Jumatatu, 13 Juni 2016
Jumapili, 12 Juni 2016
Jumamosi, 11 Juni 2016
Kuhusu ajira za walimu: TAMISEMI wanena
NEW MWALIMU EDUCATION CENTRE (MADIZINI-MAJENGO YA KANISA KATORIKI)
New mwalimu education centre (NMEC) Inakualika kuwa inaendelea na kutoa huduma ya tuition, tuition kwaajili ya likizo, itakayoanza usajiri na kusoma tarehe 30/05/2016 hadi tarehe 15/07/2016 KUANZIA SAA MBILI(8:00) Mpaka saa saba(7:00) kwa masomo yote ya;
- Science (sayansi) kama mathematics, chemistry, biology, physics, Agriculture etc
- Arts (sanaa) Kama Geography, history literature in English, English etc
#Kwa kidato chasita, nne na cha pili tutafanya solving ya past paper mbalimbali za mitihani iliyopita na kufundisha namna ya kujibu mtihani wa taifa kutokana na mtaala mpya (new approach from necta)
# Pia walimu watatoa pamphlet (vitini) Kwa kile wanachofundisha Kwa kukuza uelewa
#Mwanafunzi atapewa peni bure mara tu baada ya kufanya usajiri
#Ada Kwa mwezi ni shilling 10,000/= tu.
Tunawalimu makini, wenye uwezo na uzoefu waliofanikiwa kuwa walimu bora katika ufundishaji katika jengo la mgalilwa ambapo tumehama jengo hilo.
Kwa mawasiliano zaidi piga: +255769694963 Mwal kikoti, +255757927380 mwl kilimtali, mwl eliza +255676055136 Mwl kilangi +255659726110.
Mameya wampinga Dk Mpango Kuhusu ushuru wa majengo
Uamuzi wa Serikali kuziondolea halmashauri mamlaka ya kukusanya kodi ya majengo, umeibua sintofahamu huku baadhi ya mameya wakidai ni agenda dhidi ya upinzani.
Akiwasilisha
hotuba ya bajeti ya mwaka 2016/17, Waziri za Fedha na Mipango, Dk
Philip Mpango alisema Serikali itawasilisha Muswada wa Sheria ili kodi
hiyo iwe inakusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Alisema
lengo ni kuifanya TRA kukadiria kodi ya majengo na kuyafanyia tathmini
na kupewa uwezo wa kukusanya kodi hiyo kwa kutumia utaratibu wake wa
kawaida.
Waziri
aliliambia Bunge mjini Dodoma kuwa muswada huo utaweka utaratibu wa
namna ya kuhifadhi na kuwasilisha kodi ya majengo, inayokusanywa na TRA
kwa halmashauri husika.
Hata
hivyo, utaratibu huo umepingwa na mameya wa halmashauri za manispaa na
majiji nchini na kwa siku mbili kuanzia juzi walikutana jijini Arusha na
walitarajia kutoka na azimio la pamoja kupinga suala hilo.
Habari
kutoka katika mkutano huo zinadai kuwa huenda jana hiyo saa 7:00 mchana
mameya hao bila kujali tofauti za itikadi za kisiasa, wangetoka na
tamko la pamoja kupinga uamuzi huo mahakamani.
Hata
hivyo, mameya wanaotoka katika halmashauri zinazoongozwa na madiwani
kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wameenda mbali na kudai
kuwapo agenda mahsusi ya kuua upinzani.
Meya
wa Halmashauri ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Shaban Jacob alisema
Serikali haina historia ya kurejesha kodi inazokusanya kwa niaba ya
halmashauri.
“Serikali inaposema itarejesha si kweli. Kodi ya Ardhi imekusanywa na Serikali na sisi kama Halmashauri ya Kinondoni hatukuwahi kupewa kwa miaka 10,” alisema Jacob.
“Serikali inaposema itarejesha si kweli. Kodi ya Ardhi imekusanywa na Serikali na sisi kama Halmashauri ya Kinondoni hatukuwahi kupewa kwa miaka 10,” alisema Jacob.
