, kupitia chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Mh. Isaya
Mwita ameibuka kidedea kwa kupata kura 84 huku CCM wao wakipata kura 67
na kati ya jumla ya kura hizo 7 ziliaribikaambapo jumla ya kura za
wajumbe wote ni 158.
Hali
ilivyo muda huu ndani ya uchaguzi huo wa Umeya wa Jiji la Dar es Salaam
muda huu leo Machi 22.2016, ambapo UKAWA wameibuka kidedea
Mhe. Issaya Mwita (mbele) ambaye hadi sasa vyanzo vya ndani kutoka uchaguzi huo ameweza kupata kura 84 dhidi ya mshindani wake kutoka CCM ambaye alipata kura 67 huku kura 7 zikiharibika, hivyo kuibuka na ushindi wa Umeya wa Jiji. (Picha ya Maktaba).
Jumatatu, 21 Machi 2016
walimu wapya kwa mwaka 2016 wapewa mtihani na TAMISEMI
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, George Simbachawene ametangaza leo
March 21, 2016 kuwashughulikia wale wote wanaofanya hujuma katika sekta
ya elimu nchini, wakiwemo Walimu wanaokimbia sehemu zao za kazi hususani
vijijini na kukimbilia mijini.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo March 21, 2016 alisema…‘Katika
eneo la upangaji wa Walimu ni tatizo kubwa na nadiliki kusema hadharani
kwamba upangaji wa walimu kwenye shule zetu ni wa ovyo leo hii
tunaupungufu wa ualimu kwenye vijiji kwa asilimia zaidi ya 40% na
ongezeko la walimu mijini ni kama asilimia 50% kwa maana ya kwamba
walimu wengi wapo Dar es Salaam, walimu wengi wapo kwenye miji mikubwa
makao makuu ya mikoa na makao makuu ya wilaya’ – George Simbachawene
‘Hata
wanawake wanasema wanafuata wanaume zao huko ni kukosa uzalendo kama
ulikubali kuajiliwa lazima ukubali kufanya kazi mahala popote pale na
watanzania ni wote mpaka waliopo kule vijijini haiwezekani kukubali kazi
mjini na kukataa kijijini’ – George Simbachawene
kwa tafsiri hii ya waziri wa TAMISEM hakutokuwa na sababu zzisizona msingi zitakazokubalika kwa walimu wapya kwa mwaka 2016
Jumapili, 20 Machi 2016
TATIZO LA MAJI KATIKA MJI MDOGO WA ILULA KUISHA KABLA 2020
MBUNGE
wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto ameahidi kuongozana na wazee
wa mji wa Ilula kwenda Dodoma kuonana na waziri mkuu Kassim
Majaliwa ili kumfikishia ahadi ya maji ya Rais Dr John Magufuli kwa
wananchi wa mji mdogo wa Ilula .
Huku
akiwataka wananchi wa Ilula na Nyalumbu kutomchagua mwaka 2020 iwapo
atashindwa kutekeleza ahadi ya maji katika mji huo wa Ilula ndani ya
miaka yake mitano ya ubunge.
Akizungumza
na wananchi wa kata ya Nyalumbu na Ilula wakati wa mikutano yake
ya hadhara ya kuwashukuru wananchi wake kwa kumchagua kuwa mbunge
wa jimbo hilo la Kilolo jana ,Mwamoto alisema kuwa kero ya maji
katika mji wa Ilula imekuwa ya muda murefu jambo ambalo hatataka
kuona wananchi hao wakiendelea kutabika.
Alisema
kuwa kero hiyo ya maji imeanza kuwasumbua wananchi hao toka nchi
ipate uhuru wake mwaka 1961 hadi leo wapo katika mahangaiko ya maji
na baadhi ya viongozi wameendelea kufanya udanganyifu wa mradi huo
kama ambavyo mwaka 2010 viongozi walivyomdanganya aliyekuwa
makamu wa Rais Dr Alli Mohamed Shein kwa kupelekwa kufungua mradi
wa maji ambao viongozi walimdanganya kwa kujaza maji katika tanki
hilo ili azindue mradi huo.
