ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Ijumaa, 29 Aprili 2016

CAG: Walimu ‘vihiyo’ waongezeka nchini

RIPOTI ya Ukaguzi Maalumu Kuhusu Kiwango cha Ubora wa Elimu nchini inaonesha kuwa idadi ya walimu wa sekondari nchini wasio na sifa za ualimu imeongezeka kulingana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Katika ripoti hiyo iliyofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kutolewa mapema wiki hii mjini Dodoma, inaonesha kuwa idadi ya walimu hao imeongezeka kutoka walimu 963 mwaka 2014 hadi kufika waalimu 2,108 mwaka jana. Ilieleza kuwa sababu kubwa ya kuwa na walimu wasio na sifa zaidi ya moja imetokana na Ofisi ya Waziri Mkuu (wakati huo), Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kushindwa kuwa na mpango wa kuwaendeleza walimu waliowaajiri.
Ripoti maalumu hiyo ya ubora wa elimu nchini imebaini kuwa matarajio ya wengi ilikuwa ni kuona idadi ya walimu wasio na sifa ikipungua kutokana na wengi wao kustaafu na wengine wapya kuajiriwa ambao wana sifa, lakini cha ajabu idadi hiyo imeongezeka.

Magazeti ya Leo ijumaa ya tarehe 29/04/2016

Magazeti haya ya Leo yanaletwa kwako wewe msomaji Kwa hisani kubwa ya New Mwalimu Education Centre wanaotoa elimu ya tuition kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita na mtandao wa simu za mkononi wa tigo pata Facebook na Watsup ya bure 


















Alhamisi, 28 Aprili 2016

Makatibu tawala wa mikoa 10 waapishwa


Imeandikwa na Anastazia Anyimike
RAIS John Magufuli amewaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa wapya 10 walioteuliwa wiki hii tayari kuanza kazi. Makatibu hao wameapishwa jana Ikulu jijini Dar es Salaam sambamba na kula kiapo na kutia saini Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma walioufanya mbele ya Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji mstaafu Salome Kaganda.
Walioapishwa na mikoa yao kwenye mabano ni Richard Kwitega (Arusha), Selestine Gesimba (Geita), Armatus Msole (Kagera), Aisha Amour (Kilimanjaro), Zuberi Samataba (Pwani), Albert Msovela (Shinyanga), Dk Angelina Lutambi (Singida), Jumanne Sagini (Simiyu), Dk Thea Ntara (Tabora) na Zena Saidi (Tanga).

Wabunge wawinda posho mtegoni

Imeandikwa na Ikunda Erick, Dodoma.

KITI cha Spika wa Bunge kimesema ipo haja ya kufanya marekebisho ya Sheria pamoja na Kanuni ili kila mbunge apate posho kulingana na kazi aliyofanya bungeni, badala ya utaratibu wa sasa wa kuangalia mahudhurio pekee. Aidha, kimewataka wabunge kubadilika na kuacha tabia ya kuchukua posho za vikao vya Bunge bila kuzitolea jasho.
Kauli hiyo imekuja kutokana na Mwongozo ulioombwa Aprili 25, mwaka huu na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) ambaye alikitaka kiti cha Spika kutoa Mwongozo kuhusu usahihi wa wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kulipwa posho na mishahara wakati hawashiriki na kutimiza wajibu wao wa kuchangia kwenye mjadala wa Bunge la Bajeti linaloendelea katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la 11.
Bashe alisema mbunge huyo alitumia Kanuni ya 68(7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge akiomba Mwongozo wa Spika kutokana na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuamua kutoshiriki mjadala unaoendelea bungeni, lakini wabunge hao wanasaini na kulipwa mishahara na posho.

Ajira za walimu rasmi mwezi mei 2016 _ waziri mkuu aeleza

Waziri mkuu aliyasema hayo alipokuwa akihutubia bunge la bajeti
Mheshimiwa Spika, mnamo mwezi Mei 2016, Serikali inatarajia kutoa ajira za walimu wapatao 40,000 ikijumuisha wa cheti, Stashahada na Shahada ili kukabiliana na upungufu wa walimu uliopo katika shule za Msingi na Sekondari nchini. Zaidi ya shilingi bilioni 17 zitahitajika kwa ajili ya kulipa posho pamoja na nauli za walimu wapya watakaoajiriwa na kupelekwa katika halmashauri zote nchini.
Elimu ya Sekondari
Mheshimiwa Spika, OR - TAMISEMI inaendelea kusimamia utekelezaji wa Mpango
28
wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari awamu ya pili (MMES II) ili kuimarisha Elimu ya Sekondari. Lengo la mpango huu ni kuinua ubora wa elimu. Aidha, utekelezaji wa mpango huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya shule 264 za awamu ya kwanza ambao umekamilika kwa asilimia 64. Serikali inaendelea kukamilishaujenzi na uboreshaji wa shule 264 za awamu ya kwanza na kuendelea na uboreshaji wa miundombinu katika shule nyingine 528

MWENDELELEZO WA HOTUBA YA WAZIRI MKUU   


HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, MHESHIMIWA GEORGE BONIFACE SIMBACHAWENE (Mb) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
KWA MWAKA WA FEDHA 2016/17
Utangulizi
Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuiona siku ya leo tukiwa na afya njema. Kipekee kabisa napenda kumshukuru Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuniamini na kuniteua niongoze Ofisi yake kwa upande wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Vile vile, kwa namna ya pekee, namshukuru Mheshimiwa Jasson Constantine Rweikiza (Mb) Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na wajumbe wa Kamati kwa ushirikiano na maelekezo wanayotupatia katika kutekeleza majukumu yetu ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Magazeti ya Leo Alhamisi ya tarehe 28/04/2016

Headline za magazeti ya Leo zimeletwa kwenu Kwa hisani kubwa ya New Mwalimu Education centre inayopatikana ilula iringa Tanzania katika majengo ya kanisa katoriki elimu inayofundishwa ni kidato cha kwanza mpaka cha sita: muda kuanzia saa kumi mpaka saa moja jioni  Nyote mnakaribishwa  elimu ndio msingi imara