Meya
huyo alitoa mfano wa kodi ya majengo iliyokusanywa na TRA hadi mwaka
2013 iliporejeshwa halmashauri, kwamba kipindi chote hicho halmashauri
haikuwahi kupewa zaidi ya Sh1 bilioni.
Jacob
alisema mwaka wa fedha wa 2016/17, halmashauri yake ilipanga kukusanya
kodi ya majengo inayofikia Sh10 bilioni ambayo ndiyo kwa sehemu kubwa
ingetekeleza miradi ya maendeleo.
“TRA
haina mfumo wala watendaji kufanikisha hili. Ili TRA iweze kukusanya
Sh1 bilioni hapa Kinondoni itahitaji kuajiri vijana 5,000 kusambaza
bili, jambo ambalo hawataliweza,”alisema.
Meya
huyo alisema zipo hisia kuwa mpango huo unalenga kuzidhoofisha
halmashauri za manispaa na majiji, ambazo ziko chini ya Ukawa ili
zisiweze kutekeleza kikamilifu mipango ya maendeleo.
Vyama vilivyo chini ya Ukawa vimetwaa halmashauri za majiji ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha na manispaa ya Iringa.
Wakati
huo huo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (Alat), ambaye pia
ni Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Gulam Mkadam amesema Alat inapinga
kuipa TRA mamlaka ya kukusanya kodi za majengo.
Alisema
kitendo hicho kitadhoofisha uwezo wa mamlaka hizo kuwahudumia wananchi.
Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya, alisema uamuzi huo unaathari
mbaya, kwa vile halmashauri zilishapitisha bajeti zikitegemea fedha
hizo.
“Property
Tax (kodi ya majengo) ni chanzo kikuu cha mapato katika halmashauri
nyingi za mijini. Leo unapokiondoa chanzo hicho, hiyo miradi
itatekelezwaje? Kuna kitu kimejificha hapa,” alisema.
NEW MWALIMU EDUCATION CENTRE (MADIZINI-MAJENGO YA KANISA KATORIKI)
New mwalimu education centre (NMEC) Inakualika kuwa inaendelea na kutoa huduma ya tuition, tuition kwaajili ya likizo, itakayoanza usajiri na kusoma tarehe 30/05/2016 hadi tarehe 15/07/2016 KUANZIA SAA MBILI(8:00) Mpaka saa saba(7:00) kwa masomo yote ya;
- Science (sayansi) kama mathematics, chemistry, biology, physics, Agriculture etc
- Arts (sanaa) Kama Geography, history literature in English, English etc
#Kwa kidato chasita, nne na cha pili tutafanya solving ya past paper mbalimbali za mitihani iliyopita na kufundisha namna ya kujibu mtihani wa taifa kutokana na mtaala mpya (new approach from necta)
# Pia walimu watatoa pamphlet (vitini) Kwa kile wanachofundisha Kwa kukuza uelewa
#Mwanafunzi atapewa peni bure mara tu baada ya kufanya usajiri
#Ada Kwa mwezi ni shilling 10,000/= tu.
Tunawalimu makini, wenye uwezo na uzoefu waliofanikiwa kuwa walimu bora katika ufundishaji katika jengo la mgalilwa ambapo tumehama jengo hilo.
Kwa mawasiliano zaidi piga: +255769694963 Mwal kikoti, +255757927380 mwl kilimtali, mwl eliza +255676055136 Mwl kilangi +255659726110.
NEW MWALIMU EDUCATION CENTRE (MADIZINI-MAJENGO YA KANISA KATORIKI)
New mwalimu education centre (NMEC) Inakualika kuwa inaendelea na kutoa huduma ya tuition, tuition kwaajili ya likizo, itakayoanza usajiri na kusoma tarehe 30/05/2016 hadi tarehe 15/07/2016 KUANZIA SAA MBILI(8:00) Mpaka saa saba(7:00) kwa masomo yote ya;
- Science (sayansi) kama mathematics, chemistry, biology, physics, Agriculture etc
- Arts (sanaa) Kama Geography, history literature in English, English etc
#Kwa kidato chasita, nne na cha pili tutafanya solving ya past paper mbalimbali za mitihani iliyopita na kufundisha namna ya kujibu mtihani wa taifa kutokana na mtaala mpya (new approach from necta)
# Pia walimu watatoa pamphlet (vitini) Kwa kile wanachofundisha Kwa kukuza uelewa
#Mwanafunzi atapewa peni bure mara tu baada ya kufanya usajiri
#Ada Kwa mwezi ni shilling 10,000/= tu.