Hivyo
alisema udanganyifu huo hautapewa nafasi katika uongozi wake wa
miaka mitano lazima kero hiyo imalizike na wananchi hao waweze
kupata maji vinginevyo yupo tayari kuongoza wananchi wake kumzuia
waziri wa maji kupita Ilula kwenda jimboni kwake Njombe iwapo wananchi
hao hawatatimiziwa ahadi yao ya maji safi na salama .
Mbunge
huyo alisema katika kikao kijacho cha bunge kinachoanza mwezi ujao
ataomba wananchi wa Ilula na Nyalumbu kumteulia wazee watatu ama
wanne ili kwenda nao bungeni Dodoma kukutana na waziri mkuu ili
kwa ajili ya kumkumbusha ahadi ya Rais ya maji katika mji huo wa Ilula
.
Pia
aliagiza mamlaka ya maji ya mji mdogo wa Ilula kuchunguza vema mradi
wa maji uliopo kama umejengwa kwa kiwango ama chini ya kiwango maana
amesema mradi mdogo uliopo kwa sasa bado umekuwa na kero kubwa ikiwa
ni pamoja na baadhi ya maeneo kuvujisha maji huku akiwataka wananchi
kwa upande wao kutunza miundombinu ya maji.
Mbunge wa Kilolo Bw Venance Mwamoto (kushoto) akisalimiana na mmoja kati ya wazee wa mji wa Ilula aliyetoka kuchota maji
Katika
hatua nyingine mbunge Mwamoto alimshauri meneja wa maji wa IRUWASA
katika mji wa Ilula Teodolah Mvungi kuangalia uwezekano wa kuboresha
kituo cha maji eneo la Ilula ili kiweze kunufaisha wananchi wengi
na kuwa iwapo wataanza uboreshaji kwa upande wake ataunga mkono .
Dr Shein aongoza wazanzibar katika kupiga kura, Uchaguzi wa Marudio Zanzibar
Wananchi
wa Zanzibar leo wanapiga kura katika uchanguzi wa marudio baada ya
kufutwa kwa uchanguzi uliofanyika October 25,2025 kutokana na kasoro
zilizojitokeza.
Katika baadhi ya vituo wananchi wamejitokeza na zoezi linaendelea vizuri huku hali ya usalama ikiwa imeimarishwa.
Katika kituo cha shule ya sekondari Muembeladu ambayo ina vituo sita,vituo vitano vinawatu 350 na kituo kimoja kina watu 91. Akizungumza na wanahabari, msimamizi wa kituo hicho amesema zoezi la upigaji kura linaendelea vizuri katika jimbo la Jangombe .
Kwa
upande wa kituo cha skuli ya Muembeshauri nako hali ni shwari na zoezi
linaendelea vizuri ambapo katika skul hiyo vituo 11 vinatumika watu
kupiga kura.
Katika Jimbo la kikwajuni, zoezi linaendelea vizuri huku mwitikio wa watu ukiwa ni mkubwa.
Baadhi
ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wamesema zoezi hilo limekua
rahisi na la amani tofauti na taarifa zilivyokua zinasambazwa.
Mkazi
wa Muembeshauri aliyejitambulisha kwa jina la Hamidu Salum Haji ametoa
wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwani zoezi la kupiga kura
linaendelea kwa amani na utulivu.
