ILULA IRINGA TANZANIA

ILULA IRINGA TANZANIA
KIKOTI.COM BLOG - ILULA IRINGA TANZANIA / 0769694963 .......................................

Ijumaa, 13 Mei 2016

Magazeti ya Leo ijumaa ya tarehe 13mei 2016

Ndugu msomaji wetu usikose kipindi cha breaking news kila zinapotokea katika jina angavu La kunani kitaa























Alhamisi, 12 Mei 2016

Kitaa kunanini:Tapeli aibuka chuo kikuu cha Dar Es salaam(DUCE)

Na stanley kilangi
Picha Grace tapeli)
Katika hali isiyokuwa ya kawaida ilitokea katika chuo kikuu kishiriki cha DUCE baada ya Dada mmoja aliejulikana Kwa jina la kitapeli la Grace ambapo alijikuta akiwa katika ulinzi mkali wa polisi na walinzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam baada ya kukutwa akiwa ndani ya chuo akijihusisha na kuomba na kurubuni wanafunzi waliopo chuoni hapo
Akiongea na waziri wa ulinzi wa DARUSO- DUCE askari wa chuo hicho alidai Dada huyo amekuwa akipita getini hapo kila siku akidai anapita kuelekea nje ya geti la chuo hicho
Dada huyo alikuwa akiomba Pesa hizo Kwa wanafunzi akidai anakaa mbagala na hana uwezo wa kupata mahiji ko angehitaji msaada huo lakini Mara baada ya kufanyiwa mahojiano ya kina ilibainika kuwa dada huyo hakuwa na maisha magumu na alikuwa anaishi na mama yake katika maisha ya kawaida lakini aliamua kuwa ombaomba kutokana na faida kubwa ya kuombaomba katika vyuo vya Dar Es Salaam kikiwepo TIA na DUCE
Dada huyo aliomba msamaha na kukiri kutoridia tena. Tukio hili limetokea tarehe 02/05/2016 Ama kweli mjini shule kijijini tusheni

KUNANI KITAA

Hii ni makala maalumu ya breaking news itakayokuwa inaletwa kwenu wasomaji wetu na mwandishi wetu Stanley Kilangi kila siku  kutoka Dar Es salaam
Picha ya mwandishi wetu (Stanley Kilangi)

Mpinzani wa Museveni , Dr Kiiza Besigye Akamatwa Baada ya Kujiapisha Kuwa Rais

 
 Mpinzani mkuu wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Dk. Kizza Besigye ambaye amekuwa akipinga ushindi wa Rais huyo, amekamatwa na polisi wa nchi hiyo baada ya jana kujiapisha kuwa Rais ikiwa ni siku moja tu (leo) kabla ya Museven kuapishwa.

Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa vizuizi  vya polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha urais wa taifa hilo''.

Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana ''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa mahakama ya juu''.

Video hiyo ilisambazwa kwa kasi  kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza Yoweri Museveni kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu uliopita akiwaacha kwa mbali wapinzani wake wakuu, Kizza Besigye na Amama Mbabazi.

Kadhalika, Mahakama Kuu nchini humo ilihalalisha ushindi wa Museveni baada ya kutupilia mbali shauri la pingamizi la ushindi huo lililowasilishwa na Amama Mbabazi.

Tanzia: Msanii wa Vichekesho Mohammed Abdallah (Kinyambe) Amefariki Dunia

 
Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania kutoka katika Kundi la Vituko Show, Mohammed Abdallah ‘Kinyambe’ amefariki dunia Jumatano hii baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na uvimbe tumboni.

Taarifa za kifo chake zilianza kusambaa jana katika mitandao ya kijamii baada ya wasanii wa filamu kuanza kupost picha mbalimbali huku wakiandika RIP Kinyambe.

Mmoja kati ya wasanii wanaounda Chama Cha Wasanii Wachekeshaji Tanzania, Mkono Mkonole, amesema Kinyambe amefariki jana akiwa mkoani Mbeya.

“Kinyambe alikuwa anasumbuliwa na uvimbe tumboni kwa muda mrefu Pia watu wake wa karibu akiwemo Mke wake wanadai imetokana na kujaa Kwa maji kwenye mapafu, ila jana ndo amefariki akiwa mkoani Mbeya, katika hospitali ya mkoa wa Mbeya,” alisema Mkonole.

Kuhusu taratibu za mazishi, Mkonole amesema bado hawajapanga kwani taarifa za kifo chake wamezipokea jana usiku.

“Kusema kweli bado hatujapanga kuhusu mazishi, lakini sasa hivi tunawasiliana na ndugu zake ili kujua taratibu za mazishi na zikikamilika tutaweka wazi,” alisema Mkono.

Kinyambe atakumbukwa kwa uwezo wake wa kuigiza, hasa hasa jinsi anavyoongea pamoja na mtindo wake wa pekee wa kugeuza macho..

Mungu amlaze mahali  mahali pema peponi -Amina

Msanii Maalufu wa tasinia ya uigizaji wa comedy amefariki dunia usiku wa kuamkia Leo .Sababu ya kifo chake ikiwa bado haijajulikana ila  kifo hicho kimetokea katika hospital ya mkoa wa mbeya  .mungu amlaze mahali pema peponi kinyambe.
Mwili umechukuliwa na mazishi yake yanatarajia kufanyika Uyole mbeya


Magazeti ya Leo Alhamisi ya tarehe 12/05/2016