Tunawalimu makini, wenye uwezo na uzoefu waliofanikiwa kuwa walimu bora katika ufundishaji katika jengo la mgalilwa ambapo tumehama jengo hilo.
Kwa mawasiliano zaidi piga: +255769694963 Mwal kikoti, +255757927380 mwl kilimtali, mwl eliza +255676055136 Mwl kilangi +255659726110.
Juma Abdul, Telela kuwakosa Waalgeria
Hata hivyo wachezaji wapya wa timu hiyo, mabeki Hassan Kessy kutoka Simba, Vicent Andrew ‘Dante’ kutoka Mtibwa na Juma Mahadhi kutoka Coastal Union ni miongoni mwa nyota watakaokuwemo katika msafara huo.
Meneja wa timu ya Yanga, Hafidh Saleh alisema jana kuwa wachezaji hao wameachwa kutokana na sababu mbalimbali. “Juma Abdul ni majeruhi, hivyo hatoweza kwenda, Telela yeye mkataba wake umeisha na mpaka sasa uongozi bado haujamuongezea,” alisema Meneja huyo.
Hata hivyo,Telela inadaiwa tayari amefanya mazungumzo na timu za Simba na Azam kwa nia ya kumsajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi. Kwa mujibu wa Saleh, wachezaji Mahadhi, Dante na Kessy watakuwepo kwenye msafara huo na kwamba wanaamini timu yao itaenda kufanya vizuri ugenini.
Alisema mara baada ya mchezo na MO Bejaia watarejea Uturuki kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na watarejea nchini siku mbili kabla ya mchezo huo.
Yanga imepangwa Kundi A katika michuano hiyo na TP Mazembe ya DRC, Mo Bejaia ya Algeria na Modeama ya Ghana na itaanza ugenini nchini Algeria wiki ijayo. Kwa upande wa Kundi B zipo timu za Kawkab Athletic, Fath Union Sports zote za Morocco, Etoile du Sahel ya Tunisia na Ahly Tripoli ya Libya.
Amuua mkewe, achoma moto nyumba mbili
Mrimi amelazwa katika Hospitali ya wilaya Tarime akiwa chini ya ulinzi mkali. Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, ACP Andrew Satta alisema kuwa tukio hilo la mauaji lilifanyika June 8, mwaka huu katika kitongoji cha Nyabirama, kijiji cha Matongo Nyamongo baada ya kutokea ugomvi kati ya mke na mume.
Alisema Mrimi alikuwa akimtuhumu mke wake Maria kuwa anamloga na kushiriki katika mambo ya kishirikina lakini mke alikuwa akikana tuhuma hizo. Kamanda Satta alisema wakati wakigombana mtuhumiwa Mrimi alikuwa na panga mkononi ndipo alipomkata shingo mkewe na kuacha panga limeninginia na kisha kuchoma nyumba zao mbili zilizokuwa zimeezekwa kwa nyasi.
Thamani ya nyumba hizo na mali zilizoteketea hazikuweza kufahamika mara moja. Alisema wananchi ambao ni wakazi wa kitongoji hicho cha Nyabirama walisikitishwa na kitendo hicho na kuamua kupiga yowe na kumkamata mtuhumiwa na kuanza kumshambulia kwa mawe hadi alipookolewa na polisi waliofika mapema eneo hilo na kumchukua kwa gari akiwa hajitambui.
Kamanda Sitta alisema mtuhumiwa huyo alikimbizwa hospitalini hapo kwa matibabu zaidi na yupo chini ya ulinzi wa Polisi hadi sasa na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Kituo cha Afya Nyamongo kwa uchunguzi zaidi wakati ukisubiri kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya maziko.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)