“Ndugu zangu tusikubali kugombanishwa na watu ambao hawaitakii mema Zanzibar tusimame pamoja katika kutetea nchi yetu” amesema Haji
Wakati zoezi hilo linaendelea maduka mengi yamefunguliwa na wafanyabiashara wanaendelea na kazi kama kawaida
Rais wa Zanzibara na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohammed Shein leo amepiga kura katika kituo cha skuli ya bungi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, amepiga kura katika kituo cha skuli ya Kiembe samaki
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd amepiga kura katika kituo cha skuli ya Kitope
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, amepiga kura katika kituo cha skuli ya Kiembe samaki
Mgombea
urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar Dkt Ali Mohammed
alizungumza na wanahabari baada ya kupiga kura yake katika kituo cha
Bungi, Kibera kisiwani Unguja ambapo alisema anaamini atashinda kwa
kishindo na kuhusu kushindwa alisema tusubiri matokeo ya uchaguzi ndiyo
yataamua.
"Nimepata
nafasi ya kupiga kura kama haki yangu ya kimsingi na kumekuwa na
utulivu mkubwa kwenye zoezi hili,hali ya ulinzi imeimarishwa.
"Matumaini yangu ni kushinda kwa kishindo, kuhusu kushindwa ndugu muandishi tusubiri matokeo ndiyo yataamua".Alisema Dkt. Ali Mohammed Shein
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd amepiga kura katika kituo cha skuli ya Kitope
Jumapili, 13 Machi 2016
Dk. Vicent Mashinji ndiye Katibu Mkuu Chadema
Katika Kikao hicho cha Baraza Kuu, Freeman Mbowe alitangaza jina la Dk. Mashinji na kuungwa mkono na wajumbe wa baraza hilo, hivyo anajaza nafasi iliyoachwa na Dk. Willibrod Slaa, aliyejienguwa ukatibu mkuu wa chama hicho.Jina la Dk. Machinji halikuwa miongoni mwa wanachama wa Chadema ambao walikuwa wanatarajiwa kumrithi Dk. Slaa kwani waliokuwa wanatabiriwa kukatia kiti hicho ni Salum Ally Mwalimu, Frederick Sumaye, Benson Kigaila, John Mnyika, Dk. Marcus Albanie na Prof. Mwesiga Baregu.
Nafasi ya Katibu wa Chadema ilikuwa wazi tangu Dk. Slaa alipoondoka Chadema muda mfupi baada ya chama hicho kumpitisha Edward Lowassa aliyetokea CCM kuwa mgombea urais wa chama hicho na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Wasifu wa Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Vincent B. Mashinji
Professional experience
Clinical Advisor & TB/HIV lead
UMSOM-IHV
July 2008 – Present
ART Program Doctor/IMA team lead
IMA Worldhealth
August 2006 – June 2008 (1 year 10 months)
Medical Officer/Anaesthesiology
Regency Medical Centre
October 2005 – August 2006 (10 months)
Medical Officer
Muhimbili National Hospital
August 2003 – October 2005 (2 years 2 months)
Research Assistant
Freelance
November 2002 – August 2003 (9 months)
Intern Docor
Muhimbili National Hospital
September 2001 – October 2002 (1 year 1 month)
Education history
Open University of Tanzania
PhD
August 2010 – Present
AMREF/UCLA Anderson School
MDI Certificate
April 2010 – April 2010
Blekinge Institute of Technology
MBA
September 2007 – March 2010 (2 years 6 months)
UMSOM-IHV
IPEP Certificate
May 2008 – May 2008
Evin School of Management
Certificate in CSR
October 2005 – October 2005
Muhimbili University College of Health Sciences
MMed/Anaesthesiology
September 2003 – April 2005 (1 year 7 months)
Muhimbili University College of Health Sciences
Certificate in Research Methodology
September 2004 – September 2004
Makerere University
MBChB
October 1995 – July 2001 (5 years 9 months)
Mzumbe High School
ACSEE
July 1992 – June 1994 (1 year 11 months)
St. Pius X Seminary, Makoko
GCSEE
January 1988 – October 1991 (3 years 9 months)
Iligamba Primary School
Leaving Certificate/Primary School
January 1981 – October 1987 (6 years 9 months
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)